MayeleMayele

Usiku wa deni haukawii kucha, unaweza kusema baada ya tambo za muda mrefu vitendo ndivyo vinavyosubiriwa ndani ya Uwanja, ambapo siku ya kesho, Jumapili ya Aprili 16,2023 mashabiki na wapenzi wa kandanda watakuwa wanafuatilia mchezo baina ya watani wa jadi Simba na Yanga, wakionyeshana ubabe kwenye Dabi ya Kariakoo, ikiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu NBC Tanzania kwa msimu huu.

Mchezo huu umekuja, wakati ambao timu zote mbili, zipo kwenye kiwango bora katika historia ya mpira wa Tanzania. Hii inachagizwa na matokeo ambayo timu zote imeyapata katika siku za hivi karibuni, hasa hasa katika michuano ya kimataifa.

Simba wametinga robo fainali ya Klabu bingwa Africa na sasa watapambana na timu ya Wydad Casablanca ya Morocco wiki ijayo, jijini Dar-Es-Salaam.  Yanga nao kwa upande wao, wametinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho,  hivyo kuleta ushindani dhidi ya Simba, ambao wao wanajinadi kama timu kubwa Africa.

Simba walianza msimu huu vibaya dhidi ya watani wao katika mchezo wa ngao ya jamii ambao walipoteza kwa bao 2-1. Tangu kuanza kwa msimu huu Simba bado hajamfunga Yanga katika mechi mbili walizokutana.

Katika mechi mbili ambazo tayari walishacheza Simba ndio walikuwa wanatangulia kufunga. Bao la Pape Ousmane Sakho, liliwatanguliza Simba, kabla ya Fiston Mayele kucheka na nyavu mara mbili  na Yanga kutwaa ushindi.

Lakini katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Ligi Kuu, timu hizo zilitoshana nguvu kwa sare ya bao moja.

Augustine Okrah raia wa Ghana ndiye aliyeitanguliza Simba kabla ya Stephane Aziz Ki kuisawazishia Yanga katika kipindi cha kwanza na mchezo ukamalizika kwa sare.

derbyy-pic-dataSare hiyo ilizidisha machungu kwa wapenzi wa Simba ambao tangu mwaka 2019 hadi sasa wanasubiria kwa hamu kufahamu ni lini wekundu hao wa msimbazi wataonja utamu wa ushindi dhidi ya watani zao Yanga katika Ligi Kuu?

Nakukumbusha tu kwa mara ya mwisho Simba kuifunga Yanga kwenye michuano ya Ligi Kuu ilikuwa Februari 14,2019 kwa bao pekee la aliyekuwa mshambuliaji hatari Medie Kagere lakini tangu hapo wamepoteza mara mbili huku sare zikitawala baina yao.

Matokeo pekee mazuri kwa Simba dhidi ya Yanga ni katika michuano ya Azam Sports Federation Cup ambapo Julai 12,2020 katika nusu fainali mnyama aliwasambaratisha kwa bao 4-1, Clatous Chama,Luis Miquisone,Gerson Fraga na Deo Kanda ndio waliopeleka msiba mitaa ya Twiga na Jangwani .

Mchezo mwingine wa furaha kwa Simba ni ule wa fainali iliyopigwa Lake Tanganyika Julai 25,2021 mnyama akaunguruma tena kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Thaddeo Lwanga kwenye mchezo ulioshuhudia kiungo Tonombe Mukoko akilimwa kadi nyekundu kwa kumchezea madhambi John Bocco.

Mara zote ambazo Simba ilipokuwa ikitawala kwa kuwa na timu bora huku wakitwaa mataji ya Ligi Kuu mara nne,walijikuta wakishindwa kutamba dhidi ya Yanga,lakini stori huwa hazipishani sana kwani hata Yanga ilipoimarika nayo haijawa na matokeo ya ushindi dhidi ya Simba .

Tofauti ya sasa ni kwamba wote wana timu nzuri,Yanga ambao ndio vinara kwa tofauti ya alama 8,wameshinda mechi 13 mfululizo tangu wapoteze mchezo dhidi ya Ihefu mwaka jana, wakati Simba wamekusanya alama 26 kati ya 30 walizopaswa kuzikusanya katika mechi 10 za mwisho.

Tofauti ya alama baina ya miamba hao wawili ni alama 8 na zimesalia mechi 5 ili kuumaliza msimu,hivyo iwapo Yanga watashinda watatengeneza tofauti ya alama kuwa 11 na itawahitaji ushindi katika mechi mbili zitakazofuata ili watwae ubingwa pasipo kutazama wapinzani wao wa karibu wanapata matokeo yapi.

Ushindi wa Simba utapunguza alama na kusalia 5 na inaweza kutengeneza ahueni kwa Simba huku wakisubiria michezo ya mwisho kipi kitaamua.

Simba inazo alama 60,katika mechi 25,wameshinda michezo 18,sare 6,wamepoteza mechi 1 dhidi ya Azam Fc,wamefunga mabao 40 na kuruhusu 14 wakati Yanga wanazo alama 68,wameshinda mechi 20,sare 2 na walipoteza 1 dhidi ya Ihefu ,wamefunga mabao 50 na kuruhusu mabao 11.

Simba inajivunia kuwa na wachezaji tofauti tofauti waliofunga mabao mfano kinara wao ni Moses Phiri mwenye bao 10, John Bocco bao 9,  Saido Ntibazonkiza bao 10, Jean Baleke bao 7,Pape Ousmane Sakho bao 7,Augustine Okrah bao 4,Clatous Chama bao 3,Kibu Denis,Henock Inonga,Habibu Kiyombo,Mzamiru Yassin wote wana mabao mawili kila mmoja huku wakijivunia wakali wa kutoa pasi za mabao kinara ni Chama 14 huku Kapombe Shomari akiwa na pasi 4 naye Mohammed Hussein (4).

Yanga wao mfalme wa kucheka na nyavu ni Fiston Kalala Mayele mwenye bao 16 akifuatiwa na Aziz Ki bao 8, Clement Mzize mwenye bao 4 na Benard Morrison mwenye bao 3.

BalekeStori kubwa kuelekea mchezo huu ni kiwango cha wafumania nyavu, Jean Baleke ambaye tangu kuanza kwa mwaka huu amekuwa kwenye ubora wa aina yake,amefunga bao 7 katika michezo 6 ya Ligi Kuu na amefunga katika michezo mitano ya mwisho ambapo juzi alifunga mawili dhidi ya Ihefu.

Stephan Aziz Ki,Bernard Morrison na Fiston Mayele ambao wamekuwa na bahati ya kuifunga Simba nao wote waliibuka mashujaa katika mchezo wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar ambapo walifunga ikiwa ni matayarisho kuelekea mchezo huu.

Ni Derby ya kwanza kwa Kocha Robertinho lakini Nassredine Mohamed ana uzoefu wa mechi ya aina hizi na amepoteza mara moja tu katika fainali ya ASFC.

Unafikiri ni timu gani itaondoka inacheka na timu gani itaondoka wamenuna?

Kama kawaida yetu SportPesa tumeshakuwekea mechi hii katika tovuti yetu sportpesa.co.tz au piga *150*87#. Kucheza.

Share this: