Young Africans vs Al AhlyYoung Africans vs Al Ahly
  • Vita ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika CAFCL na Kombe la Shirikisho Afrika CAFCC, itaendelea tena kutimua vumbi wikiendi hii.  
  • Kati ya pambano ambalo linasubiriwa kwa hamu ni ule wa Young Africans vs Al Ahly
  • Mchezo huu wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), utapigwa dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika, yataendelea tena kutimua vumbi wikiendi hii.  Kati ya michezo mikubwa inayosubiriwa ni ule wa Young Africans vs Al Ahly. Mchezo huu wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League), unatarajiwa kupigwa kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.

SOMA HII PIA: Al Ahly 2-0 Yanga SC CAF Champions League/ Stats,highlights

Je, bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

H2H, Young Africans vs Al Ahly

Young Africans vs Al Ahly
Young Africans vs Al Ahly H2H

Katika historia ya soka la ushindani Young Africans vs Al Ahly wamekutana katika michezo 9, katika siku za karibuni. Mpaka sasa Al Ahly wamekuwa bora, ambapo Katika michezo 9 waliyokutana wameshinda 6. Young Africans wameshinda mechi moja tu, huku mechi 2 zikimalizika kwa sare. Hivyo mchezo huu, ni nafasi kwa Wananchi kuboresha rekodi hii.

Vikosi tarajiwa Young Africans vs Al Ahly

Timu hizi mbili hazitarajiwi kuwa na mabadiliko makubwa ya vikosi kuendana na vile ambavyo vilikutana wiki iliyopita. Hii ni kwakuwa hakuna majeraha mapya yaliyoripotiwa.

Kikosi cha Young Africans

Kikosi cha Young Africans
Kikosi cha Young Africans

Kipa: Diarra

Walinzi: Mwenda, Mohammed, Mwamnyeto, Bacca

Viungo: Abuya, Damaro, Pacome, Maxi, Okello

Washambuliaji: Dube

Kikosi cha Al Ahly

Kikosi cha Al Ahly
Kikosi cha Al Ahly

Kipa: El Shanawy

Walinzi: Hany, Yassin, Yasser, Koka

Viungo: Dieng, Attia, Zizo, Trezeguet, Eid

Mshambuliaji: Othman

SOMA HII ZAIDI: Al Ahly vs Young Africans: CAFCL: Live Score, h2h, lineups, utabiri, Habari za timu

Walichosema Young Africans kuhusu kuwavaa Al Ahly

Akizungumzia mchezo huo Ofisa Habari wa Young Africans, Ali Kamwe amesema: “Tunatambua kuwa tunacheza dhidi ya klabu kubwa Afrika hilo linahitaji heshima, hautakuwa mchezo rahisi lakini kama tunataka kuwa sehemu ya historia ya soka la Afrika, si suala la kuwa na hofu ni suala la kucheza mpira.

“Tupo nyumbani na tunataka matokeo ya ushindi, ili uwe timu bora ni lazima ucheze dhidi ya timu bora. Tunaamini kikosi chetu kina ubora, wachezaji wana hali nzuri na wana hamu ya kutoa kila kitu kwa ajili ya timu. Tunawaamini wachezaji wetu na tunaamini kuwa tutapata matokeo tunayoyataka.

“Kundi letu ni gumu sana. Tunawaheshimu wapinzani wetu wote kwa sababu wana historia kubwa na wametwaa mataji mengi barani Afrika. Lakini ukweli ni kwamba sisi pia tuna mipango ya muda mrefu ya kuwa miongoni mwa timu bora Afrika. Tuna pointi nne na bado tuna nafasi nzuri ya kuvuka hatua ya makundi.”

Young Africans vs Al Ahly, Ratiba ya Ligi ya Mabingwa Afrika

Depu vs Al Ahly
Depu vs Al Ahly

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mchezo wanne wa hatua ya makundi kwa timu hizi, na mchezo ‘back-to-back’ dhidi ya Al Ahly. Mchezo wa kwanza ulipigwa nchini Misri Ijumaa ya Januari 23, mwaka huu na mchezo wa marudiano unapigwa Jumamosi ya Januari 31, mwaka huu. Ikumbukwe michezo hii ni mwendelezo wa mechi za hatua ya Makundi, ya Caf Champions League.

Young Africans vs Al Ahly, Wananchi waiteka Zanzibar

Uwanja wa New Amaan Complex- Zanzibar
Uwanja wa New Amaan Complex- Zanzibar

Kuelekea ratiba ya mechi hii, tayari kikosi cha Yanga kimewasiri Zanzibar na kinaendelea na mazoezi ya mwisho, kabla ya kuwavaa Mafarao Jumamosi. Taarifa njema kwa Young Africans ni kuwa hakuna majeruhi aliyeongezeka. Hii inampa wigo mpana kocha Pedro kupanga kikosi chake.

SOMA HII PIA: Yanga SC vs AS FAR CAF Champions League: Kocha Pedro awaandalia dozi waarabu

Hitimisho

Young Africans vs Al Ahly ni zaidi ya mechi, hii ni vita ya thamani ya kuisaka Robo Fainali. Kila timu itajaribu kuboresha takwimu za kukutana kwao, ambapo mpaka sasa Al Ahly amekuwa bora. Katika michezo 9 waliyokutana waarabu wameshinda mechi 6, Yanga wameshinda mechi moja tu, huku mechi 2 zikimalizika kwa sare.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.