Wikiendi ndio hivyo inaanza leo ambapo, viwanja mbali mbali vinategemewa kuwa na shughuli mbali mbali za kimichezo hasa hasa mpira wa miguu ambao unafuatiliwa na mamilioni ya watanzania katika pembe zote za nchi yetu.
Habari kubwa wikiendi hii kwa hapa nyumbani ni mechi za ligi ya CAF za kombe la klabu bingwa Africa na Kombe la shirikisho Afrika ambapo Simba na Yanga, kuanzia kesho na kesho kutwa zitakuwa vibaruani kusaka nafasi ya kufuzu robo fainali kutoka hatua ya makundi.
Simba wao watawakaribisha Horoya ya Guinea, ambao wapo wote kwenye kundi C wakipishana kwa nafasi moja. Simba wapo nafasi ya 2 katika msimamo wa kundi C ambapo Raja Club Athletic anaongoza kundi akiwa na pointi kumi na mbili, baada ya kucheza mechi nne.
Iwapo Simba atashinda mechi yake ya kesho atafikisha pointi 9 ambazo zitamfanya aweze kufuzu kwenda hatua nyingine, kwani kwa mechi zilizobakia, Simba atabaki na mechi moja dhidi ya Raja Athletic kule Tunisia, ambapo hata akifungwa, si Horoya wala Vipers atakayeweza kuzifikia pointi za Simba, hivyo kufanya Simba kusonga mbele.
Kwa Upande wa Yanga wao wapo kundi D, wakiwa pamoja na US Monastir ya Tunisia, TP Mazembe ya DRC Congo, na AS Real Bamako ya Mali. Mpaka sasa Yanga ina pointi 7 nyuma ya US Monastir ambayo ina pointi 10, baada ya wote kucheza mechi 4.
Mechi ya Yanga dhidi ya US Monastir ni muhimu sana kushinda kwani itawahakikishia nafasi ya uhakika kwenda hatua ya robo fainali.
Kwingineko duniani leo kuna mechi katika ligi mbali mbali tukianzia na English Premier League, mechi za kusisimua ni pamoja na Nottingham Forest dhidi ya Newcastle. Hii ni mechi itakayopigwa katika uwanja wa City Ground na itachezwa kuanzia majira ya saa tano usiku.
Huko La Liga leo kuna mechi moja ya kusisimua ambapo timu ya Valladolid itamenyana na Club Athletic, ambapo Athletic yupo nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi, wakati Valladolid yupo nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi.
Bundesliga leo kuna mechi moja yenye mvuto ambapo timu ya Borussia Monchengladbach itapambana na Werder Bremen, katika mechi itakayopigwa katika uwanja wa Borussia Park kuanzia majira ya saa nne na dakika arobaini usiku.
Kule Italia, kwenye ligi ya Serie A, leo kuna mechi kati ya Sassuolo VS Spezia na Atalanta VS Empoli. Wote Sassuolo na Atalanta wanategemewa kushinda mechi zao.
Kule Ufaransa Ligie 1 kuna mechi kati ya Lyon VS Nantes, ambapo Lyon yupo kwenye nafasi ya kumi katika msisamamo wa ligi nchini Ufaransa, akiwa na matokeo yasiyoridhisha kwenye mechi 5 alizo kwishacheza hivi karibuni.
Nantes nao kwa upande wao wako katika nafasi ya 14 katika msimamo wa ligi, na katika mechi 5 walizocheza wameshinda moja, wamefungwa tatu na kutoa droo mechi 1. Kwa matokeo ha ya ni wazi timu ya Lyon inayo asilimia kubwa ya kupita
Tunaenda mpaka Uturuki kuangaza ligi ya huko nayo ina nini. Kule tunakutana na mechi moja ya kusisimua kati ya timu ya Konyaspor VS Glatasaray. Mechi hii itapigwa katika uwanja wa Konya Buyuksehir Arena, ambapo mara ya mwisho timu hizi mbili kukutana ilikuwa Septemba 16, 2022 na matokeo yalikuwa, Galatasaray ilishinda 2-1.
Tukirudi Afrika timu ya Cotton Sports ya Cameroon itakuwa inapambana na Al Ahly ya Misri ambayo Jumamosi iliyopita ilifungwa magoli 5-1 na Mamelodi Sundowns.
Al Merreikh ya Sudan itapambana na timu ya Esperance ya Tunisia, Jijini Khartoum, wakati CR Belouizdad ya Algeria itapambana na Zamalek ya Misri.
Kwa ufupi siku ya leo Ijumaa, kesho Jumamosi na Jumapili kuna mechi nyingi sana katika tovuti yetu SportPesa, ambazo tayari zimeshawekwa na zinakusubiria wewe, kuweka ubashiri wako na kusubiria mikwanja.
Kumbuka kuna multibet bonus, kuna Supa Jackpot ya mechi 17,16,15,14, na 13, ambayo mechi zipo tayari na kiwango chake kwa wiki hii ni 1,090,583,531.

