skip to Main Content
Muuza Kuku Azoa Tshs 14,817,786 Jackpot Bonus Ya Sportpesa
Mshindi wa Jackpot Bonus Noel Jacob Minyambi akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 14,817,786/- baada ya kubaashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 kwenye promosheni ya Bet Bonanza.

Muuza Kuku Azoa Tshs 14,817,786 Jackpot Bonus Ya Sportpesa

Mkazi wa Kitunda, Mwanagati, Wilaya ya Ilala, jijini Dar-es-Salaam, Noel Jackob Mnyambi, ameshinda Tshs 14,817,786 katika Jackpot Bonus ya Sportpesa iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyoisha, baada ya kupatia kwa usahihi mechi 12 kati ya mechi 13.

Akizungumza baada ya hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi katika ofisi za Sportpesa jijini Dar-Es-Salaam, Noel, ambaye pia anajishughulisha na biashara ya kuuza kuku anasema alianza kucheza na Sportpesa miaka miwili iliyopita.

Artboard- -copy- -

Mshindi wa Jackpot Bonus Noel Jacob Minyambi akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 14,817,786/- baada ya kubaashiri kwa usahihi mechi 12 kati ya 13 kwenye promosheni ya Bet Bonanza.

‘’Nakumbuka nilianza kucheza na Sportpesa mwaka 2020 baada ya kuwa naona matangazo na washindi kwenye mitandao na maeneo mengine, kama kwenye magazeti. ‘’Mimi huwa na desturi ya kuweka mikeka sio chini ya minane kila wiki.

Hii Jackpot nimeikosa kosa kidogo sababu timu moja ya Ufaransa nafikiri Le havre ndio wamenitibulia kunyakua mzigo huo wa bilioni na ushehe kwani mechi hiyo nilicheza dabo kombinesheni ya wa nyumbani Valenciennes ashinde au asuluhu, lakini alipigwa na Le Havre.

Anamalizia kwa kusema alikuja kujua kashinda siku ya Jumatatu asubuhi alipomka na kukuta meseji ya hongera. ‘’Baada ya sikukuu ya pasaka, nilikuwa nimeamka asubuhi na mapema nyumbani nikakuta sms ikinipa hongera kwa kushinda jackpot bonus.

‘’Hii pesa niliyoshinda nitaongeza kwenye mtaji wangu wa Kuku na pia nitamnunulia mke wangu kipande cha ardhi kama zawadi yake.

Akizungumza kwa niaba ya Sportpesa Meneja uhusiano na mahusiano Sabrina Msuya alimpongeza Noel kwa ushindi huo wa Jackpot bonus na kuwataka watanzania kuendelea kucheza kwani Jackpot imesimamia 1,171,243,460 wiki hii.

Taarifa zaidi kuhusu Sportpesa bonyeza hapa.

 

 

Share this:
Back To Top