skip to Main Content
SportPesa, Tigo Pesa, Airtel Money Na M-Pesa Wazindua Promosheni Ya Mshiko Deilee.

SportPesa, Tigo Pesa, Airtel Money na M-Pesa wazindua promosheni ya Mshiko Deilee.

  • Washindi Zaidi ya 913 kwa mwezi mzima.
  • 10,000Tzs kila siku, 1,000,000 TZS kila wiki na mshindi wa mwisho wa kuondoka na 15,888,000 TZS.

Alhamisi Juni 10,2021. Kampuni ya michezo na burudani SportPesa wamezindua kampeni maalumu kwa ajili ya mechi za mwezi huu.

Promosheni hii imezinduliwa leo katika ofisi zao Masaki, Dar es Salaam ikihusisha makampuni ya mitandao ya simu Tigo, Vodacom na Airtel ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja hasa katika kipindi hiki cha mechi za Euro na mechi zingine zinazoendelea ikiwepo Copa America na VPL.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Meneja Uhusiano na Mawasiliano alisema katika kipindi hiki tumeona tuwazawadie wateja wetu wote kwa kuzindua promosheni inayoenda kwa jina la “Mshiko Deilee”.

Promosheni hii inaanza rasmi kesho tarehe 11 mwezi huu na kumalizika mwezi ujao tarehe 11. Kutakuwa na washindi wa kila siku ambao watajishindia kiasi cha shilingi elfu 10 kila mmoja kwa watu 30, pia tutatoa shilingi milioni 1 kila wiki kwa washindi wa 3 na mwisho wa promosheni tutatoa 15,888,000/- kwa mshindi mmoja mwenye bahati”.

“Droo zitachezwa kila siku na washindi watatangazwa kupitia kurasa zetu za Instagram na Facebook, kurasa za washirika wetu ambao ni Tigo, Vodacom na Airtel, pamoja na kurasa za timu za Simba na Yanga”

“Ili kushiriki kwenye promosheni hii ni lazima kuweka pesa kuwenye akaunti yako ya SportPesa kisha kuanza kucheza ili kuingia kwenye droo na kupata nafasi ya kuibuka mshindi, kwa wateja wapya watatakiwa kujisajili kwanza kisha kufuata mtirirko huo huo”.

“Napenda kuwakaribisha watumiaji wa mitandao yote kushiriki kwenye promosheni hii hata wale ambao hawajajisajili na SportPesa ili waweze kushinda zawadi za kila siku, kila wiki na zawadi kubwa kabisa ya zaidi ya shilingi milioni 15”.

Washirika wa promosheni

Kutoka kushoto Meneja biashara TigoPesa Fabian Felician ,Meneja Mauzo Mpesa Kelvin Nyanda , Meneja Uhusiano na Mawasiliano SportPesa Sabrina Msuya na msimamizi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Joram Mtafya kwenye uzinduzi wa promosheni ya Mshiko Deilee ya SportPesa itakayodumu kwa muda wa mwezi 1, ambapo mshindi mkubwa atashinda 15,888,000/-

Akizungumza kutoka Tigo Meneja biashara, TigoPesa Fabian Felician alisema,

“Katika msimu huu wa mechi za Euro na zinginezo tumeona ni vizuri kushirikiana na washirika wetu SportPesa ili wateja wetu wa Tigo Pesa waweze kubashiri kwa urahisi na kupata nafasi ya kujishindia mamilioni ya pesa”

Kushiriki ni rahisi, mteja wa Tigo Pesa anapaswa kujisajili na Sportpesa,  na kuweka pesa kwenye akauti yake ya SportPesa kupitia huduma ya Tigo Pesa, kubashiri  mechi anayoipenda na kupata nafasi ya kuingia kwenye droo ili kujishindia zawadi za kila siku, wiki na hatimae zawadi ya mwisho wa promosheni ambayo ni shilingi 15,888,000/-.”

“Kumbuka mteja wa Tigo kupitia huduma ya Tigopesa anaweza kuweka pesa kwenye akaunti ya SportPesa kwa kupiga *150*01# au kupitia Tigo Pesa App.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa M-Pesa, kutoka kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC Kelvin Nyanda alisema, mbali ya kuwa ligi hii ni ya muda mchache, lakini itawapa fursa watumiaji 10 kila siku kujinyakulia kiasi cha shilingi elfu 10 kila mmoja, na hivyo kupata washindi 310 kwa mwezi mzima.

Kushiriki ni rahisi sana, kila mteja wa M-Pesa ana nafasi ya kushinda katika kipindi hiki kwa kuingia kwenye menyu ya malipo ya M-Pesa kisha chagua lipa bili, halafu michezo, kisha SportPesa, halafu fuata maelezo.

Ukimaliza utapata majibu papo hapo kuwa umeingia kwenye droo ya siku/wiki/mwezi, na washindi watapigiwa simu kujulishwa kuwa wameshinda na majina yatatangazwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii (Social media pages) za SportPesa.

“Napenda kuchukua nafasi hii kuwakaribisha wateja wetu kushiriki mara nyingi wawezavyo, maana ushindi upo kwa ajili yao sababu ya “Mshiko Deilee” alimaliza.

 

Share this:
Back To Top