Real-Madrid-Real-Madrid-

Usiku mwingine wa Ulaya unachukua nafasi yake siku ya kesho kwa mchezo mwingine wa robo fainali ya kwanza ya kombe la klabu bingwa Ulaya, UEFA Champions League,ambapo mabingwa wa kihistoria, Real Madrid watakabiliana na miamba kutoka Jiji la London, Chelsea FC katika dimba la Santiano Bernabeu.

Real Madrid wanaanzia nyumbani kama wenyeji katika mchezo wa mkondo wa kwanza, wakiwakabili Chelsea katika robo fainali ambayo timu hizi mbili zinakutana katika msimu wa pili mfululizo. Ikumbukwe msimu uliopita The Blues walitupwa nje na Los Blancos kwa jumla ya mabao 5-4,  baada ya vuta nikuvute katika mchezo wa marudiano ambao ulilazimika kuchezwa hadi dakika za nyongeza.

Hii ni mechi kabambe na ngumu kwa Chelsea kwakuwa wanakutana na Real Madrid ambayo katika hatua ya 16 bora waliwasambaratisha Liverpool kwa jumla ya magoli 6-2 baada ya michezo miwili.

Mchezo huo wa kesho unatarajiwa kuwa mgumu sana kwa Chelsea, kama ambavyo ilikuwa kwa Liverpool, ikizingatiwa kiwango na ubora wa timu hii kuporomoka, katika siku za hivi karibuni.

Real Madrid wamezidiwa maarifa na Barcelona katika mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania hivyo michuano ya Klabu bingwa ni kipaumbele kwa Kocha Carlo Anceloti. Hata hivyo pamoja na kiwango dunia cha Chelsea ambao mara zote wanapokuwa kwenye mazingira mabaya katika Ligi ya ndani wamekuwa wakishangaza katika UEFA Champions League.

Frank Lampard alikuwa ni sehemu ya safari ya The Blues kutwaa ubingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya ,2021, ambapo baada ya kuifikisha hatua ya robo fainali aliondoshwa na mikoba yake alikabidhiwa Thomas Tuchel ambaye aliwaondosha Real Madrid hawa kabla ya kuwafunga Manchester City katika fainali. Je Lampard ambaye amekabidhiwa mikoba iliyoachwa na Graham Potter atakamilisha mpango wake uliokatizwa na mmiliki wa Chelsea kwa wakati huo Roman Abramovich?

Chelsea ilitinga hatua hii baada ya kuiondosha Borussia Dortmund kwa jumla ya mabao 2-1 licha ya kupoteza katika mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 nchini Ujerumani wakati Real Madrid iliitupa nje Liverpool kwa bao 6-2 .

Huu ni mchezo unaozikutanisha timu bingwa ambapo Chelsea imetwaa taji mara 2, lakini Real Madrid ndio mabingwa wa kihistoria wakiwa wametwaa  taji hili mara 14.

Karim Benzema ni ndiye mshambuliaji anayetajwa kuwa mwiba zaidi kwa Chelsea ambapo msimu uliopita alifunga Hat trick katika mchezo wa mkondo wa kwanza pale Stanford Bridge wakati Los Blancos wakishinda bao 3-1, kabla ya kufunga bao muhimu katika mchezo wa marudiano, ambapo licha ya Chelsea kushinda 3-2 lakini walitupwa nje ya michuano kutokana na tofauti ya magoli ya jumla.

Kocha wa Real Madrid Carlo Anceloti, hajawa na matokeo mazuri katika ligi ya nyumbani, nazungumzia La Liga na wameachwa na Barcelona kwa takriban pointi 15 katika msimamo wa ligi.

Chelsea Cha kushangaza hali imekuwa tofauti kwa timu ya Real Madrid kwenye michuano hii ya Ulaya na hawakuonekana kuyumba walipokabiliana na Liverpool na sasa wanatarajiwa kuwekeza nguvu kubwa katika michuano hii ya Ulaya msimu huu.

Frank Lampard ambaye ni bingwa wa UCL enzi zake akiwa akiwa mchezaji hana wakati mzuri katika kibarua chake tangu kukabidhiwa timu wiki iliyopita baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Wolves huku timu yake ikionyesha mchezo usio na tija.

Aidha kesho hiyo hiyo, mechi nyingine ya robo fainali itashuhudiwa katika Jiji la Milan katika  dimba la San Siro, ambapo kutapigwa mchezo kati ya mabingwa mara 7 wa UEFA Champions League ,AC Milan dhidi ya Napoli ikiwa ni mchezo mwingine mzuri na wa kuvutia wa hatua ya robo fainali.

Huu ni mchezo ambao unazikutanisha timu zilizokutana siku chache zilizopita kwenye kipute cha Sere A ambapo AC Milan ikiwa ugenini iliwashangaza wengi kwa kuwalaza vinara wa Ligi Kuu ya Italia,Napoli kwa mabao 4-0 tena wakiwa kwenye dimba lao la nyumbani la Diego Armando Maradona.

AC Milan walitinga hatua hii ya robo fainali baada ya kuwaondosha Tottenham Hotspurs ya England kwa bao 1-0 wakati Napoli iliwaondosha Eintratch Frankfurt ya Ujerumani kwa ushindi wa mabao 5-0.

Katika michezo sita iliyopita ya mashindano yote AC Milan imeshinda mmoja pekee dhidi ya Napoli wakati wakitoka sare mara tatu na kupoteza mmoja wakati Napoli wao wameshinda mara nne huku wakipoteza mara mbili.

Vijana wa kocha Luciano Spalleti walikuwa kwenye kiwango bora kabla ya kukutana na AC Milan ambapo walifunga bao 9 lakini  katika mchezo huo walishindwa kupata bao lakini pia rekodi inaonyesha katika mechi tatu zilizopita wamepoteza mara 2 na kushinda moja.

Kikosi cha Kocha Stefano Pioli kimefunga katika mechi tatu zilizopita jambo ambalo lina ashiria safu ya ushambuliaji ya AC Milan inayo ongozwa na mkongwe Olivier Giroud na chipukizi Rafael Leao inaweza ikawa tishio dhidi ya ukuta wa Napoli.

Hakujawa na ripoti ya moja kwa moja kuhusu hali ya mshambuliaji tishio katika Seria A na hata Ulaya kwa sasa, Victor Osimhen aliyepata majeraha kwenye mchezo uliopita lakini uwepo wake ni muhimu kwani amefunga mabao manne katika michezo mitano aliyocheza.

Kama kawaida yetu Sportpesa tumekuwekea michezo hii miwili mikubwa kwa siku ya kesho, lakini kubwa kuliko yote mechi hizi mbili Odds zake zimebustiwa. Sasa unaweza kuzicheza kupitia tovuti yetu sportpesa.co.tz na kwa wenye Sportpesa App. Kwa wale wanaotumia simu za viswaswadu unapiga *150*87#.

Share this: