MWANACHUO UDOM ASHINDA JACKPOT BONUS MIL 8
- MWANACHUO ASHINDA JACKPOT BONUS MIL 8
Waswahili wana msemo, ‘’mgaa gaa na upwa hali wali mkavu’’, hivi ndivyo methali ya wahenga ilivyotimia, kwa kijana Hamisi Moshi Masanja, baada ya kuibuka na ushindi wa Tsh 8,189,223, baada ya kushinda mechi 11, kati ya 13, katika Jackpot Bonus ya Sportpesa ya wikiendi iliyokwisha.
Khamisi (26), ni mwenyeji wa Kahama mkoani Shinyanga, ambaye kwa sasa anaishi Dodoma, akiwa masomoni chuo kikuu cha UDOM, akifanya shahada ya biashara akibobea kwenye masoko.

Mshindi wa Jackpot bonus wa mechi 11 Moshi Hamis Masanja akishikilia mfano wa hundi ya shilingi 8,189,223.
Akiongea katika ofisi za Sportpesa, jijini Dar-Es-Salaam, baada ya utambulisho na makabidhiano ya mfano wa hundi, Hamisi anasema juhudi yake ya kucheza na kutokata tamaa, ndizo zilizompatia ushindi.
‘’Unajua nimeanza kucheza na Sportpesa miaka mitatu iliyopita, na kwa muda wote huo, nimekuwa najaribisha bahati yangu bila kuchoka. Mfano wiki ile ya nyuma, nilishinda mechi nne tu, kati ya kumi na tatu. Lakini sikukata tamaa na kuacha kucheza’.
Nilikuwa navutiwa sana, kwa namna niliyokuwa naona vijana wenzangu, walivyokuwa wanashinda mara kwa mara’’.
Anaendelea kwa kusema alikuwa na mazoea ya kuperuzi kurasa za mitandao ya kijamii ya Sportpesa na kuona washindi kila mara. ‘’Nilihamasika sana kwa jinsi nilivyoona wenzangu wakiwekwa kwenye kurasa za Instagram, Facebook na Twitter za Sportpesa,
Nilitamani na mimi siku moja nibahatike kutokea, na kweli leo na mimi ni mmoja wa washindi’’.
Akielezea namna alivyocheza Jackpot ya wikiendi iliyoisha ambayo ndio iliyompatia ushindi, Khamisi anasema aliziona mechi za ushindi siku ya Jumatano iliyopita na kisha alijipa siku mbili za kufanya tathmini na uchambuzi wa kina.
‘’Unajua siku ya Jumatano nilifungua Sportpesa App na kukuta timu kumi na tatu zilizowekwa kwa ajili ya Jackpot. Niliangalia na kufuatilia mwenendo wa kila timu zilizowekwa na kujua namna ya kuzicheza.
Anaendelea kwa kusema, siku ya Ijumaa majira ya saa saba mchana, baada ya kutuliza kichwa alipanga mkeka wake. Anasema ‘’Kati ya timu kumi na tatu, niliweka timu tisa ili zishinde na timu nne zitoe droo. Kati ya hizo mpaka Jumamosi usiku kati ya timu kumi, timu nane zilipata matokeo niliyoyataka’’.
Hapo nilipata matumaini kidogo, ingawa kwangu mimi kupata wastani wa timu saba mpaka timu tisa kwenye Jackpot, kilikuwa ni kitu cha kawaida sana. Sikushtuka wala kuhamaki, ila nilikuwa nasubiria tu mechi tatu zilizokuwa zimesalia kucheza.
Wakati naingia kulala, moja kati ya mechi tatu zilizosalia Waalwijk dhidi ya Fortuna Sittard ilianza. Dakika ya pili tu ya mchezo Waalwijk wakapata bao. Baada ya hapo nilipitiwa na usingizi na nilipokuja kuamka asubuhi nilikutana na meseji ya hongera umeshinda Jackpot Bonus ya Sportpesa.
Hamisi ambaye pia ni mfanyabiashara ya mpunga, amewaasa watanzania kutokata tamaa na kujaribu bahati yao na Sportpesa kila wanapopata nafasi, kwani ndio njia pekee ya uhakika ya kushinda. ‘’
‘’Ninawaomba vijana wenzangu na watanzania kwa ujumla wachezena Sportpesa kuanzia multi bet, single bet na hata hii Jackpot ambayo nimeshinda mimi timu kumi na moja.
Naye Meneja Uhusiano wa Sportpesa Sabrina Msuya amewaasa watanzania kutokata moyo na kujaribisha bahati yao kwa kucheza.
‘’Niwaombe sana kujaribu bahati zenu kwani Jackpot sasa imepanda wiki hii mpaka Tsh 878,152,880’’. Lakini hata kama hujabahatika kushinda Jackpot bas Jackpot bonus inakusubiri kwa watakaobashiri kwa usahihi mechi 10 hadi 12.
“Wiki hii SportPesa imepata jumla ya Washindi 59 wa Jackpot bonus kwa Washindi waliobashiri kwa usahihi mechi 10 hadi 12 ambapo mechi 12 amepata Tsh. 23,397,780, mechi 11 amepata bonus ya Tsh. 8,189,223 na mechi 10 amejishindia Tsh. 693,267”
Kufahamu washindi mbalimbali wa Jackpot bonus angalia hapa.