Fundi Ujenzi wa kupaua nyumba, kutoka Mlandizi Stendi, Pwani Kenedy Kellya, ameibuka na kitita cha shilingi Milioni 10,124,322 katika Supa Jackpot bonus ya wikiendi iliyopita baada ya kupatia kwa usahihi mechi 15 kati ya 17 za Supa jackpot.
Akizungumza katika ofisi za SportPesa Oysterbay, Dar-Es-Salaam, Kenedy anasema alianza kucheza na SportPesa mwaka 2022, Mwezi wa tisa, baada ya kushwishika na washindi wa SportPesa waliokuwa wakitangazwa.
‘’Nilianza kucheza na SportPesa mwaka jana mwezi kama wa tisa, baada ya kushawishika na namna nilikuwa naona washindi wa SportPesa wakiwa wanatangazwa kupitia mitandao ya kijamii, taarifa za habari na kwenye magazeti.
Anaendelea kusema baada ya kushawishika alimuomba mshikaji wake (ambaye hakutaka kumtaja jina) amsaidie kupakua App ya SportPesa na baada ya kufanya hivyo alianza kucheza bila kukata tamaa.
‘’Mimi wakati naanza kucheza kwa mara ya kwanza nilikuwa nacheza michezo ya Kasino. Katika kucheza michezo hiyo ya Kasino nimewahi kushinda laki tatu ambazo zilinipa moyo ya kuwa naweza kupata zaidi’’. Anasema Kenedy.
Akizungumzia mkeka wake wa Supa Jackpot ulioshinda Kenedy anaelezea kwamba kwanza yeye sio mchezaji wa mara kwa mara wa ubashiri wa mpira. Lakini anajitahidi mara kwa mara kucheza Jackpot za SportPesa kila anapopata nafasi.
‘’Nikikusimulia kuhusu huu mkeka unaweza kushangaa. Siku niliyoweka huu mkeka uliyoshinda ilikuwa Jumatano iliyopita. Nilikuwa kijiweni pale Mlandizi Stendi nikamuomba rafiki yangu mmoja anipe hela niweke mkeka wa Supa Jackpot”.
“Mshikaji alinipa Sh 5000. Mara baada ya kuuweka huu mkeka ukatokea ubishani mkubwa sana. Niliwaambia washkaji zangu waweke mkeka kwa kuufuatisha na walikataa na kuniambaia haya mambo ya ubashiri ni uongo, watu wanapangwa na hata nikishinda sitalipwa’’.
Anaendelea kusema siku ya Jumamosi alifuatilia matokeo na kukuta amepatia kwa usahihi mechi 10 za Supa Jackpot kati ya 17. Baada ya hapo hakufuatilia tena mpaka ilipofika Jumatatu asubuhi, akiwa yeye na mkewe alichukua simu kutoka kwenye chaja na kukuta sms ya Hongera.
‘’Nafikiri asubuhi ya Jumatatu itabaki kwenye kumbukumbu zangu kwa muda mrefu. Cha kwanza sikutarajia kushinda kiwango hichi cha fedha. Cha pili baada ya kuona sms nilimuonyesa mke wangu nikamwambia nimeshinda, lakini kwa muda ule wenge lilishaaanza kuniingia mpaka kiwango nilichoshinda nikawa sikiamini. “
Mke wangu alinithibitishia mara mbili mbili kwamba nimeshinda Milioni 10 ila baada ya makato ni Milioni 9. Bado sikuamini hivyo nilitoka na Kwenda moja kwa moja maskani pale stendi na kumuonyesha jamaa yangu mmoja (jina kapuni) ambaye yeye ana kibanda cha kuonyesha mpira.
“Wakati nafika SportPesa nikapokea simu kutoka kitengo cha huduma kwa wateja wakimtaarifu kwamba anatakiwa afike ofisi za SportPesa ili suala lake lishughulkiwe. Kwa bahati nzuri alikuwa tayari ameshafika”.
Nilipokewa kwa ukarimu mkubwa na kuelekezwa kujaza fomu zenye maelezo yangu na kisha akaunti zikafunguliwa.

Kenedy anamalizia kwa kusema baada ya kupitia hatua zote za kujiridhisha na hivyo anawaasa watanzania kuiamini SportPesa kwani malipo ni papo hapo na pia wasikate tamaa waendelee kucheza kwani hakuna aijuaye siku yake.
‘’Sina maeneno mengi, washkaji zangu sasa wananiomba niwafundishe namna ya kucheza, baada ya wao kutilia mashaka kama nikishinda nitalipwa. Nawaomba mcheze ili na nyinyi mshinde kama mimi’’.
Naye mkuu wa kitengo cha Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya alimpongeza Kenedy na kumtaka akawe balozi mzuri wa SportPesa na pia aendelee na moyo huo huo alionao wa kuwafundisha watanzania wenzake, ili na wao waweze kushinda.
‘’Nikupe Hongera kwa kushinda Supa Jackpot Bonus ya milioni 10. Wewe ni mmoja kati ya washindi wengi ambao wanashinda kila wiki na kila siku. Supa Jackpot yetu wiki hii imesimamia 1,087,305,640.
Kucheza Jackpot ya SportPesa bofya hapa.

