skip to Main Content
The Quest For BERMUDA RICHIES, Ujue Mchezo Wa JOHN HUNTER!
Bermuda-richies

The Quest for BERMUDA RICHIES, Ujue mchezo wa JOHN HUNTER!

Natumai wadau wetu mu wazima na mnaendelea vizuri na mihangaiko ya kujitafutia riziki. Kama ilivyo ada yetu SportPesa leo tunawaletea mchezo wa John Hunter and The Quest for Bermuda Rich. Kama ambavyo jina la mchezo linavyo jieleza, mchezo huu umetengenezwa ukiangalia maudhui ya mtu ambaye ndiye john akiwa na kiu ya kupata utajiri wa Bermuda.

Mchezo huu wa Quest for Bermuda Rich unatumia maduara (Reel) 7 yenye mashimo 7 pia. Kwa kifupi kila duara, kwenye mchezo huu nisawa na mizunguko toka juu kwenda chini. Baadhi ya alama zinazoonekana katika mchezo huu zinawakilisha malipo madogo, malipo ya kati na malipo makubwa.

Alama nyingine kama ya kichwa cha mtu cha kuchonga chenye maandishi ya WILD inamaanisha thamani ya ziada katika mchezo huu, huku picha ya mtu mwenye kofia ya safari ni alama yenye maandishi Scatter, ikimaanisha itokeapo inakupa michezo ya ziada ama nyongeza (Re Spin)

Alama kuu zinazoonekana kwenye mchezo huu ni pamoja na makasha ya pesa aina za sarafu, picha ya kinubi, kikombe cha dhahabu, alama ya shupaza yenye kito cha almasi ya bluu, alama ya kisu na mavi kama za mchezo wa karata zenye vito vya almasi, na pete ya dhahabu yenye nakshi za kungáa.

x -Facebook-Instagram-post-with-logoAlama hii ya makasha ya sarafu zipo za aina nne. Alama hii inatumika pale muda wa malipo katika mizunguko yako unapowadia. Sasa swali la muhimu linajitokeza, alama hizi zinafanayaje kazi katika mchezo huu.

Alama ya jumla ni ya makasha ya sarafu. Alama hii inapatikana pale mizunguko inapokuwa inachezwa kumaanisha mizunguko ikiwa hai, na pia inaweza kujitokeza katika maduara yote 7.

Pili makasha haya yanamaanisha malipo na makusanyo. Wakati mchezo ukiwa unaendelea ukafanikiwa kupata malipo kupitia alama nilizozitaja hapo juu, (shupaza, kisu, kikombe, pete, na mavi), basi kutegemeana na thamani ya kila alama iliyo husika katika mzunguko ulio hai, moja kati ya makasha manne litaambatana na alama zilizolipa ikimaanisha umepata pesa.

Hapa lazima niwaeleze kwa kina jinsi alama za makasha zinavyotofautiana.

Kasha la kwanza lina picha ya kasha lililowazi na sarafu zikionekana, kama nilivyosema awali kasha hili linamaanisha malipo ya fedha.

Kasha la pili ni kasha lililofungwa lakini kwa juu lina mistari miwili ya madini ya fedha (silver), kasha hili limepewa kazi iliyotambulishwa kama (Collect) kwa kiswahili ‘’kusanya’’. Maneno haya yanamaanisha thamani ya pesa yote iliyopatikana, kujumlishwa na kulipwa kupitia alama zilizoko kwenye skrini yako kwa muda huo.

Kasha la pili ni kasha la makusanyo la malipo ya ziada (Extra credit collect) ambayo yatajitokeza wakati mchezo ukiwa unalipa. Alama hii ya kasha ni kasha lenye mistari miwili ya dhahabu iliyozunguka kasha lililofungwa.

Ikiwa alama ya kasha hili itajitokeza basi alama hii itajiunga na alama ya kasha la kwanza na kuongeza thamani ya malipo mwishoni, wakati hesabu ya jumla ikiwa inajipiga.

Kasha la tatu na la mwisho ni kasha la lenye rangi mbili za zamanbarau linalokwenda kwa jina la makusanyo yaliyozidishwa au yatakayozidishwa maradufu (Multiplier collect). Hii ni thamani ya pesa iliyopatikana kupitia kasha la kwanza ambapo malipo yatakuwa bado yanaonekana kwenye skrini ukizidisha na thamani ya alama za makusanyo yaliyozdishwa.

Tafsiri au maana yam akasha hay ani malipo ya ziada yenye ongezeko linaloweza kujizidisha wakati wa majumuisho ya mwisho ya malipo, hivyo kukupa mchezaji wigo mpana wa malipo mpaka mara 5000, ukizidisha dau unalotumia.

Kasha la nne na la mwisho ni kasha la makusanyo ya ziada yaliyodondoka (extra drop Collect). Kabla makusanyo ya pesa iliyodondoka hayajaanza, mchezaji ataona alama ya pesa nyingi zilizotawanyika bila mpangilio maalum, katika maduara  katika skrini yake zikiwa na viwango tofauti vya thamani.

Ikiwa alama nyingi za makusanyo zitatokea kwenye skrini mwishoni mwa mtetemo (at the end of trumbling) uliotokana na mzunguko wa mchezo, kila alama ya makusanyo itahesabiwa kwa mpangilio unaoanzaia kulia mwa duara namba 1 mpaka duara namba 7, na kutoka juu mpaka chini mwa maduara.

Alama ya ‘’ CURSED WILD”, ikiwa mchezaji utaona alama au maandishi ya neno hilo basi ujue moja kati ya yafuatayo litatokea.

Alama zote za CURSED WILD zilizopo kwenye skrini zitazidishwa mara mbili zaidi katika kila kombinesheni ya ushindi, ikiwemo alama zenyewe za ‘’CURSED WILD’’.

Alama mbali mbali za WILD zitaongezeka sehemu mbali mbali za skrini bila mpangilio maalum.

THE QUEST for BERMUDA RICHIESMICHEZO YA BURE

Kama nilivyo tambulisha awali alama ya kichwa cha mzee mwenye kofia ya ni ishara ya michezo ama mizunguko ya bure, ambayo ikitokea inakuja na maandishi ‘’Scatter’’. Kwenye uhalisia utaona picha kamili ya mtu mwenye kichwa chenye kofia ya Safari.

Ikitokea alama ya mtu huyu na zikatokea alama tatu zilizotokea bila mpangilio maalumu, basi ujue utakuwa umepata michezo 12 ya mizunguko ya kujirudia ya bure. Hapa ndipo utamu wa mchezo huu unapokuja.

Wakati michezo ya mizunguko ya bure ikianza kuzunguka basi na alama za pesa na makasha yote manne ya makusanyo nazo zinaanza kufanya kazi na kuwa hai. Uzuri mmoja kila pesa utakayoshinda katika mizunguko hii ya bure itakusanywa katika chungu kimoja na kujumulishwa mwishoni mwa michezo ya bure na inaweza kuwa pesa yako ya ushindi.

Cha kukusanua ni kwamba kabla mizunguko kwisha kuna gurudumu litatokea likiwa na vipande 10. Gurudumu hilo litazunguka na kusimama kwenye aidha vipande vitatu vya kushinda au vipande vitatu vya kukosa.

Ikiwa gurudumu litasimama kwenye moja kati ya vipande vitatu vya kushinda basi mkwanja huo wa nyongeza utakuwa wako.  Lakini kama gurudumu litasimama kwenye moja kati ya vipande saba, basi utaikosa pesa hiyo.

Cha ziada ni kwamba wakati michezo kumi na mbili ya nyongeza inazunguka ikitokea tena alama ya mtu mwenye kofia ya safari basi mchezaji atapata michezo mingine mitatu kama nyongeza kwenye mizunguko yake.

KIWANGO CHA JUU CHA MALIPO

Mteja anayecheza mchezo huu ana -nafasi ya kushinda kiwango cha dau analocheza katika kila mzunguko X 5000.  Mfano kama mteja unacheza Sh 3000 katika kila mzunguko, basi unaweza ukapata malipo ya 3000X 5000 ambayo nis awa na milioni 15,000,000.

NUNUA MICHEZO YA BURE

Katika mchezo huu wa mteja amepewa nafasi ya kununua michezo ya bure kwa utaratibu ufuatao.

Kulingana na dau ambalo mteja anacheza basi atatakiwa kupandisha dau lake mara (X 100). Mfano mteja anacheza dau la Tsh 500. Ili aweze kununua mizunguko ya bure itambidi apandishe dau lake mpaka 50,000.

Ni matumaini yetu kwamba utakuwa umepata mwanga kidogo kuhusiana na mchezo wa huu wa John Hunter and The Quest for Bermuda Rich.

Zama sportpesa.co.tz kisha angalia kitufe cha Casino alafu utafute mchezo huu wa John Hunter and The Quest for Bermuda.

  

Share this:
Back To Top