skip to Main Content
YAJUE MAAJABU YA MCHEZO WA GEMS OF SERENGETI
Gem-of-Serengeti-

YAJUE MAAJABU YA MCHEZO WA GEMS OF SERENGETI

Gems Of Serengeti ni mmoja wa michezo ya Kasino inayopatikana katika tovuti yetu Sportpesa.co.tz, katika kitufe kilichoandikwa maneno ‘’popular’’, ambapo wachezaji wetu wana nafasi ya kujishindia vitita vinono katika michezo mbali mbali ya Kasino.

Leo tutakuelezea kwa undani kidogo kuhusu mchezo huu ambao unafananishwa sawa na mtu ambaye anakwenda porini kutafuta Almasi au Dhahabu na vito vya aina nyinginezo ambavyo vinapatikana huko.

Mchezo huu wa Gems of Serengeti ni aina ya mchezo wa kasino wa tovuti unaotumia mfumo wa mistari 5 kwa 4, ikiwa na jumla ya mistari 20 ya malipo kutegemeana na kiwango chako cha dau unachoweka katika kila mizunguko, utakaokuwa unacheza.

Kama nilivyo eleza hapo juu, mchezo huu umechukua uhalisia wa mtu au kijana shupavu anayeamua kwenda porini kusaka vito au madini yenye thamani kubwa. Vivyo hivyo ndivyo mchezaji ambaye anaamua kuchagua mchezo huu naye anavyotafsiriwa.

Kama ilivyo kwa msaka madini anavyo amua kuchimba ama kuingia shimoni, ilia pate madini, ndivyo na mchezaji wa mchezo wa Gems of Serengeti naye anavyo usaka utajiri kwa kufungua mchezo, kuweka dau lake na kuchagua mistari ya kumlipa, huku akiombea viduara vya mistari ile imlipe malipo makubwa.

Watengenezaji wa mchezo huu wamewawekea wachezaji aina ya bonus ambapo mteja anayecheza akipata alama ya madini ya Almasi katika mizunguko ya mchezo wake basi anakuwa amepata fursa ya michezo ya bure (free Spin).

Gem-of-Serengeti-Na ikiwa atapata hizo almasi kwa wingi tena basi mchezaji atapata fursa ya michezo ya bure kuongezeka na kujirudia tena hivyo kumpa nafasi ya kupiga mkwanja mrefu zaidi katika malipo yake atakayoyapata.

Mchezo huu unatumia mistari 20 (20 Lines) kulipa mchezaji, kutokea vyumba vya mistari inayoanzia upande wa kushoto kuelekea upande wa kulia. Pia mchezo huu una malipo makubwa sana katika mstari mmoja mmoja tofauti na michezo mingine.

Seti tofauti za viduara na mistari yake inatumika kutoa malipo, michezo ya bure, pamoja na bonus za michezo ya kujirudia.

Nembo zinazotumia katika mchezo huu.

Kuna aina tisa za alama zinazotumika katika mchezo huu wa Gems of Serengeti. Alama kuu inayobeba taswira ya mchezo huu ni kichwa cha mtu chenye pembe kilichonakishiwa kwa dhahabu.

Alama hii ionekanapo, huja na neno ‘’WILD’’ ambalo lenyewe hujitokeza kama maandishi. Alama hii hutoa malipo pale inapotokea katika kiduara chochote, kutegemeana na alama nyingine. Alama hii ina uwezo wa kutokea kwenye viduara vyote vya mistari, na hivyo kukupa uwezekana wa kukupa malipo makubwa.

Alama ya pili ni ile inayoitwa Scatter. Alama hii haitoi malipo ya moja kwa moja, bali inakupa mizunguko 10 ya bure pale ikitokea imetokea katika viduara namba 1,3,5 katika mchezo au mizungko ya kawaida.

Alama ya tatu ni ile ya ‘’Hold n Respin’’, alama hii haina malipo lakini inatokea katika mizunguko ya bure.

Alama ya nne ni Selo tupu(Empty Cell), wote tunajua selo ni chumba wanachowekwa maabusu. Hivyo alama hii ikitokea ina maanisha hakuna malipo. Alama hii hutokea kwenye michezo ya kawaida au mizunguko ya nyongeza yaani (Re Spin).

Narudi nyuma kidogo kwenye alama ya Hold n Re Spin ili uone selo na Hold Respin zinafanyaje kazi kwa pamoja.

Ikitokea unacheza mchezo huu wa Gems of Serengeti, alafu alama 5 za Hold n ReSpin zikatokea kwenye scrini yako, basi utazawadiwa michezo mitatu ya bure (3 free Spin awarded).

Katika michezo hiyo mitatu utakayocheza Hold n Respin, itakagua kila chumba cha selo ambacho ni kitupu, kuangalia kama kuna alama mpya za Hold n Re Spin zitajtokeza. Ikiwa alama ya Hold n Re Spin itajitokeza tena katika scrini basi utapata tena michezo mitatu ya bure.

Hali hii itaendelea tena mpaka pale ambapo hapatatokea tena alama ya Hold n Respin katika vyumba vya selo au kama alama za Hold and Spin zitajaa na kufunika scrini yote, kwa maana ya kuwa hizo alama kujaa katika mistari yote 20 katika mizunguko ya bure.

Mchezaji atajikusanyia kitita kinono cha pesa kadiri alama nyingi za Hold n Re spin zitakavyokuwa zinajitokeza na pesa kuzidishwa mara kiwango cha dau uliloweka, itakapofika mwisho wa mizunguko.

Ni matumaini yangu mchezo huu utakupa appetite ya kuucheza, pindi utakapouona katika tovuti sportpesa.co.tz ama App ya SportPesa.

Share this:
Back To Top