Azam FC yaivuruga Simba SCLameck Lawi
  • Lameck Lawi nyota wa mchezo Azam FC 1-0 Simba SC, NMB Mapinduzi Cup 2026
  • Azam FC yaivuruga Simba SC yaifunga mara mbili mfululizo NBC Premier League matokeo Simba SC 0-2 Azam FC.
  • Kariakoo Dabi hakuna tena hatua ya fainali kwa mafahari wawili Yanga SC vs Simba SC

Azam FC yaivuruga Simba SC 2025/26 baada ya kupata matokeo mara mbili mfululizo. Wababe hawa wamekutana mara mbili mashindano tofauti. Simba SC 0-2 Azam FC ilikuwa ligi na Azam FC 1-0 Simba SC, NMB Mapinduzi Cup. Kupoteza kwa Simba SC kunafanya matarajio ya Kariakoo Dabi fainali kukosekana kabisa.

SOMA HII: Simba SC 0-2 Azam FC ni matokeo yaliyovunja rekodi/ Ratiba ya mechi zijazo CAF Champions League

Vuna mamilioni sasa hivi

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

image

Azam FC yaivuruga Simba SC kwa mbinu uwanjani

Himid vs Simba SC
Himid wa Azam FC vs Kante wa Simba SC, NMB Mapinduzi Cup 2026. Source: Azam FC.

Azam FC yaivuruga Simba SC kwa mbinu uwanjani katika Mzizima Dabi. Kwenye mechi mbili mfululizo safu ya ushambuliaji ya Simba SC haijafunga goli. Matajiri wa Dar wamemfunga mnyama magoli 3.

Matokeo ya Azam FC vs Simba SC 2025/26

Simba SC 0-2 Azam FC, NBC Premier League

Azam FC 1-0 Simba SC, NMB Mapinduzi Cup

Matokeo ya Simba SC Mapinduzi Cup 2026

 Januari 3,2026

Simba SC 1-0 Muembe Makumbi City

Mfungaji: Bajaber

Januari 5,2026

Fufuni FC 1-2 Simba SC

Mfungaji: Hassan Mbegu na Nabby Camara

Januari 8,2026

Azam FC 1-0 Simba SC.

SOMA HII: Simba SC vs Azam FC 2026 NMB Mapinduzi Cup/ Lineups, live score, prediction

image

Kikosi cha Simba SC nusu fainali dhidi ya Azam FC

Mlinda mlango

Hussen Abel

Mabeki

Duchu

Mligo

Chamou

De Reuck

Viungo

Kante

Jean Ahoua

Naby Camara

Ellie Mpanzu

Neo Maema

Mshambuliaji

Jonathan Sowah

Azam FC vs Simba SC
Azam FC vs Simba SC NMB Mapinduzi Cup 2026.

Azam FC matokeo yake Mapinduzi Cup 2026

Desemba 31,2025 Azam FC 1-1 Singida Black Stars

Mfungaji: Kitambala Jephte

Januari 2,2026

Azam FC 2-0 Mlandege

Zidane na Himid Mao

Januari 5,2026

Azam FC 2-1 URA Uganda

Wafungaji: Kitambala Jephte na Alobogast

Januari 8,2026

Azam FC 1-0 Simba SC

Mfungaji: Lameck Lawi.

image

Kikosi cha Azam FC vs Simba SC

Langoni

Air Manula

Mabeki

Chilambo

Zouzou

Lawi

Twalib

Viungo

Himid

Zidane

Kibeku

Kitambala

Akaminko

Diakite

Mchezaji bora wa mchezo

Lawi---
Lameck Lawi mchezaji bora Azam FC vs Simba SC, Mapinduzi Cup.

Beki Lameck Lawi alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Nyota huyo alifunga goli pekee la ushindi dakika ya 73 ambalo lilidumu mpaka mwisho. Ni zawadi ya milioni mbili alikabidhiwa baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.

Kocha Simba SC Steve Barker kapishana na kombe

Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amepishana na kombe la Mapinduzi. Kupoteza mbele ya Azam FC kunawakosesha tiketi kusonga mbele. Unakuwa mchezo wa kwanza kupoteza akiwa kwenye benchi la ufuni.

“Tulikuwa tunahitaji matokeo mazuri kuendelea kwenye mashindano lakini haijawezekana. Wachezaji walipata nafasi lakini hawakuzitumia. Tutakwenda kufanyia kazi makosa ili kuwa bora,”.

Maoni ya Ibenge, kocha wa Azam FC

Florent Ibenge, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema wachezaji walijituma na kutengeneza nafasi. Kwa namna ambavyo wamechezaji ni furaha kupata matokeo mazuri.

“Maandalizi ambayo tulifanya yalikuwa kwa umakini. Vijana wamejituma na kucheza vizuri. Kwa matokeo tuliyopata bado tunapaswa kufanya vizuri mchezo ujao,”.

Hitimisho

Azam FC yaivuruga Simba SC kwa kuwaondoa katika NMB Mapinduzi Cup. Kijana Lameck Lawi alizima ndoto za mnyama kutinga hatua ya fainali. Lango la Azam FC lilikuwa linalindwa na mchezaji wa zamani wa Simba SC, Aishi Manula.

Share this: