JKT Tanzania vs Simba SCJKT Tanzania (-)JKT Tanzania (-)

Libasse
Libasse Gueye nyota wa Simba SC

JKT Tanzania vs Simba SC | Pamba Jiji FC vs Coastal Union | Live score | Prediction

  • NBC Premier League mechi tatu kupigwa ikiwemo JKT Tanzania vs Simba SC, Pamba Jiji FC vs Coastal Union na Dodoma Jiji FC vs Fountain Gate., 21/11/2026
  • Fountain Gate ipo nafasi ya 15 na pointi 6 baada ya mechi 11 inakutana na Dodoma Jiji FC iliyo nafasi ya 6 na pointi 16.
  • Kwa habari za papohapo za JKT Tanzania vs Simba SC fuatilia SportPesa Blog, huku SP Score ikikuandalia livescores.

Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo baada ya mapumziko mafupi, JKT Tanzania vs Simba SC ukiwa ni mchezo unaosubiriwa kwa shauku kubwa.Hii inatokana na ushindani kwa timu hizi mbili na rekodi ya mnyama kucheza mechi 10 bila kupoteza. Mbali na mchezo huu utakaopigwa Uwanja wa Mej.Gen.Isamuyo pia Pamba Jiji FC vs Coastal Union na Dodoma Jiji FC vs Fountain Gate.

SOMA HII PIA:JKT Tanzania: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.

image

JKT Tanzania vs Simba SC na ratiba za leo

Wakati mechi 3 zikitarajiwa kupigwa mchezo mzito ni JKT Tanzania vs Simba SC kuna mapambano mengine makubwa mawili yanapigwa.Ikumbukwe kwamba Steve Barker Kocha Mkuu wa Simba SC ameongoza kikosi katika mechi 10 bila kupoteza.Jambo hilo linaongeza mvuto wa mchezo kusubiri maajabu kutoka kwa JKT Tanzania kuandika rekodi ya kuifunga ama kupoteza baada ya dakika 90.

Pamba Jiji FC vs Coastal Union itapigwa saa 10:00 jioni

JKT Tanzania vs Simba SC itapigwa saa 12:30 jioni

Dodoma Jiji FC vs Fountain Gate, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma saa 3:00 usiku.

Umuhimu wa raundi hii kwa timu kubwa

Muda wa mavuno kwa timu kusaka ushindi ndani ya dakika 90.JKT Tanzania inapambana kumaliza ndani ya 4 bora inakutana na Simba SC inayosaka taji la lili lililo mikononi mwa Yanga SC.Kila timu inaingia uwanjani kwa hesabu zake.

Pamba Jiji FC inapambana kujinasua kutoka kushuka daraja ina pointi 6 nafasi ya 14.Coastal Union nafasi ya 10 ina pointi 11 bado haijawa kwenye mwendo mzuri.Fountain Gate hali ni mbaya inapambana kutoshuka daraja.Imekusanya pointi 6 baada ya mechi 14.

Dodoma Jiji FC nafasi ya 6 ina pointi 16.Kila pointi tatu raundi hii ni muhimu jambo linaloongeza ushindani ndani ya ligi.Hakuna timu nyepesi zote zipo imara.

SOMA HII PIA:Simba SC vs JKT Tanzania NBC Premier League | H2H, takwimu, utabiri, 6 kukosekana | SportPesa Blog

Nini cha kutarajia kutoka kwa wachezaji na makocha

Wachezaji wanatarajiwa kuonyesha kiwango cha juu cha utendaji baada ya mapumziko. Makocha nao watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha timu zao zimejiandaa vyema kimwili na kiakili.Mbinu mpya za kiufundi zinaweza kuonekana leo, huku kila kocha akijaribu kutafuta njia ya kuwashinda wapinzani wao.

Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema wamefanya maandalizi mazuri kwa mchezo dhidi ya JKT Tanzania.Aliongeza kuwa wachezaji wapo tayari na wanatarajia kupambana kupata ushindi ugenini.

“Tunatarajia kuwa na mchezo mgumu dhidi ya JKT Tanzania.Kikubwa ni kuwa tayari na kila mchezaji anatambua umuhimu wa pointi tatu.Tuna amini tutafanya kazi kubwa na tunawaheshimu wapinzani,”.

Kocha Mkuu wa JKT Tanzania, Ahmad Ally amebainisha kuwa wamejiandaa kiakili na kisaikolojia.Alibainisha kuwa wapo tayari kwa mchezo dhidi ya Simba SC.Kocha huyo aliongeza anatambua wapinzani wao ni timu kubwa.

“Simba SC ni timu kubwa si ndani ya Tanzania bali Afrika.Huu mchezo utakuwa fursa kujifunza na kupima uwezo kwa wachezaji.Tuna amini tutakuwa na wakati mzuri uwanjani,”.

Hitimisho

Katika ratiba ya leo JKT Tanzania vs Simba SC ni moja ya mechi kali kati ya zile 3.Dodoma Jiji FC vs Fountain Gate hii itakuwa kete ya funga kazi.Pamba Jiji FC vs Coastal Union pambano la kwanza kabisa leo Novemba 21,2026.

Share this: