
Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC :NBC Premier League | H2H | Prediction
- Wanakutana Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC kwenye pambano kali la NBC Premier League, Oktoba 16,2026.
- H2H katika mechi 4 za NBC, Pamba Jiji FC imepata ushindi mara 3 na sare ikiwa ni mara moja kwa timu zote mbili.
- Kwenye msimamo Fountain Gate ipo nafasi ya 16 na Pamba Jiji FC nafasi ya 15 zote zina pointi 4.
- SportPesa Blog tumekuletea takwimu za mchezo,msimamo na utabiri
Ni Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC wanajiandaa kukutana katika pambano la kusisimua la Ligi Kuu NBC Oktoba 16,2026. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali huku timu zote zikihitaji pointi muhimu kuboresha nafasi zao kwenye msimamo wa ligi.Mechi hii itapigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid , Arusha.Kick-off inatarajiwa kuwa saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Mashabiki wanatarajia kuona kandanda safi na mikakati ya hali ya juu kutoka kwa makocha wa timu zote mbili. Hapa tumekuletea uchambuzi wa kina wa mchezo huu.
SOMA HII PIA:Fountain Gate FC: Ngome Inayochipukia ya Soka Tanzania – Ratiba, Wachezaji na Maelezo Muhimu ya Klabu
Vuna mamilioni ukibashiri na SportPesa
Nafasi niyako sasa hivi ukisuka mkeka kupitia SportPesa.Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC ni hela inakusubiri baada ya dakika 90.Kuna nafasi yakushinda hata kabla ya dakika 90 kwa kufanya chaguo sasa.Beti kwa uwajibikaji, bofya link hapa chini:-

Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC taarifa muhimu
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Mchezo | Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC |
| Uwanja | Sheikh Amri Abeid |
| Tarehe | 16/10/2026 |
| Timu mwenyeji | Fountain Gate FC |
Habari za timu na majeruhi
Kwa upande wa Fountain Gate FC, hakuna majeruhi au wachezaji watakaokosekana. Hii inamaanisha Kocha Mkuu, Felix Minziro anaweza kuwa na kikosi kamili cha kuchagua.Kuna urejeo wa kiungo wa Daniel Joram ambaye alikuwa nje kwa muda mrefu.
Pamba Jiji FC chini ya Kocha Mkuu,Francis Baraza wapo tayari kwa mchezo wachezaji wakiwa kamili. Kocha huyo amebainisha wanatambua umuhimu wa mchezo wakiwa ugenini watapambana kupata matokeo mazuri.Timu zote zimecheza mechi 7 msimu wa 2026/27.
Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC H2H
Historia ya Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC inaonyesha ushindani mkali. Katika mechi za hivi karibuni, Pamba Jiji FC wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Fountain Gate FC.Kwenye mechi 4, ushindi ilikuwa ni mechi 3 kwa Pamba Jiji FC na sare moja.
30/04/2026 Fountain Gate FC 1-2 Pamba Jiji FC
23/11/2025 Pamba Jiji FC 1-0 Fountain Gate FC
08/04/2025 Pamba Jiji FC 1-1 Fountain Gate FC
05/11/2024 Fountain Gate FC 1-3 Pamba Jiji FC
Wachezaji muhimu na mbinu
Fountain Gate FC watahitaji kutegemea wachezaji wao wa kati kuweza kudhibiti mchezo na kuunda nafasi za kufunga.Uwepo wa Derick Mukombozi,Obasi Macdonald na Awara Jr unaongeza nguvu katika kikosi cha wenyeji. Ulinzi wao pia utahitaji kuwa imara kukabiliana na mashambulizi ya Pamba Jiji FC.
Kwa upande wa Pamba Jiji FC, kasi ya washambuliaji wao na uwezo wa kutumia nafasi watakuwa muhimu. Mbinu ya kocha Baraza itazingatia jinsi ya kuvunja ngome ya Fountain Gate na kupata mabao.Zabona Mayombwa mchezaji bora mchezo uliopita dhidi ya Fountain Gate FC bado yupo imara anaaminiwa na benchi la ufundi.
Utabiri na mtazamo wa wahariri
Pamba Jiji FC haijawa imara kwenye ulinzi katika mechi zilizopita.Baada ya mechi 7 imeruhusu mabao 13 inakutana na Fountain Gate iliyoruhusu mabao 11.Katika upande wa ufungaji imefunga mabao 8 huku wenyeji wakiwa wamefunga mabao 3 baada ya mechi 7.
Licha ya Fountain Gate FC kuwa nyumbani, haijawa ni faida kwake. Mchezo uliopita ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya JKT Tanzania na ilianza kufunga.Matokeo ya mchezo wa leo itakuwa ni sare kwa wababe hawa wawili. Fountain Gate FC 1-1 Pamba Jiji FC.Haya ni maoni ya mhariri na sio matokeo rasmi.
SOMA HII PIA:Matokeo NBC Premier League | Fountain Gate 0-2 Yanga SC | Man of The Match | SportPesa Blog
Hitimisho
Wababe wawili Fountain Gate FC vs Pamba Jiji FC wanakutana kwenye pambano zito.Wote wapo kwenye mstari wakushuka daraja.Kila timu inapambania kujinasua katika eneo hilo la hatari jambo linaloongeza ushindani katika mchezo wa leo.

