Sevilla-picSevilla-pic

MANCHESTER United kesho inaikaribisha timu ya Sevilla inayoshiriki Ligi kuu ya Uhispania katika mchezo wa ngwe ya kwanza ya robo fainali ya michuano ya ligi ya Europa, utakaochezwa katika Uwanja wa Old Trafford, nchini Uingereza.

United wanaingia katika mchezo huowa kesho, wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuzinyanyasa timu 3 za soka kutoka Uhispania, na kuziondosha katika michuano hiyo zikiwemo timu za Real Sociedad, Barcelona and Real Betis zilipokutana kwa nyakati tofauti.

Manchester United inashika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza, ikiwa na pointi 56, katika michezo 29 iliyoshuka dimbani.

Timu hii yenye maskani yake jijini Manchester, ipo nyuma ya New Castle, Manchester City pamoja na vinara wa ligi hiyo Arsenal inaingia katika mchezo huu ikiwana matokeo mazuri katika mechi mbili ilizocheza hivi karibuni.

Manchester imeshinda michezo miwili dhidi ya Everton, Brentford na kupoteza mchezo mmoja dhidi ya Newcastle United katika jumla ya michezo ya mitatu iliyopita.

Marcus Rashford ndiye kinara wa magoli ndani ya Klabu ya Manchester akiwa amefunga jumla ya magoli 15 katika michuano mbalimbali ambayo timu hiyo imeshiriki msimu huu.

Bruno Fernandez ana magoli 5 pamoja na Jadon Sancho mwenye magoli 4 timu ikichezo mchezo wa kushambulia kutokea pembeni.

Kwa upande wa Sevilla, timu hii inashika nafasi ya 13, ikiwa na pointi  32 katika msimamo wa Ligi Kuu ya nchini Hispania, inayoongozwa na kinara Barcelona yenye pointi 7.

Sevilla inaingia katika mchezo wa kesho ikiwa imeshinda mchezo mmoja, kutoa sare mchezo mmoja na kupoteza mchezo mmoja katika jumla ya michezo mitatu iliyocheza, hivi karibuni.

Kimsingi Sevilla inamtegemea mchezaji wake Youssef En Nesyri, raia kutoka katika Taifa la Morroco katika upachikaji wa mabao, akiwa ameifungia klabu hiyo jumla ya magoli 7 katika michuano mbalimbali ambayo klabu hiyo imecheza akifuatiwa na Muagentina Lamela Erik mwenye jumla ya magoli 4 katika michuano yote y msimu huu ambayo ameichezea timu yake.

Kwa takwimu za haraka haraka zinaonesha kuwa United ipo katika nafasi nzuri ya kushinda mchezo huu wa kesho na pengine hata katika mchezo wa maruadiano utakaofanyika April 20 nchini Hispania.

Manchester United

Ujio wa kocha Mholanzi Erik Teg Hag ambaye tayari ameiwezesha United kuchukua komba la Carabao msimu huu, anaingia katika mchezo huu wa kesho kuliwinda kombe la UEFA EUROPA LEAGUE (UEL)ambalo kwa mara ya mwisho ililichukua mwaka 2017.

Mchezo huu wa mkondo wa kwanza, unaonekana kuwa mwepesi  kwa vijana wa Hag, ambao hawajashindwa katika Uwanja wa Old Trafford katika mechi 24, ambazo wamecheza wakishinda michezo 21, na kutoka sare michezo mitatu, katika kipindi cha kuanzia  Septemba 2022.

Hata hivyo, Sevilla inaweza kuwa ‘mnyama’ tofauti kwani vijana hao wa kocha José Luis Mendilibar, wamewasili Uingereza wakiwa hawajapoteza mchezo hata mmoja, dhidi ya Mashetani Wekundu katika michezo mitatu waliyowahi kukutana kipindi cha nyuma.

Sevilla wanaingia wakiwa na matumaini ya kufanya vizuri ingawa pia kumbukumbu ya sare ya magoli 2-2 iliyoipata mechi ya mwisho dhidi ya Celta Vigo inayoshiriki ligi ya Hispania imeonyesha kuwakatisha tamaa.

Katika mchezo wa kesho timu ya Man United inategemewa kumtegemea zaidi mchezaji Anthony Martial kama mshambuliaji kiongozi, kwani straika tegemeo Marcus Rashford alipata majeraha katika mechi dhidi ya Everton na bado hali yake haijatengemaa vya kutosha.

Vile vile Manchester inaweza kumtumia mchezaji Casemiro kama beki wa kati, huku kwenye nafasi ya kiungo Manchester wanatarajiwa kuwatumia Scot Mc Tominay, Marcel Sabitzer.

Wengine wanaotarajiwa kuanza siku ya kesho ni pamoja na De Gea, Wan Bissaka, Verane, Martinez, Malacia, Fernandes na Sancho.

Duru za kimichezo barani Ulaya zinaeleza kuwa, pamoja na Manchester United kupewa nafasi kubwa ya kushinda mechi ya kesho, timu ya Sevilla ni moja ya timu zenye rekodi nzuri katika mashindano ya kombe la Ulaya, wakiwa na rekodi ya kutwaa taji hilo mara 6, tangu msimu wa mwaka 2006.

Sevilla itawategemea zaidi wachezaji wake Rafa Mir, En Nesyri, Erik Lamella, Fernando, Acuna, Jesus Navas, Dmitrovic, Alex Telles, Rakitic na wengineo ambao wapo katika msafara wa watu 22, uliosafiri kwenda Manchester.

Kwetu SportPesa, hii ni moja ya mechi ambazo tayari ipo kwenye tovuti yetu sportpesa.co.tz.

Kwa watumiaji wa viswaswadu piga *150*87#

Share this: