Yanga SC vs CFFA FCNondo na SelemanNondo na Seleman

Yanga SC vs CFFA FC
Aboutwalib mlinda mlango wa Yanga SC

Yanga SC vs CFFA FC CAF Champions League | H2H | Prediction | SportPesa Blog

  • Watoto wa Jangwani Yanga SC watakabiliana na vijana kutoka Madagascar CFFA FC kwenye mchezo utakaotoa mshindi wa jumla CAF Champions League Oktoba 21,2026.
  • Mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,Oktoba 17 ilikuwa CFFA FC 0-4 Yanga SC, Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
  • Jumatano itakuwa moto saa 1:00 usiku kwa wababe hawa kusaka ushindi Uwanja wa Azam Complex, Dar.
  • Aboutwalib Mshery mlinda mlango wa Yanga SC ameanza na rekodi yake CAF

Ni Yanga SC vs CFFA FC CAF Champions League ni ratiba ya mchezo unaofuata katika kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi.Matokeo ya mchezo uliopita 17/10/2026 ilikuwa CFFA FC 0-4 Yanga SC, Uwanja wa Azam Complex. Wakiwa ugenini walitangaliza mguu mmoja hatua ya makundi.Mchezo wa marudio wanahitaji sare ama ushindi wa aina yoyote wasonge mbele.

SOMA HII PIA:CFFA 0-4 Yanga SC | CAF Champions League, Highlights, magoli, Livescore, habari za timu

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha kindege

Una nafasi yakushinda mamilioni ukipaisha kindege sasa hivi na SportPesa. Marubani wapo hewani wanavuna mkwanja. Zamu yako ni sasa bofya hapa chini.

image
 

Yanga SC vs CFFA FC CAF taarifa muhimu

Kipengele Maelezo
Mashindano CAF Champions League
Matokeo Yanga SC vs CFFA FC
Uwanja Azam Complex
Tarehe 21/10/2026
Timu mwenyeji Yanga SC

H2H Yanga SC vs CFFA FC

Wababe hawa wamekutana mara moja katika mchezo wa CAF.Yanga SC ilipata ushindi wa mabao 4-0 ikiwa ugenini.Mchezo wa pili utaamua mshindi wa jumla atakayesonga mbele mpaka hatua ya makundi.

17/10/2026, CFFA FC 0-4 Yanga SC

21/10/2026, Yanga SC vs CFFA FC

Aboutwalib Mshery na rekodi CAF

Mlinda mlango wa Yanga SC, Aboutwalib Mshery ameanza na rekodi katika mashindano ya CAF.Mchezo wake wa kwanza ameanza na clean sheet.Kipa huyo mzawa alianza langoni mara baada ya kipa namba moja Djigui Diarra kupata maumivu mazoezini.

Yanga SC vs CFFA FC prediction

Kasi waliyonayo Yanga SC inawapa faida kupata ushindi kwenye mchezo wa pili.Faida ya uwepo wa mashabiki Uwanja wa Azam Complex wakiwa nyumbani inaongeza morali.Matokeo ni Yanga SC 3-0 CFFA FC, haya ni maoni ya mhariri, matokeo rasmi baada ya mchezo.

SOMA HII PIA:Safari ya Yanga SC na Simba SC CAF Champions League 2026/27: Ratiba, Timu na Matarajio ya Klabu za Tanzania

Hitimisho

Yanga SC vs CFFA FC CAF ni mchezo wa maamuzi kwa wababe hawa wawili kusaka tiketi ya kusonga mbele kimataifa.Wageni kutoka Madagascar wana mlima mkubwa kupanda kurejesha mabao 4 na kusaka bao la ushindi.Wenyeji Yanga SC wataingia kwa umakini kulinda ushindi na kutafuta tiketi kutinga hatua ya makundi.

Share this: