skip to Main Content
Mshindi Bet Bonanza Aelezea Furaha Yake Ya Ushindi Wa 15,888,000/-
Mshindi wa promosheni ya Bet Bonanza akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 15,888,000/- baada ya kutangazwa rasmi kama mshindi wa kufungia promosheni hiyo.

Mshindi Bet Bonanza aelezea furaha yake ya ushindi wa 15,888,000/-

Mshindi wa droo ya mwsiho na kubwa ya Bet Bonanza ya Sportpesa George Jafari Kimaro, leo asubuhi alifika katika ofisi za Sportpesa kujitambulisha rasmi na pia kuzungumza nasi kuhusiana na ushindi wake huo na kutuelezea machache kumhusu yeye.

Akiongea ndani ya ofisi za Sportpesa George anasema, jana wakati anapokea simu ambayo ilimtaarifu kuhusiana na ushindi wake alikuwa mtaani kwake Lukobe akiwa amekaa na mzee mmoja (ambaye hakutaka kumtaja jina).

‘’Nilikuwa nimekaa na mzee wangu mmoja majira ya kuanzia saa tano na nusu nikasikia simu inaita. nilipoipokea kuna jamaa alijitambuslisha anaitwa Frank Gibebe na anapiga kutokea Sportpesa. Kwa muda ule sikuwa naelewa nini anataka kuongea na mimi, ila aliniuliza kama ninabashiri na Sportpesa’’.

SportPesa Bet Bonanza

Mshindi wa promosheni ya Bet Bonanza akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 15,888,000/- baada ya kutangazwa rasmi kama mshindi wa kufungia promosheni hiyo.

Anaendelea kusema baada ya swali hilo ilibidi asogee pembeni aongee na Gibebe ili kujua kulikoni, ndipo alipo ambiwa kwamba ameshinda zawadi kubwa ya Bet Bonanza kiasi cha Tshs 15,888,000 katika droo ya mwisho ambayo ilikuwa jana. ‘’Aliniuliza majina yangu na pia nipo wapi na nafanya shughuli gani’’.

‘’Pamoja na taarifa hizo jamaa aliniambia kuwa nitapigiwa simu punde baada ya kuongea nae. Kusema ukweli sikumuamini, ila kitu kimoja nilichofanya ni kuangalia namba za watoa huduma kwenye app ya Sportpesa na kuwapigia na kuuliza. Walinipa majibu ya matumanini kwamba kama ni kweli nimepigiwa basi nisubiri watawasiliana na mimi’’.

Anaendelea zaidi na kusema baada ya muda si mrefu alipigiwa simu tena na kuambiwa afike ofisi za Sportpesa siku ya Jumatano tarehe 13/4/2022 kwa hatua na taratibu zingine zinazofanywa kwa washindi.

Akiongelea kuhusiana na historia yake ya kubashiri na Sportpesa George anasema alianza kucheza mwanzoni mwa mwaka jana. ‘’Hapo kabla nilikuwa naijua Sportpesa kuanzia 2018, ambapo wakati nipo shule kuna vijana wenzangu walikuwa wanacheza sana, ila kwa wakati ule sikujishughulisha nayo.

Anaongezea kwa kusema kwamba mzanzoni alikuwa anatumia simu ya tochi lakini akakuta baadae kwenye uchaguzi ana uwanda mdogo hivyo ilimlazimu kutafuta simu janja ambayo ndio anayotumia mpaka leo.

‘’Unajua Sportpesa wako vizuri  kwenye app yao na malipo yao ni fasta ndio vinavyonivutia zaidi.Mimi nacheza zaidi maltibet na nimewahi kushinda kama mara 4 mpaka 5 kabla ya ushindi huu. Nakumbuka kiwango cha juu mimi kushinda ilikuwa laki 6, hiyo ilikuwa mwezi wa kumi.

Akizungumzia pesa aliyoshinda ni nini ataifanyia George anasema yeye ni fundi ujenzi msaidizi lakini hiyo haimzuii kununua boda boda na pia kuongeza mtaji kwenye biashara yake ya mitumba na pia nyingine atawapatia familia yake.

George amewashauri watanzania na wachezaji wenzake waiamini Sportpesa kwani ni ya uhakika na hakuna longolongo katika malipo.

 

 

 

Share this:
Back To Top