Vita ya wakubwaVita ya wakubwa
  • Ni siku 10 tu, zimesalia kabla ya kufunguliwa kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Morocco.
  • Mashindano ya mwaka huu yatafanyika Morocco, ambapo yataanza kutimua vumbi Desemba 21, 2025.
  • Hii ni mara ya pili kwa nchi hiyo, kuhodhi mashindano haya makubwa. Makala hii inakuletea mastaa 5 wanaotabiriwa kufanya makubwa.

Siku 10 tu, zimesalia kabla ya filimbi kupulizwa kuashiria kufunguliwa kwa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 Morocco. Mashindano ya mwaka huu yatafanyika nchini Morocco, ambapo yataanza kutimua vumbi Desemba 21, 2025. Hii ni mara ya pili kwa nchi hiyo, kuhodhi mashindano haya makubwa. Makala hii inakuletea mastaa 5 wanaotabiriwa kufanya makubwa katika mashindano hayo.

SOMA HII PIA: AFCON 2025: Joto lapanda Morocco, Jeshi la Tanzania laweka kambi Misri

Je, bado hujashinda? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Mastaa 5 wanaotabiriwa makubwa AFCON 2025 Morocco

AFCON ndiyo mashindano makubwa zaidi ya soka barani Afrika, Hivyo kunatarajiwa mkusanyiko wa vipaji vya juu vyenye asili ya barani Afrika vinavyowasili Morocco. Kutokana na hili jicho la dunia hukazia zaidi, kuliko wakati mwingine wowote. Lakini miongoni mwa mastaa wote wanaotarajiwa Morocco, majina haya matano yanatajwa zaidi:

Achraf Hakimi (Morocco)

Hakimi
Hakimi

Baada ya kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika mwezi uliopita, Achraf Hakimi anaendelea kuuguza jeraha alilopata akiwa na PSG. Taarifa za kitabibu zimethibitisha kuwa anatarajiwa kupona kwa wakati na kushiriki AFCON. Hakimi ataiongoza Morocco kama taifa mwenyeji. Kwa sasa beki huyo wa PSG yuko katika kilele cha ubora wa kiwango chake. Tabia ya uongozi, kasi na ushawishi mkubwa upande wa kulia vinamfanya kuwa silaha muhimu ya Morocco.

Uwezo wake wa kuzuia, kushambulia nafasi na kubadilisha ulinzi kuwa hatari unamfanya kuwa mchezaji wa pembeni anayehofiwa zaidi katika mashindano haya. Mbele ya mashabiki wa nyumbani, Hakimi ana kila kitu cha kuandika historia. Hasa baada ya kuwa na msimu bora akiwa na PSG.

SOMA HII ZAIDI: AFCON 2023: Your guide to the games, Groups, Fixtures, Venues & everything you need to know

Mohamed Salah (Misri)

Salah (-)
Salah

Kwa sasa anapitia wakati mgumu ndani ya kikosi cha Liverpool, hii ni kutokana na mahusiano na kocha wake kuingia doa. Majibizano ya maneno kati yao yameshuhudia staa huyo akipigwa benchi mechi 3 mfululizo, huku mechi dhidi ya Inter Milan akiachwa kabisa kwenye listi ya waliosafiri. Hali hii huenda ikampa ari zaidi Nyota huyo.

Misri inamtarajia kuongoza safari ndefu baada ya kutoridhisha katika AFCON iliyopita. Farao huyo ataingia akiwa na kiu ya kurejesha ufalme wake Afrika, kama mshambuliaji hatari zaidi barani. Mzigo wote upo mabegani mwake. Ubunifu, mabao, uzoefu na uongozi wa Salah ni silaha muhimu kwa Misri, akikiwasha mashindano yote yanaweza kubadilika.

Nicolas Jackson (Senegal)

Jackson
Jackson

Kwenye moja ya vikosi imara zaidi barani Afrika, Nicolas Jackson amejihakikishia nafasi muhimu kutokana na nafasi yake akiwa na Bayern Munich. Haijalishi anaanza, au anatokea benchi, amekuwa akifunga mabao muhimu tena katika mazingira magumu na yenye ushindani. Kasi yake, uimara na umaliziaji ndani ya eneo la hatari vinamfanya kuwa nyongeza kamili kwa wachezaji wazoefu wa Senegal. Akipata moto, Senegal huenda ikawa moja kwa moja miongoni mwa wagombea wakuu wa taji.

SOMA HII PIA: Top African footballers who never tasted AFCON glory

Bryan Mbeumo (Cameroon)

Mbeumo
Mbeumo

Katikati ya sintofahamu inayoikumba Cameroon kwenye uongozi wake wa soka, Bryan Mbeumo ndiye nguvu thabiti zaidi kwenye timu. Mshambuliaji huyu wa Man United ameanza na moto mkubwa ndani ya EPL. Yuko kwenye ukomavu mkubwa, akichanganya ubunifu, kubadilika nafasi uwanjani. Bila utulivu wa kiutawala kwenye kikosi chao, Cameroon inahitaji mchezaji mwenye uwezo wa kubadilisha mchezo kwa ubora binafsi na hilo ndilo Mbeumo analileta.

Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon)

AFCON 2025 Morocco
Aubameyang

Hii huenda ikawa AFCON ya mwisho kwa Pierre-Emerick Aubameyang, hivyo hakuna mchezaji anayeelewa wajibu kama yeye. Mfungaji bora wa muda wote wa Gabon na kiongozi wa zaidi ya muongo mmoja. Mkongwe huyo mwenye miaka 36 anaingia akiwa na dhamira ya kuacha alama ya mwisho barani. Gabon haijawahi kuvuka robo fainali hivyo wakihitaji kuvunja rekodi hiyo, ni lazima watamtegemea tena Aubameyang kwa ufungaji,

Hitimisho: Majina matano, lengo moja

AFCON 2025 Morocco inasubiriwa kwa hamu kubwa kutoa majibu ya maswali mengi, kuanzia nani atakuwa bingwa, mchezaji bora na tuzo nyingine binafsi. Wapo mastaa wengi wanaoweza kufanya maajabu nje yah awa wanaopewa nafasi kubwa, lakini ni wazi Hakimi anataka kung’ara nyumbani. Salah anatafuta ukombozi. Jackson analenga kuthibitisha ubora wake. Je, Mbeumo ataipa Cameroon utulivu? Aubameyang anatafuta mwonekano wa mwisho wa kifahari.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.