Barcelona 6-1 Alaves | Yamal, Raphinha wafunga mabao 4, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

LamineLamineLamine

Barcelona 6-1 Alaves | Yamal, Raphinha wafunga mabao 4, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

Barcelona 6-1 Alaves | Yamal, Raphinha wafunga mabao 4, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

  • Barcelona 6-1 Alaves ndivyo ulivyosomeka ubao wa matokeo Uwanja wa Camp Nou katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania La Liga.
  • Mastaa wawili wa Barcelona, Lamine Yamal na Raphinha kila mmoja alifunga mabao mawili, huku Lamine akiasisti bao moja na Fermin Torres akiasisti mara 2 na kufunga bao 1.
  • Ushindi huu unakuwa wa kwanza kwa Barcelona baada ya kupoteza mechi mbili mfulululizo, dhidi ya PSG na Real Madrid.
  • Makala hii inachambua kwa picha baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu za mchezo huu.

Mabingwa watetezi wa La Liga wamerudi katika njia za ushindi, hii ni baada ya matokeo ya Barcelona 6-1 Alaves katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania La Liga. Kwenye mchezo huu uliopigwa Uwanja wa Camp Nou mastaa wawili wa Barcelona, Lamine Yamal na Raphinha kila mmoja alifunga mabao mawili, huku Lamine akiasisti bao moja na Fermin Torres akiasisti mara 2 na kufunga bao 1. Ushindi huu unakuwa wa kwanza kwa Barcelona baada ya kupoteza mechi mbili mfulululizo, dhidi ya PSG na Real Madrid.

SOMA HII PIA: Barcelona FC ratiba, matokeo, kikosi, msimamo na habari

Kipindi cha kwanza Barcelona 4-0 Alaves

Lamine x Raphinha
Lamine x Raphinha

Barcelona walionyesha dhamira Dhahiri ya kushinda mchezo huo mapema tu baada ya kufunga bao la kuongoza dakika ya 8 ya mchezo kupitia kwa Raphinha. Dakika ya 23, Fermin Lopez aliifungia Barcelona bao la pili kabla ya Raphinha kufunga bao la 3 dakika ya 41. Muda mfupi kabla timu hizo hazijaenda mapumziko, Lamine Yamal aliifungia Barca bao la 4.

Shinda mpaka shilingi Milioni 800 sasa, cheza kindege ‘aviator’ ya SportPesa gusa hapa chini

image
Win big with Aviator

Kipindi cha pili Barcelona 6-1 Alaves

Matokeo Barcelona vs Alaves
Matokeo Barcelona vs Alaves

Licha ya uongozi mkubwa, Barcelona waliendelea kusaka mabao ya ziada na dakika ya 64, Lamine Yamal akaifungia Barcelona bao la 5 kabla ya, Anthony Gordon kumalizia karamu ya ushindi kwa bao la mwisho dakika ya 81. Bao pekee la wageni lilifungwa dakika ya 84 na Diaz.

Hitimisho

Ushindi huu unaifanya Barcelona kufikisha pointi 30, hivyo kusalia kileleni mwa La Liga. Alaves wao wanaporomoka mpaka nafasi ya 10 baada ya kukusanya pointi 12 pekee mpaka sasa. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.