Chelsea vs LiverpoolChelsea-v-Liverpool

MOTO utawaka Barani Ulaya ambako miamba ya soka baina ya Chelsea na Liverpool katika ligi ya English Premier League, almaarufu kama EPL watapambana katika mwendelezo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza.

Mchezo huu unatarajiwa kupigwa majira ya saa nne kamili usiku, kwenye Uwanja wa Stamford Bridge uliyopo, kusini Magharibi mwa jiji la London, nchini Uingereza.

Yote kwa yote mechi hii inabeba mustakabali wa Chelsea na Liverpool kwani timu zote mbili nikianza na Chelsea wenyewe wako nafasi ya 10, katika msimamo wa Ligi, wakiwa wamejikusanyia pointi 38, baada ya kucheza mechi 27.

Liverpool kwa upande wao wapo nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi, wakiwa wamejikusanyia pointi 42, baada ya kucheza mechi 26. Hii inamaanisha Chelsea kama atashinda atapanda mpaka nafasi ya tisa ambayo kwa sasa imekaliwa na Fulham.

Liverpool wao wakishinda watafikisha pointi 45, na hivyo kuendelea kuinyemelea nafasi ya kuingia ‘’top four’’ ili wapate nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa katika msimu wa Mwaka 2023/2024.

Kumbukumbu zinatuonyesha, katika michezo mitano ya mwisho ambayo timu hizo zilikutana, hakuna timu iliyopata ushindi zaidi ya kuambuliwa sare pekee.

Matokeo ya michezo hiyo mitano yalikuwa hivi; Liverpool 0-0 Chelsea uliokuwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Chelsea 0-0 Liverpool      wa Kombe la FA, Chelsea        0-0 Liverpool wa Kombe la Carabao.

Chelsea 2-2 Liverpool na Liverpool1-1 Chelsea hiyo miwili yote ilikuwa ya Ligi Kuu ya Uingereza. Katika mchezo huo yoyote ana nafasi ya kupata ushindi na kupanda juu katika msimamo.

Kuelekea mchezo huo, Liverpool kama kweli wanahitaji ushindi, basi mabeki wake wanatakiwa kumachunga kiungo mshambuliaji hawa wa Chelsea Kai Havertz mwenye mabao saba akicheza michezo 26.

Wengine ni Raheem Stering mwenye mechi 19 akifunga mabao manne pekee tangu kuanza kwa msimu akifuatiwa na Thiago Silva yeye ni mkali wa kupiga pasi za mwisho na ana umiliki mzuri wa mpira.

Chelsea wenyewe hawatakiwi kumpa nafasi ya kucheza mshambuliaji wa Liverpool, Mohammed Salah aliyecheza michezo 26 akifunga mabao 11 wengine hatari ni Andy Robertson aliyecheza michezo 20 akipachika 8 na Roberto Filimino 8.    

Chelsea vs LiverpoolMabeki wa kati wa Chelsea, wanatakiwa kuongeza umakini kwa Salah ambaye ni mjanja, mara nyingi akitokea pembeni kuchukua mipira na kuanzisha mashambulizi katika goli la wapinzani.

Hivyo mabeki wa Chelsea wanatakiwa wawe na mawasiliano mazuri, pia maamuzi ya haraka katika kumzuia ili hasipate nafasi ya kumiliki mpira ndani na nje ya 18 ya goli lao.

Salah anashika nafasi ya kumi katika ufungaji bora katika kinyanganyiro cha ufungaji bora akipachika mabao 11.

Idadi hiyo ya mabao hakuna mchezaji wa Chelsea ambaye ameifikia kwa sasa huku anayemkaribia akiwa ni Kai Havertz ambaye amefunga mabao saba pekee, akiwa naye amezidiwa na mshambuliaji wa Liverpool Roberto Firmino aliyepachika magoli nane.

Kwa uchache huu wa mabao, inadhihirisha kuwa Chelsea hawana straika tishio katika kikosi chao cha msimu huu ambacho hakina mwenendo wa matokeo mazuri.

Washambuliaji kumi bora katika orodha ya wafungaji bora katika ligi ni mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland ndiye anayeongoza aliyefunga mabao City28, Harry Kane 21 (Tottenham Hotspur), Ivan Toney 16 (Brentford), Marcus Rashford 14 (Manchester United), Gabriel Martinelli 13 (Arsenal).

Wengine ni Bukayo Saka 12 (Arsenal), Miguel Almirón 11 (Newcastle), Aleksandar Mitrovic 11 (Fulham), Rodrigo 11 (Leeds) na Mohamed Salah 11 (Liverpool).

Pia kwa upande wa Liverpool yupo kiungo mshambuliaji Darwin Núñez yeye ana mabao manane, tofauti na Salah ambao hao wana  muunganiko mzuri katika safu ya ushambuliaji.

Mastaa hao wote wanajua kutengenezeana mipira wakiwa ndani na nje ya 18 ya goli la wapinzani, hivyo Chelsea hawataki kumtolea macho Salah pekee.

Yupo kiungo mwingine mshambuliaji wa Liverpool ambaye ni Cody Gakpo yeye amefunga mabao manne pekee ni idadi chache ya mabao, lakini ni mchezaji msumbufu anayetakiwa kuchungwa na mabeki wa Chelsea.

Tayari SportPesa tumeshakuwekea mechi hii kupitia tovuti yetu ya sportpesa.co.tz. Kwa wewe unaetumia simu za kitochi au kiswaswadu piga *150*87# ili uweze kucheza na kushinda kumbuka kuna bonus kama utaweka multibet hadi asilimia 1000 kuanzia mechi tatu za mkeka wako.

Share this: