Michael Carrick: Mechi 9 zinazomuondoa Carrick Manchester United, EPL 2026/27, Lives core, taarifa za timu
- Mambo yanazidi kuwa mabaya kwa, Michael Carrick ndani ya kikosi cha Manchester United kufuatia taarifa kuwa kocha huyo atafukuzwa muda wowote kuanzia sasa.
- Taarifa hizi zinakuja wakati timu hiyo ikipitia kipindi kigumu cha kucheza mechi 10 bila ushindi na wakiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi Kuu England EPL.
- Mabosi na wamiliki wa Manchester United, wanatajwa kumalizana na kocha Mauricio Pochetino, huku tamko la kuhusu hatima yake liikisubiriwa kwa hamu.
- Makala hii inachambua kwa ufupi kinachoendelea katika viunga vya Manchester.
Hali ya mambo inazidi kuwa mabaya kwa, Michael Carrick ndani ya kikosi cha Manchester United kufuatia taarifa kuwa kocha huyo atafukuzwa muda wowote kuanzia sasa. Taarifa hizi zinakuja wakati timu hiyo ikipitia kipindi kigumu cha kucheza mechi 9 bila ushindi na wakiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi Kuu England EPL. Mabosi na wamiliki wa Manchester United, wanatajwa kumalizana na kocha Mauricio Pochetino, huku tamko la kuhusu hatima yake liikisubiriwa kwa hamu.
SOMA HII HAPA: Michael Carrick kufukuzwa Manchester United! : EPL 2026/27, Lives core, taarifa za timua
Nini kinaendelea ndani ya Manchester United?

Katika hali ambayo haikutarajiwa na wengi Chini ya uongozi wa Michael Carrick, Manchester United imekuwa ikipitia kipindi kigumu msimu huu ambacho hakijawahi kushuhudiwa kwa zaidi ya miaka 40. Timu hiyo kwa sasa inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza 2026/27, hali inayoashiria mwanzo mbaya wa msimu. Mchezo wa mwisho timu hiyo iliponea chupuchuppu kupokea kichapo cha mbele ya Aston villa na mchezo kuisha kwa sare ya 4-4.
Shinda mpaka zaidi ya Shilingi Milioni 800, cheza kindege ‘aviator’ sasa gusa hapa chini
Mechi 9 zazua balaa
Matokeo ya sare ya mabao 4-4 waliyopata Manchester United vs Aston Villa yanaifanya timu hiyo kufikisha mechi 9 bila ushindi. Hii inafanya ukosefu huo wa ushindi uwe wa kwanza ndan ya miaka 40. Kati ya mechi hizo, mechi 8 ni mechi za Ligi Kuu England yaani EPL.
Mabosi wamalizana na Pochettino

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Manchester United zinathibitisha kuwa mabosi watimu hiyo wamefikia uamuzi wa kumfuta kazi kocha Michael Carrick na kumalizana na kocha wa zamani wa Spurs, Mauricio Pochettino. Kulingana na ripoti mbalimbali, viongozi wapya wa Manchester United, Omar Berrada na Jason Wilcox, wametoa mapendekezo yao kwa wamiliki, Sir Jim Ratcliffe na familia ya Glazers.
SOMA HII ZAIDI: Manchester United: Ratiba, kikosi, usajili na matarajio msimu wa 2026/27
Kwanini Pochettino?

Maswali yamekuwa mengi juu ya kwanini uongozi wa Manchester United wanakaribia kumalizana na Pochettino. Taarifa zinaeleza kuwa hii inatokana na uzoefu mkubwa wa kufundisha vilabu vikubwa barani Ulaya na anajulikana kwa falsafa yake ya soka ya kushambulia. Falsafa, ambayo inaweza kuwavutia mashabiki wa United wanaotamani kuona timu yao ikirejea kwenye ubora wake.
SOMA HII PIA: Manchester United 4-4 Aston Villa, Premier League 2026/27 | Highlights | SportPesa Blog
Hitimisho
Sakata la kocha Michael Carrick kufukuzwa Manchester United linazidi kuwachanganya wengi kati ya mashabiki wa timu hiyo ambao wanaamini kuwa kocha huyo hana makosa, bali uongozi unatakiwa kuondoka. Uamuzi wa mwisho kuhusu Michael Carrick utakuwa na athari kubwa kwa mwelekeo wa klabu msimu huu na miaka ijayo. Mashabiki wanatumai kuwa uamuzi wowote utakaofanywa utaleta utulivu na mafanikio kwa timu yao pendwa, endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa taarifa zaidi.


