
Polisi Tanzania vs Pamba Jiji:NBC Premier League |Live score | Prediction | 23/10/2026
- Mechi ijayo NBC Premier League Polisi Tanzania vs Pamba Jiji FC ni Ijumaa, Oktoba 23,2026.
- Pambano hili kali linatarajiwa kupigwa Uwanja wa Ushirika, Moshi saa 10:00 jioni.
- Polisi Tanzania ipo kwenye fomu nzuri ndani ya ligi kuu ya Tanzania ipo nafasi ya 8 kwenye msimamo inakutana na Pamba Jiji FC iliyo nafasi ya 15.
- Makala hii imekuandalia uchambuzi, utabiri wa mchezo na wachezaji muhimu.
Polisi Tanzania vs Pamba Jiji FC ni mchezo ujao katika Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) 2026/27.Pambano hili litapigwa Oktoba 23, 2026. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali huku timu zote zikihitaji pointi muhimu katika harakati zao za ligi ni Uwanja wa Ushirika, Moshi.
Uchambuzi huu unatoa mtazamo wa kina wa awali wa mechi hii, ukichunguza hali ya timu, wachezaji muhimu, na utabiri wa kitaalamu. Lengo ni kutoa picha kamili ya kile kinachoweza kutarajiwa katika pambano hili muhimu la ligi.
SOMA HII PIA:Polisi Tanzania: Ratiba, Matokeo na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27
Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa
Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.
Uwanja na muda wa kuanza
Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Oktoba 23, 2026.Uwanja wa Ushirika, saa 10:00 jioni.Wenyeji wamerejea nyumbani, mara baada ya uwanja huo kudhibitishwa na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).
Hali ya timu na habari za wachezaji
Polisi Tanzania
Polisi Tanzania wamekuwa wakionyesha mchezo wa kujituma msimu huu. Wanategemea zaidi nidhamu ya kimbinu na ulinzi imara. Hali ya wachezaji wao muhimu inahitaji kufuatiliwa kwa karibu kabla ya mchezo huu muhimu.Anuary Jabir ni mshambuliaji tegemeo katika kikosi.Keneth Kunambi alifunga bao la usawa mchezo uliopita ugenini dhidi ya Kagera Sugar wakifungana 1-1.
Pamba jiji FC
Pamba Jiji wamekuwa wakijitahidi kupata matokeo chanya katika mechi zao za hivi karibuni. Wanategemea zaidi kasi ya washambuliaji wao na ubunifu wa viungo. Morali ya timu itakuwa muhimu sana katika pambano hili.Lanso alifunga bao moja kwenye sare ya kufungana 1-1 dhidi ya Fountain Gate.Mafie na Lutonja ni miongoni mwa wachezaji muhimu.
Rekodi ya hivi karibuni na fomu
Uchambuzi wa rekodi za hivi karibuni za Polisi Tanzania na Pamba Jiji unaonyesha jinsi timu hizi zilivyofanya katika mechi zao zilizopita. Fomu ya sasa ni muhimu sana katika kutabiri matokeo ya mchezo ujao.Polisi Tanzania imecheza jumla ya mechi 8 imepata ushindi katika mechi 3, sare 2 nakupoteza mechi 3 ina pointi 11 nafasi ya 8.
Pamba Jiji FC chini ya Kocha Mkuu,Francis Baraza haijawa kwenye matokeo mazuri.Baada ya mechi 8 imepata ushindi mchezo mmojasare 2 na imepoteza mechi 5.Ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 5.
Takwimu za h2h (head-to-head)
Rekodi za kihistoria za Polisi Tanzania vs Pamba Jiji FC zinaonyesha kuwa pambano la wababe hawa ni kali.Kwenye mechi mbili zilizopita Pamba Jiji FC alipata ushindi.Kwa fomu ya msimu wa 2026/27 inaongeza ugumu kwa timu zote mbili.
24/11/2023, Polisi Tanzania 0-1 Pamba Jiji FC
30/03/2024, Pamba Jiji FC 5-1 Polisi Tanzania
Polisi Tanzania vs Pamba Jiji FC prediction
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na matokeo ya timu zote mbili kwenye ligi.Kurejea nyumbani Polisi Tanzania,Uwanja wa Ushirika kunaongeza nguvu ya ushindi.Matokeo ni Polisi Tanzania 2-1 Pamba Jiji FC.Haya ni maoni ya mhariri, matokeo rasmi yatajulikana mara baada ya mchezo.
SOMA HII PIA:Polisi Tanzania 2-0 Mbeya City NBC Premier League | Msimamo | Highlights | SportPesa Blog
Hitimisho
Wanakutana wababe wawili Polisi Tanzania vs Pamba Jiji FC katika pambano la ligi.Uwanja wa Ushirika, Moshi pambano hili kali litapigwa.Timu zote mbili zimetoka kugawana pointi mojamoja mechi zao zilizopita hivyo zitaingia uwanjani kwa hesabu kali.


