Elie Mpanzu KibisawalaMpanzu Ellie (-)Mpanzu Ellie (-)

Elie Mpanzu Kibisawala
Elie Mpanzu winga wa Simba SC.

Elie Mpanzu Kibisawala: Nyota wa Simba SC anayetajwa kuwindwa na Yanga SC

  • Winga wa kulia Elie Mpanzu Kibisawala raia wa DR Congo anatajwa kuwindwa Yanga SC.
  • Nyota huyu amezaliwa 01/01/2002 ana umri wa miaka 24 chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Steve Barker.
  • Bao alilofunga mchezo wa Kariakoo Dabi, Oktoba 10,2026 limekuwa gumzo kila kona.

Elie Mpanzu Kibisawala ameibuka kuwa jina lisiloweza kupuuzwa katika kikosi cha Simba SC, akionyesha uwezo wa hali ya juu na kuwavutia mashabiki wengi. Mchezaji huyu amekuwa nguzo muhimu, hasa katika mechi zenye presha kubwa kama Dabi ya Kariakoo. Oktoba 10,2026 alifunga bao la ushindi Uwanja wa Uhuru matokeo yalipokuwa Simba SC 2-1 Yanga SC.

Kutokana na uwezo wake amekuwa akitajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC katika tetesi.Jambo hili kwa msimu wa 2026/27 litakuwa gumu kwa kuwa aliongeza mkataba msimu wa 2025/26.Ikiwa mabosi wa Yanga SC wanahitaji huduma yake watapaswa kuvunja mkataba na mabosi wa Simba SC.

SOMA HII PIA:Elie Mpanzu Kibisawala: Moto wa hatari NBC Premier League, Takwimu zake hizi hap ani balaa

Cheza na ushinde mpaka milioni 800 ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa kwa shilingi 1

Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu kwa shilingi 1 tu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege.Rubani huku mkwanja upo wakutosha unakusubiri.Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

image

Elie Mpanzu ni raia wa wapi?

Mwamba huyu ni raia wa DR Congo huyu ni winga wa kulia ama kushoto mwenye uwezo wa kucheza eneo la ushambuliaji.Amezaliwa Januari Mosi 2002 ana urefu wa mita 1.65. Ana umri wa miaka 24 na mguu anaupenda kuutumia sana ni ule wa kulia.Miogoni mwa timu ambazo aliwahi kucheza kabla ya kujiunga na Simba SC ni AS Vita.

Simba SC kuhusu tetesi za Mpanzu

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa bado mchezaji huyo ana mkataba katika timu hiyo. Ameongeza kuwa ikiwa kuna timu inahitaji huduma yake inapaswa kufuata utaratibu.

“Ellie Mpanzu Kibisawala ni mchezaji halali wa Simba SC.Kwa timu ambayo inahitaji huduma ya Mpanzu inapaswa kufuata utaratibu unaotakiwa.Hivyo kwenye hili hatupaswi kuwa na mashaka yoyote, tunajua wanahitaji mhezaji bora wanapaswa kusubiri kwanza anaendelea kutumikia mkataba wake,”.

Yanga SC kuhusu tetesi za Mpanzu

Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC hivi karibuni aliweka wazi kuwa hana taarifa kuhusu nyota huyo.Alibainisha kwamba wanatambua utaratibu unaotakiwa kufanyika kwenye usajili.

“Elie Mpanzu ni mchezaji wa watu na sina taarifa kuhusu huyo.Yeye ni mchezaji wa timu nyingine lakini ni mchezaji mzuri,”.

Rekodi yake katika Kariakoo Dabi

Katika mechi alizocheza ndani ya NBC Premier League 2026/27 iliyomuongezea umaaarufu zaidi ni dhidi ya watani wa jadi Yanga SC. Katika mchezo huo alikuwa kwenye ubora na alichaguliwa kuwa mchezaji bora. Alifunga bao la ushindi lililowapa pointi 3 Simba SC.

Mbali na kufunga bao hilo alichaguliwa kuwa Man of The Match kwenye mchezo huo.Kwa mitaa ya Kariakoo kila mchezaji ni fahari kwake kufunga katika Kariakoo Dabi.Nyota huyo amesema kuwa bado kuna kazi kubwa yakufanya kwa mechi zinazofuata.

“Bado kuna kazi kubwa kwenye mechi zetu ambazo tunacheza. Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji kupata matokeo mazuri.Tuna jukumu lakufanya vizuri na kupata matokeo chanya katika mechi zinazofuata,”.

SOMA HII PIA:Usichokijua kuhusu usajili wa Mpanzu: Je, ni kweli Yanga SC walimpa mkataba?

Hitimishi

Mwamba Elie Mpanzu Kibisawala ni miongoni mwa wachezaji wenye utulivu mkubwa katika uwanja.Amekuwa na sifa ya kuwa na pasi zenye uhakika akiwa ndani ya uwanja.Ni miongoni mwa wachezaji wakuchungwa kwenye mechi ambazo anacheza.

Share this: