
Chelsea 0-2 Tottenham Hotspur | Mike Penders kuanza vs Liverpool Oktoba 28,2026
- FT:Chelsea 0-2 Tottenham Hotspurs, mlinda mlango Mike Penders kuanza mchezo ujao vs Liverpool.
- Xabi Alonso, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kipa huyo anazidi kujengwa kuwa imara zaidi kupitia makosa.
- Cole Palmer zikiwa zimesalia dakika 10 pambano kuisha alionyeshwa kadi nyekundu.
Kocha Mkuu wa Chelsea, Xabi Alonso amesema kuwa mlinda mlango Mike Penders atakuwa langoni mchezo dhidi ya Liverpool,Oktoba 28,2026. Mike alikuwa langoni ubao uliposoma Oktoba 24,2026 Chelsea 0-2 Tottenham Hotspurs.Mlinda mlango huyo mwenye miaka 21 alijifunga dakika ya 77 na bao la pili likafungwa na Mathys Tel dakika ya 87.
Pambano hilo la English Premier League, Cole Palmer alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 80.Mike alikwama kuokoa kona ya Spurs, Uwanja wa Stamford Bridge katika harakati za kuokoa ilipelekea mpira kwenda kwenye nyavu zake na dakika 10 mbele Tel akafunga bao la pili.Kipa huyo amechukua mikoba ya Emiliano Martinez ambaye alipata maumivu kwenye mchezo vs Everton.
SOMA HII PIA:Chelsea FC: Ratiba, Matokeo, Msimamo, Kikosi na Habari Mpya
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege
Una nafasi yakushinda mamilioni ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini.
Xabi Alonso kuhusu Mike Penders
Alonso anatarajia kumpa nafasi kikosi cha kwanza Jumatano vs Liverpool, Uwanja wa Anfield. Pambano hili linavutia kwa kiwa kocha anakutana na timu yake ya zamani katika mchezo wa Carabao Cup,raundi ya 4. Kocha amethibitisha Penders ataanza vs Liverpool ugenini.
“Ni sehemu ya mchezo kwa yaliyotokea, tunahitaji kufanyia kazi makosa.Tunaongeza hali ya kujiamini kwa Mike na atakuwa langoni kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.Tunashinda na tunapoteza pamoja na ni sehemu ya kazi kushughulikia makosa. Mimi mwenyewe na kila mmoja,”.
Takwimu za mchezo Chelsea 0-2 Tottenham Hotspurs
Unakuwa ushindi wa pili kwa Spurs 2026/27.Baada ya mechi 8 ushindi ni kwenye mechi 2, sare 3 ikipoteza mechi 3 nafasi ya 14 kwenye msimamo.Chelsea mechi 8 nafasi ya 5 ushindi mechi 4, sare moja na ikipoteza mechi 3.
Chelsea ilipiga mashuti 6 huku wageni wakipiga mashuti 11. Yaliyolenga lango kwa timu zote mbili ni mashuti 4.Timu zote mbili faulo ilikuwa ni 14 na kadi za njano ilikuwa 3 kwa wababe hawa wawili.Kadi nyekundu ni mchezaji pekee wa Chelsea Cole Palmer alionyeshwa.
SOMA HII PIA:Historia ya Chelsea FC
Hitimisho
Mike Penders kijana mdogo anatarajiwa kuanza katika mchezo ujao ugenini wakiwakabili Liverpool.Pambano lijalo linatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa wawili.Kwa taarifa za hivi punde, matokeo endelea kusoma SportPesa Blog.


