JE LIVERPOOL KUPINDUA MEZA LEO KWA REAL MADRID UEFA.
JE LIVERPOOL KUPINDUA MEZA LEO KWA REAL MADRID UEFA.
Leo ni moja kati ya siku nzuri ya kimichezo, ambapo katika ligi mbali mbali duniani, mechi za michuano, zitachezwa katika viwanja tofauti, hasa hasa barani Ulaya, ambapo mashindano ya UEFA Champions league yanaendelea katika viwanja mbali mbali.
Mechi kubwa na zenye msisimko siku ya leo ni ile inayopigwa leo usiku katika uwanja wa Santiago Bernabeu kati ya Real Madrid VS Liverpool na Napoli VS Frankfurt itakayopigwa katika uwanja wa Diego Armando Maradona, nchini Italia.
Mechi hizi mbili za leo, ni marudiano baada ya timu hizi kukutana kwenye mzunguko uliopita, na sasa zinarudiana, ambapo Liverpool ilifungwa magoli matano kwa mawili na Real Madrid na mechi ya Napoli dhidi ya Frankfurt ya Ujerumani, Napoli alishinda goli mbili bila.
Kama wadau wa michezo ya ubashiri wa michezo ya Soka, leo tumekuwekea mechi hizi mbili na zinginezo. Kwa sasa nitakuchambulia kidogo kuhusu timu hizi.
Timu ya Real Madrid imetokea kundi F ambapo katika msimamo wa kundi timu ya Real Madrid ilikuwa namba moja ikiwa na pointi 13 baada ya mechi 6, ambazo tayari imeshacheza.
Kwa upande wa Liverpool wao wametokea kundi A ambapo walikuwa wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa kundi, wakiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 6.
Timu zote hizi mbili, yaani Real Madrid VS Liverpool yeyote atakayeshinda anapita kwenda robo fainali ya kombe la klabu bingwa ya ligi ya Ulaya yaani (UEFA champions league).
Kwa namna ambavyo matokeo ya mechi ya kwanza yalikuwa, Real Madrid anapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele, ingawaje lolote linaweza kutokea kwani Liverpoool sio mgeni wa kupindua matokeo.
Kumbukumbu zinaonyesha, Liverpool ameshawahi kupindua matokeo msimu wa 2016/2017 baada ya kupata suluhu mchezo wa kwanza dhidi ya Dortmund ambapo walitoka 1-1 na baadae Liverpool akashinda 3-1 na kusonga mbele.
Rekodi ya kuvutia na ya kuvutia ya siku za karibuni kuwahi kushikiliwa na Liverpool kwenye hatua kama hii ya mtoani kuelekea makundi ni ya msimu wa 2018/2019 ambapo Liverpool alicheza na Barcelona Nou Camp na kufungwa 3-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza. Shughuli ilikuwa kwenye mechi ya marudiano mzunguko wa pili ambapo Liverpool aliishangaza dunia kwa kushinda magoli 4-0 dhidi ya Barcelona.
Hapa utaona Liverpool tayari ana mtaji wa magoli matatu na hivyo anahitaji magoli manne na asifungwe goli lolote ili aweze kusonga mbele kwenda hatua ya robo fainali.
Ni matumaini yetu mchezo utakuwa wa kuvutia na wenye ushindani mkubwa kuliko mechi ya kwanza ambapo Liverpool ilionekana kutokuwa makini baada ya kutangulia kuongoza mchezo huo kabla ya kufungwa magoli matano ya haraka haraka.
Mechi nyingine ni mechi kati ya Napoli VS Frankfurt, ambao nayo inapigwa leo majira ya saa tano za usiku na mechi hii inakutaniasha miamba miwili kutoka ligi ya Serie A Italia na ligi ya Bundesliga Ujerumani.
Tukianza na Napoli, wao mechi ya kwanza walishinda 2-0, dhidi ya Frankfurt, wikiwa ugenini, na hivyo tayari wanafaida ya magoli mawili ya ugenini, ambayo yalifungwa na Viktor Osimhen, mshambuliaji hatari wa Napoli kwa msimu huu akiwa na magoli 22, baada ya kucheza mechi 27, akiwa na assist 4 katika mechi zote alizocheza msimu huu.
Mchezaji Giovanni Di Lorenzo alifunga goli la pili, likiwa ni goli lake la kwanza kwa msimu huu katika mechi 25 alizocheza.
Tunategemea pia mechi hii kuwa na ushindani na tayari mechi hii ipo kwenye tovuti yetu.
Kwingineko duniani kutakuwa na mechi za ligi mbali mbali kama Southampton VS Brentford, Brighton VS Crystal Palace, Blackburn VS Reading, Hull City VS Burnley, Tottenham (W) VS Leicester City (W).
Kumbuka Supa Jackpot yetu imesimamia 1,090,583, 531, unaweza ku share mikeka yako na ndugu jamaa na marafiki kupitia Facebook, Twitter, Instagra, SMS na QR Code. Unaweza kucheza Supa Jackpot, na tayari timu zote zilizotajwa kwenye hii post zipo kwenye tovuti.
Nakukumbusha tu, kutoka katika tovuti yetu mechi hizi mbili yaani ya Real Madrid VS Liverpool na Napoli VS Frankfurt ODDS zake zimebustiwa.