skip to Main Content
Milioni Tatu Zatolewa Wiki Ya Kwanza-Mshiko Deilee
Kushoto Mtangazaji Frank Charles, Aggrey Charles Meneja Airtel Money Biashara, Sabrina Msuya Meneja Uhusiano SportPesa na Kelvin Nyanda Meneja huduma ya Mpesa wakichezesha droo ya mshindi wa wiki ambao wamejishindia kiasi cha milioni 1 kila mmoja kupitia promosheni ya Mshiko Deilee. Promosheni bado inaendelea na kila siku SportPesa inatoa washindi 30 kutoka kila mtandao.

Milioni tatu zatolewa Wiki ya kwanza-Mshiko Deilee

DROO ya wiki ya kwanza ya Promosheni ya SportPesa inayojulikana kama Mshiko Deilee imechezeshwa leo na washindi watatu wamepatikana kwa kila mmoja kujishindia Shilingi 1, 000, 000.

Washindi hao wamepatikana baada ya kubashiri kupitia mitandao ya simu kupitia huduma ya Airtel Money, TigoPesa na Mpesa.

Mshindi wa kwanza aliyejinyakulia Shilingi 1, 000, 000 kupitia Tigo ni Noel Changwa, 25 kutoka mkoani Songea Mjini baada ya kubashiri kwa kupitia Tigopesa.

Na mshindi wa pili ni kutoka mtandao wa Vodacom ambaye ni mwanamke Jacky Abraham kutoka Goba, Dar es Salaam aliyebashiri na SportPesa kupitia Mpesa.

Mshindi mwengine watatu wa mwisho ni kupitia mtandao wa Airtel ni Jeremia Rrenatus wa Bunda, Mara aliyebashiri na SportPesa kupitia Airtel Money.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Uhusiano wa SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya alisema kuwa leo alisema kuwa bado promosheni hiyo inaendelea kwa wiki sita ambayo kila wiki watatoka watatu kupitia mitandao ya Tigo, Airtel na Vodacom.

“Leo tumeweza kupata washindi watatu kutoka mitandao ya Tigo, Vodacom na Airtel bado kuchezesha droo ya kwanza kabisa.

“Kikubwa wateja wetu waondoe hofu ya matapeli kwani simu yetu tunayoitumia kuwapigia washindi imesajiliwa na SportPesa, hivyo wateja wetu waondoe hofu.

“Droo yetu hii inaendelea kwa washindi watatu wa wiki kabla ya droo kubwa itakayokuwa ya mwisho na mshindi atayepatikana atajishindia Sh 15,888,000.

“Hivyo kila wiki watatoka washindi watatu watakaocheza na SportPesa kupitia mitandao ya Tigo, Vodocom na Airtel kwa muda wa mwezi mmoja,” alisema Sabrina.

Baada ya droo hiyo kuchezeshwa, Meneja wa Huduma ya MPESA, Kelvin Nyanda alisema kuwa “Nampongeza Jacky na washindi wengine waliocheza kwa kushinda mtandao wa Airtel na mitandao mngine. Hivyo niwatake wateja wetu kuendelea kucheza na SportPesa kupitia ili washinde na Promosheni ya Mshiko Deilee.

Kwa upande wa Meneja wa Biashara wa Airtel, Aggrey Charles alisema kuwa “Nampongeza mshindi wetu kutoka Bunda, hivyo niwatake wateja wetu kuendelea kucheza na Airtel kupitia huduma yetu ya Airtel Money ili nao wawe washindi.

Mpaka sasa SportPesa imetangaza jumla ya washindi 210 wa 10,000 za kitanzania kila siku.

Share this:
Back To Top