Orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27 | Jabir na Peter Shalulile kwenye vita | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

November 7, 2026
Orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27Jabir AnuaryJabir Anuary
  • Anuary Jabir wa Polisi Tanzania anaongoza orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27.
  • Peter Shalulile raia wa Afrika Kusini mshambuliaji wa Yanga SC amefunga mabao 6 yupo nafasi ya pili.
  • Elie Mpanzu na Clatous Chama wote wa Simba SC wamefunga mabao 4 kwenye ligi.
Orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27
Peter Shalulile mshambuliaji wa Yanga SC

Hapa tumekuletea orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27.Kinara ni Anuary Jabir wa Polisi Tanzania akiwa amefunga mabao 7.Peter Shalulile mshambuliaji wa Yanga SC yeye ni namba mbili akiwa amefunga jumla ya mabao 6.Vita inazidi kuwa kali kwa kila mchezaji ndani ya uwanja kutimiza majukumu yake.

SOMA HII PIA:Matokeo ya Ligi Kuu ya NBC 2026/27 | Man of The Match | Maxi Nzengeli | Nathaniel Chilambo | Msimamo| SportPesa Blog

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.

Hii hapa orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27

Kwenye orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27 kinara ni mzawa Anuary Jabir ambaye yupo kikosi cha Polisi Tanzania.Nyota namba mbili ni raia wa Afrika Kusini Shalulile.Bado vita ni mbichi kutokana na kila mchezaji kuwa na mechi nyingi za kucheza.Nani ataibuka mfungaji bora?

MchezajiTimuMechiDakikaPenatiMabao
Anuary JabirPolisi Tanzania1189947
Peter ShalulileYanga SC967006
Herbert LukindoNamungo FC847915
Obrey ChirwaGeita Gold970225
Clatous ChamaSimba SC966104
Elie MpanzuSimba SC1070804
Anicet OuraSimba SC1080904
Ani ElijahTRA United956714
Abdul SopuAzam FC738434
Oscar MwajangaMbeya City733803

Kwa upande wa Simba SC kuna mastaa wawili wenye mabao mengi.Clatous Chama na Elie Mpanzu hawa wote ni viungo wakiwa wamefunga mabao 4.Mshambuliaji Ibrahim Doumbia raia wa Mali yeye hajafungua bado ukurasa wa mabao ndani ya kikosi cha Simba SC.

SOMA HII PIA:Timu bora zilizofunga ndani ya boksi la 18 Ligi kuu ya NBC Tanzania 2024/2025- Azam FC, Simba SC na Yanga Sc ni balaa

Hitimisho

Ni orodha ya wafungaji NBC Premier League 2026/27 inazidi kupasua anga kila leo.Mwanzo alianza kuongoza Obrey Chirwa ambaye amefunga mabao 5.Anuary Jabir anavutwa kwa kasi kubwa na mshambuliaji wa Yanga SC, Peter Shalulile akiwa amefunga mabao 6 tofauti ya bao moja pekee.

Share this: