Kama wewe ni shabiki wa mpira, ama mpenzi wa mechi za ligi kuu ya Uingereza, EPL, basi utakuwa unajua nini kinaenda kutokea kesho pale katika uwanja wa Anfield.
Timu ya Liverpool itakuwa mwenyeji wa timu ya Arsenal, ‘’The Gunners’’ almaarufu kama washika bunduki kutoka kaskazini mwa jiji la London, ambao kwa sasa ndio vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Klabu hizi zinakutana wakati timu ya Arsenal, chini ya kocha Mikel Arteta itakuwa inajaribu kutimiza ndoto ambayo ni kama ilikuwa ya kufikirika ambayo ni ya kutwaa taji lao la kwanza tangu msimu wa 2003/04.
Kwa upande wa Liverpool, mambo yao yanazidi kwenda mrama, ambapo mpaka sasa majogoo hawa wanapambana kumaliza ndani ya nne bora ili wasipoteze nafasi ya kucheza Ligi ya mabingwa msimu ujao.
Tangu msimu wa 2019/20, timu hizi zimekutana mara 6, na katika kila mechi za ligi kuu ya English Premier League walizocheza, Liverpool waliibuka na ushindi mara 5, huku The Gunners wao wakishinda mara 1, tena wakiupata msimu huu kwa jumla ya mabao (3-2) kwenye dimba la Emirates.
Haikuwa rahisi kuona tofauti baina ya timu hizi mbili inakuwa kubwa kiasi hiki ambapo hadi sasa Arsenal yenye alama 72 imeiacha Liverpool kwa tofauti ya alama 30. Wakali hao wa Anfield mpaka muda huu wa kuandika makala hii wana alama 42.
Vijana wa Kocha Jurgen Klopp wapo nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi, hivyo wanahitaji kukusanya alama katika mchezo wa kesho ili kupunguza pengo kati yao na Tottenham Hotspurs na Manchester United walio katika nafasi ya 4 na 5, kwa tofauti ya pointi 50 kila mmoja.
Katika orodha ya walio juu ya Liverpool wamo pia Brighton&Hove Albion, nafasi ya (6) na Brentford nafasi ya (7) wenye tofauti ya pointi na Liverpool kwa pointi 3 kila mmoja.
Arsenal kwa upande wao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 72, alama 8 zaidi ya mabingwa watetezi Manchester City, ambao wao wana alama 64. Ikitokea Arsenal akashinda mechi ya kesho dhidi ya Liverpool, basi matokeo hayo yatakuwa na maana kubwa sana katika mbio za kutwaa ubingwa wa EPL kwa msimu huu wa 2022/2023 na kusogea karibu kabisa kulibeba taji hilo, akiwa amebakia na mechi 8 kumaliza msimu.
Ikumbukwe, katika mchezo wa kwanza uliohusisha timu hizi mbili, washika bunduki wa London Arsenal, waliibuka kidedea, kwa ushindi wa magoli 3-2, mnamo Oktoba 9,2022.
Mchezaji Gabriel Martinel alifunga goli moja, wakati Bukayo Saka alifunga magoli mawili katika mechi iliyopigwa katika dimba la Emirates.
Magoli ya Liverpool yaliwekwa kimiani na Darwin Nunez na Roberto Firmino.
Kwa sasa, Arsenal imeimarika kwenye maeneo mengi, ikiwemo eneo la ulinzi, ambapo ndio timu pekee iliyopoteza mechi 2 tu, sawa na Newcastle United waliopoteza mechi 3.
Ki takwimu Arsenal ni timu yenye sare chache kuliko timu yeyote (3), pia ndio timu ya pili kufunga mabao mengi (70), ikizidiwa bao moja pekee na Man City, ambao ndio vinara kwa kufunga bao 71.
Arsenal ndio timu ya pili yenye wastani mzuri wa kuruhusu mabao (27) wakati Man City wameruhusu mabao machache zaidi (23).
Takwimu za Liverpool hazionyeshi mwenendo mzuri katika ligi ya EPL msimu huu. Katika mechi 27 ambazo tayari wamekwishacheza, Liverpool wameshinda mechi 12, wamepoteza mechi 9, na kutoa sare mechi 6.
Wenyewe wameweza kufunga magoli 48 na kuruhusu kufungwa mabao 33 na hiyo ni ishara kwamba Jurgen Klopp na vijana wake wanapitia hali ngumu msimu huu.
Japokuwa Liverpool waliushangaza ulimwengu walipokutana na Manchester United ambapo walionekana kuwa timu ya tofauti baada ya kutoa kipigo cha aina yake cha bao 7-0 jambo ambalo liliamsha hisia za tofauti kwa wapenzi wa EPL wakiamini huenda majogoo wa Jiji wamereja kwenye njia yao.
Beki na nahodha wa zamani wa Liverpool Jamie Gharrager amesema timu yake itawazuia Arsenal kwenye mchezo huo na kuziweka matatani mbio zao za kutwaa ubingwa wa kwanza wa EPL baada ya miaka 19.
‘’Mechi hii itakuwa ni ya maamuzi kwa pande zote mbili, licha ya matatizo wanayoyapitia Liverpool. Ninaamini hawatokuwa tayari kuruhusu kupoteza mechi na ninajua watatoa ushindani mkubwa dhidi ya Arsenal na hawatokubali kuwa dhaifu kwakuwa wao ni washindani halisi katika Ligi’’Gharrager
Upande wa Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa ‘’kwakuwa tutakuwa nyumbani,tunapaswa kusahau yaliyopita baada ya kupoteza dhidi ya Man City,tutajipanga kwa ajili ya kushinda na kuona muendelezo bora kwa mechi zilizosalia.
Naye Kocha wa Arsenal,Mikel Arteta amesema’’Kuna tofauti kidogo ya mechi kati yetu na anayetufuatia,lakini sisi tunapaswa kushinda mechi zetu ikiwemo dhidi ya Liverpool ili tuone mwisho wa safari yetu’’.
Wachezaji ambao wapo katika wakati mzuri kwa Arsenal ni Gabriel Martinelli mwenye bao 13 akifuatiwa na Bukayo Saka mwenye bao 11 na hawa ndio walioiangamiza Liverpool katika mchezo mkondo wa kwanza lakini kwa Liverpool kinara wao ni Mohamed Salah mwenye mabao 12 akifuatiwa na Darwin Nunez bao 8 na aliwafunga Arsenal katika mchezo wa kwanza.
Tayari SportPesa tumekuwekea mechi hii na pia tume boost odds za timu zote mbili. Kujisajili na kucheza tembelea sportpesa.co.tz au piga *150*87#.

