skip to Main Content
SportPesa Supa Jackpot Ya Mechi 13/13, Milionea Kuondoka Na Sh. 248,672,790

SportPesa Supa Jackpot ya Mechi 13/13, Milionea kuondoka na Sh. 248,672,790

  • Mkulima Ashinda Sh 248,672,790 Supa Jackpot Ya SportPesa.
  • Supa Jackpot ya Mechi 13/13, Milionea  kuondoka na Sh. 248,672,790

 

Dar-Es-Salaam. 15 Februari 2023. Kampuni ya michezo, burudani na ubashiri SportPesa leo imemtambulisha rasmi mbele ya waandishi wa habari mshindi wa Supa Jackpot ya mechi 13/13 Japhet Msangawale mkazi wa Kijiji cha Sumbawanga, Rukwa.

Akizungumza katika jijini Dar-Es-Salaam, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tarimba Abbas aliwashukuru waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari kwa kujitokeza kwa wigi katika hafla hiyo.
‘’Nianze na kuwakaribisha na pia kuwashukuru ndugu waandishi kwa kufika kwa wingi katika ofisi zetu ili muweze kuwa habarisha watanzania, kuhusu mshindi wetu wa Supa Jackpot ya mechi 13 ambaye leo tunamtambulisha kwenu rasmi’’.


Mh Tarimba alichukua wasaa huo pia kumpongeza Japhet Msangawale Mamboleo, Mkulima na mkazi wa Rukwa kwa ushindi huo wa Sh 248,672,790 ambaye, alishinda pesa hiyo siku ya Jumapili usiku wa Tarehe 12 Mwezi wa pili, Mwaka 2023, majira ya saa tano usiku.

‘’Kama ilivyokuwa dhamira yetu tangu awali ya kuwawezesha watanzania ambao wanabashiri na kampuni yetu ya SportPesa, leo ninayo furaha ya dhati kumtambulisha na pia kumkabidhi mfano wa hundi ya pesa yake Japhet Msangawale Mamboleo ambayo ameshinda siku ya Jumapili usiku”

Mshindi huyu ni kijana mdogo wa miaka 25, ambaye kwa miaka takriban mitatu na zaidi alikuwa anajaribu kutimiza ndoto zake, na leo hii, ndoto hiyo si ya kusadikika tena, bali imekuwa ndoto ya kweli, kwa yeye kushinda fedha hizi kupitia mchezo wa Supa Jackpot ambao mechi zake huchezwa siku za mwisho wa wiki’’.

“Ninyi ni mashahidi wetu ambao tumekuwa tukiwaalika mara kwa mara kutambulisha ama kuwapa taarifa juu ya washindi wetu wengi ambao wanashinda vitita tofauti tofauti vya pesa ikiwemo washindi wa Multibet bonus, Mid-week Jackpot bonus, Casino na yule wa milioni 147 wa bet spinner Peter Mbawala wa kule Dodoma, ambaye alishinda Mwezi wa 12 2022.”

“Nitoe rai kwa watanzania kuiamini SportPesa kama ambavyo kijana Japhet alivyoiamini kampuni yetu na kupata ushindi huu wa Supa Jackpot. kwani washindi wengi wamepatikana kupitia bidhaa zetu nilizozitaja hapo juu.”

“Ni sehemu ya ahadi yetu kuu kwamba mshindi anapopatikana basi malipo yake hufanyika papo hapo hata mkimuuliza hapa tayari pesa iko kwenye akaunti yake”


Akizungumza katika hafla hiyo ya kumtambulisha na kumkabidhi mfano wa hundi, mshindi wa Supa Jackpot ya mechi 13, Japhet ameishukuru SportPesa kwa ushindi wake na pia kama sehemu ambayo imewezesha yeye kushinda kiasi kikubwa cha fedha ambacho pengine isingekuwa rahisi kwake kukipata katika mazingira yake ya kawaida.

‘’Nachukua fursa hii kutoa shukrani zangu za dhati kuwashukuru SportPesa kwa kunileta Dar-es-Salaam, na kwa mara ya kwanza nimepanda ndege, kitu ambacho nilikuwa sitegemei katika maisha yangu.”

“Mwanzoni nilikuwa siamini kama nitaipata pesa hii, lakini, baada kushinda nilipata sms ya kunipongeza kwa ushindi wa Jackpot na baadae usiku uleule nilipigiwa simu na mtoa huduma kwa wateja ambaye alinitaarifu juu ya ushindi wangu na kuniambia nitapigiwa simu ili nipewe utaratibu wa namna ya kuja Dar-es-Salaam, kuhakikiwa na kuthibitishwa na kisha kulipwa fedha zangu.”

‘’Nimefarijika sana kwa namna SportPesa walivyokuwa karibu na mimi kimawasiliano tangu niliposhinda usiku ule wa JumapiIi ya wiki iliyoisha. SportPesa wamenipa kila aina ya ushirikiano na kuhakikisha ninapata stahiki yangu kwa wakati’’.

Ikumbukwe tangu kuanzishwa kwake SportPesa imeshatoa washindi nane wa Jackpot na huyu Japhet anakuwa wa tis ana kila mshindi ni lazima alipe kodi, hata Japhet pia amelipa Sh 24,867,179.

 

Share this:
Back To Top