Ukizungumzia mechi kali za mpira katika bara la Ulaya kwa siku ya kesho, basi uwezi kuacha kutaja mechi kati ya timu ya Manchester City dhidi ya Bayern Munich. Mechi ya kwanza ya robo fainali ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya, almaarufu kama UEFA Champions League.
Mechi hiyo itakayopigwa siku ya kesho (jumanne) katika uwanja wa Ettihad,jijini Manchester, inazikutanisha timu mbili zenye muundo na falsafa tofauti ya mpira, moja ikitumia mpira wa madaha na nyingine ikitumia mpira wa nguvu zaidi.
Licha ya matokeo mabovu katika mchezo wao wa hivi majuzi dhidi ya Bayer Leverkusen, Bayern Munich bado ni miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kubwa ya kufuzu kwenda kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Istanbul, Uturuki baadaye mwezi ujao.
Hata hivyo timu ya Bayern Munich ilimaliza hatua ya makundi ikiwa imeshinda mechi zote 6 na kujikusanyia jumla ya pointi 18, wakati Manchester City, ilimaliza hatua ya makundi katika kundi G ikiwa imeshinda mechi 3 na kutoa sare mechi mbili.
Mechi hii baina ya timu hizi mbili inapewa hadhi ya fainali ambayo ingetakiwa kuchezwa kule Instanbul hapo baadae mwaka huu, kutokana na aina ya timu na mifumo ya uchezaji ambao unategemewa kuzalisha upinzania wa hali ya juu wakati timu hizi zitakapokutana siku ya kesho.
Ili iweze kusonga mbele kwenda hatua ya nusu fainali Bayern itabidi kuwa makini zaidi katika safu yake ya ulinzi ambayo mpaka sasa imesharuhusu kufungwa mechi tatu katika ligi ya Bundesliga, mechi ambazo ilicheza na Bayer Leverkusen hapo majuzi, wamepoteza mechi dhidi ya FC Augusburg, na mechi nyingine ni dhidi ya Borrusia Monchengladbach.
Manchester City nao kwa upande wao wao wako nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya Uingereza almaarufu kama English Premier League wakifukuzana na timu ya Arsenal inayoongoza ligi ikiwa na tofauti ya pointi 8.
Ushindi kwa timu ya Manchester City utategemea zaidi mbinu za kocha Kocha Pep Guardiola ambaye inaeleweka anategemea zaidi ubora wa mshambuliaje wake Eerling Halland kuweza kumpatia magoli ambayo yatafanya timu yake isonge mbele.
Utamu wa mechi hii unategemewa kuwepo zaidi katika nusu ya uwanja kwani timu zote mbili zina viungo bora ambao wanatarajiwa kuipa mechi hii ubora na hadhi ya juu.
Eneo lingine ambalo linachagiza utamu wa mechi hii ni uwepo wa kocha Thomas Tuchel, kocha wa zamani wat imu ya Chelsea, ambaye kwa sasa ndiye kocha mkuu wa Bayern Munich.
Ikumbukwe kocha huyu anaielewa fika timu ya Manchester City na anaelewa mbinu zote za Pep Guardiola, kama ambavyo walikuwa wakipambana wakati yupo na timu ya Chelsea.
Tukianza na Bayern Munich wao wanamtegemea zaidi mchezaji Joshua Kimmich, ambaye yeye hushirikiana kwa ukaribu na wachezaji wenzake wakiwamo Matthijs De Ligt, Serge Gnabry, Alphonso Davies, Le Roy Sane, Yann Sommer, Noussair Mazraoui, Josip Stanisic, Leon Goretzka, Kingsley Coman na Sadio Mane.
Kwa upande wa kocha Pep Guardiola, Yeye anaeleweka kwamba anazo silaha za kumpatia matokeo kwa kutumia wachezaji wake wa kati kati ya uwanja nazungumzia wachezaji kama Rodrigo Hernandes Cascante, ambaye anajulikana zaidi kama ‘’Rodri’’, Kevin De Bruyne, Ikay Gundogan, Bernado Silva, Phil Phoden, Jack Graelish, Kalvin Phillips, Manuel Akanji, Nathan Ake, Joao Cancelo, Riyad Mahrez na Kyle Walker.
Tayari rekodi za mchezaji huyo zinambeba kufanya vizuri katika mechi hiyo ya kesho kwani toka hatua ya makundi mpaka hiyo kesho timu hizi mbili zinapoenda kukutana ameshafunga magoli 10, katika mechi 6 za kombe la UEFA alizocheza.
Bayern kwa upande wao wao watakuwa wanamtegemea zaidi mshambuliaji raia wa Cameroon Eric Choupo Moting ambaye amefanikiwa kufunga magoli 15 msimu huu ,huku akifunga goli moja dhidi ya PSG katika mechi ya mwisho ya kundi C.
Ni matumaini yangu utakuwa umepata pa kuanzia kuhusiana na timu hizi mbili kwa namna ambavyo tumekuwekea takwimu za timu zote.
Mechii tayari ipo kwenye tovuti ya Sportpesa.co.tz na timu zote mbili odds zao zimesha bustiwa.
Kubasiria mechi hii tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#

