skip to Main Content
SportPesa Yazindua Rasmi Lucky Numbers/Nambari Za Bahati.

SportPesa yazindua rasmi Lucky Numbers/Nambari za Bahati.

Zaidi ya michezo 160 ya Lucky Numbers kutoka sehemu mbalimbali.

Droo huchezwa kila dakika.

Kampuni ya michezo na kubashiri SportPesa imezindua rasmi bidhaa yake mpya ya Lucky Numbers (Namba za bahati) mwezi huu ikiwa na nia ya kutanua wigo la michezo na kuwapa nafasi wateja wake kufurahia mchezo huo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi Meneja Uhusiano na Mawasiliano Sabrina Msuya alisema “Tumezindua huduma hii ikiwa na michezo zaidi ya 160 yenye masoko zaidi ya 14 kwa ajili ya wateja wetu kuwa na wigo mpana wa kucheza. Kumbuka kuwa hizi ni droo zinazochezwa sehemu mbalimbali duniani na matokeo yake sio ya siri”

Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya akifafanua jambo wakati wa uzinduzi wa bidhaa Yao mpya ya Lucky Numbers.

Jinsi ya Kucheza.

Mteja wa SportPesa anaweza kucheza Nambari za Bahati akiwa amejisajili na kuweka pesa kwenye akaunti yake.

Cheza mchezo wa Nambari za Bahati/Lucky Numbers kwa kuchagua mchezo uupendao kwa kuzingatia muda uliopangwa kucheza, baada ya kuchagua utapokea masoko zaidi ya 14 yanayopatikana kulingana na droo uliyochagua.

Weka dau lako kwa kuweka kiasi cha kucheza kisha weka ubashiri wako. Mara baada ya droo kuchezwa matokeo hupatikana kwenye tovuti na APP yetu.

“Kima cha chini cha kucheza Nambari za bahati ni kuanzia shilingi 50 za kitanzania na unaweza kujishindia mamilioni kupitia hicho kiwango.

“Aina hii ya mchezo ni burudani ambayo inakupa nafasi wewe kama mteja wetu kushiriki kwenye droo za kimataifa kulingana na bahati yako.”

“Ni wakati wetu sasa kujifunza vitu vipya na kufurahia mchezo huu wenye kukupa nafasi ya kujishindia fedha nyingi zaidi kwa dau la shilingi 50.

Huduma hii inapatikana kupitia tovuti yetu Pamoja na APP yetu kwa mitandao yote ya simu.

Mwisho!!

Share this:
Back To Top