Barcelona 1-2 Real Madrid: Kylian Mbappe afunga mabao 2, kuipa Real Madrid ushindi wa El Clasico, La Liga, Highlights
- Ubao wa matokeo wa Uwanja wa Spotify Camp Nou ulionyesha Barcelona 1-2 Real Madrid baada ya filimbi ya dakika 90 kupulizwa.
- Huu ni ushindi wa kwanza wa Real Madrid kwenye Uwanja wa Camp Nou kwenye mashindano ya La Liga, baada ya miaka 5 tangu mwaka 2021.
- Ni mabao mawili ya, Kylian Mbappe ndiyo yameihakikishia Real pointi 3 muhimu, na chachu ya vita ya ubingwa`.
- Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu kwa picha za mchezo huu.
Baada ya miaka 5, hatimaye ubao wa matokeo wa Uwanja wa Spotify Camp Nou ulionyesha, Barcelona 1-2 Real Madrid baada ya filimbi ya dakika 90 kupulizwa. Mabao mawili ya Kylian Mbappe yameipa ushindi muhimu Real Madrid,na kufufua matumaini ya mbio za ubingwa. Nini kilitokea? Makala hii inachambua matukio muhimu ya mchezo huo.
Mwanzo mgumu kwa barcelona

Barcelona ilianza mchezo kwa kusuasua, jambo lililowapa Real Madrid fursa ya kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza. Jude Bellingham aliendeleza kiwango chake bora akihusika kwenye kutawala eneo la kiungo, na kuchangia upatikanaji wa bao la pili. Mabao ya dakika za mwisho za kipindi cha kwanza, na kipindi cha 2 yaliihakikishia timu hiyo ushindi ugenini.
SOMA HII ZIADI: Barcelona vs Real Madrid Supercopa Clasico: Live score, lineups, h2h, prediction, Habari za timu
Shinda mpaka Sh. Milioni 800 za sportPesa, cheza aviator kwa kugusa kindege hapo chini
Mbappé aamua mchezo

Wakati mchezo ukielekea ukingoni na Barcelona wakionekana kurejea mchezoni, Kylian Mbappé aliibuka shujaa. Bao lake la pili na la ushindi katika mchezo huo alilifunga dakika za mwisho, na kuhakikisha Real Madrid wanapata ushindi muhimu na kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya Barcelona. Ushindi huu unaongeza presha kwa Barcelona, ambao sasa wanahitaji kujipanga upya ili kuweza kushindana vyema katika mbio za ubingwa wa LaLiga.
Athari kwa msimamo wa laliga

Matokeo haya yana maana kubwa kwa msimamo wa ligi. Real Madrid sasa imepunguza pengo la pointi dhidi ya Barcelona, ikiimarisha nafasi yao ya kutwaa taji la LaLiga msimu huu. Kwa upande wa Barcelona, wanahitaji kurekebisha makosa yao na kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika michezo ijayo, ili wasipoteze matumaini ya ubingwa.
Hitimisho
Matokeo ya Barcelona 1-2 Real Madrid ni kama sasa yamerudisha mbio za ubingwa wa La Liga miongoni mwa timu 3 za Real Madrid, Atletico Madrid na Barcelona. Mchezo huu unasalia kuwa El Classico ya kusisimua na kubaki kama kumbukumbu ya mechi bora. Endelea kufuatilia SportPesa Blog.


