Salzburg 0-4 AC Milan | Europa League, Highlights, magoli, Cisse apiga hattrick Livescore, habari za timu

ByJoel Thomas

October 16, 2026
AC MilanAC MilanAC Milan

Salzburg 0-4 AC Milan | Europa League, Highlights, magoli, Cisse apiga hattrick Livescore, habari za timu

  • Ubao wa matokeo wa Red Bull Arena umemalizika kwa kuonyesha matokeo ya Salzburg 0-4 AC Milan leo Alhamisi Oktoba 15, 2026.
  • Hii ni katika mchezo wa mashindano ya ligi ya Europa.
  • Nyota wa AC Milan, Alphadjo Cisse ndiye aliyeongoza maumivu baada ya kufanikiwa kufunga mabao 3, yaani Hattrick.
  • Makala hii inachambua baadhi ya matukio ‘highlights’ muhimu za mchezo huu.

Mashindano ya Ligi ya Europa yameendelea ambapo miongoni mwa matokeo ya  ushindi mkubwa yakiwa ya mchezo wa Salzburg 0-4 AC Milan. Ni nyota wa AC Milan, Alphadjo Cisse ndiye aliyeongoza maumivu kwa wenjeji baada ya kufanikiwa kufunga mabao 3, yaani Hattrick. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Red Bull huko Salzburg, nchini Austria. Makala hii inavhambua highlights za mchezo huo.

SOMA HII PIA: Juventus vs AC Milan: Live Score, H2H, Vikosi, Msimamo na Takwimu

Salzburg 0-4 AC Milan, mchezo ulikuwaje?

Salzburg 0-4 AC Milan
Salzburg — AC Milan

Milan ilianza mchezo kwa kasi, ikitafuta bao la mapema kupitia mashambulizi yaliyokuwa yakiongozwa na Omari Hutchinson na Alphadjo Cisse. Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 15, Cisse alipofunga kwa kichwa akimalizia krosi ya Hutchinson na kuupachika mpira kwenye kona ya chini ya lango la Salzburg. Baada ya bao hilo, Milan iliendelea kutawala mchezo huku Ruben Loftus-Cheek na Hutchinson wakipata nafasi za kuongeza uongozi, lakini kipa wa Salzburg, Christian Zawieschitzky, pamoja na Kevin Boma, waliokoa hatari kadhaa zilizokuwa zikielekea langoni mwao. Hata hivyo, Salzburg ilishindwa kuhimili mashambulizi ya Milan na kuruhusu bao la pili muda mfupi baada ya dakika ya 30.

Davide Bartesaghi alipokea pasi nzuri ya juu kutoka kwa Adrien Rabiot kabla ya kupiga krosi ya kwanza iliyomaliziwa na Cisse, aliyeendelea kuonyesha makali yake katika eneo la hatari. Kipindi cha pili kilianza kwa Milan kuendeleza ubabe wake, na dakika ya 49 Cisse alikamilisha hat-trick yake baada ya kuunganisha mpira uliowasilishwa na Rabiot katika eneo la lango. Bao hilo lilithibitishwa baada ya ukaguzi wa VAR, na kuifanya Milan kuongeza uongozi wake hadi mabao 3-0.

Milan iliendelea kuwa tishio, huku Hutchinson akikosa nafasi ya kuongeza bao jingine baada ya shuti lake kuzuiwa na Zawieschitzky. Bao la nne la Milan lilifungwa na Goncalo Ramos dakika ya 72 baada ya Ardon Jashari kunufaika na kosa la umiliki wa mpira la Bartosz Mazurek. Mpira ulimfikia Ramos, ambaye alimalizia kwa utulivu na kuhitimisha matumaini ya Salzburg ya kuokoa matokeo. Milan ililazimika kumaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya Filippo Terracciano kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za mwisho kwa kumchezea vibaya Dominik Schmid akiwa mchezaji wa mwisho wa ulinzi.

SOMA HII ZAIDI: Italy Serie A Table 2025/26

Cisse aweka rekodi mpya Ulaya

Salzburg 0-4 AC Milan
Cisse

Mbali na ushindi huo, Cisse aliandika historia akiwa na umri wa miaka 19 na siku 358. Hii inamfanya kuwa mchezaji mdogo zaidi wa Italia kufunga mabao matatu au zaidi katika mchezo mmoja wa mashindano makubwa ya vilabu barani Ulaya. Pia, mabao yake mawili ya kipindi cha kwanza yalimfanya kuwa mchezaji mdogo zaidi katika historia ya AC Milan kufunga mabao zaidi ya moja ndani ya kipindi kimoja katika mashindano makubwa ya Ulaya.

SOMA HII PIA: Ligi ya Europa 2026/27: Matokeo ya Raundi ya Tatu na Droo ya Play-off

Hitimisho

Mechi
Mechi

Matokeo ya Salzburg 0-4 AC Milan yanaipa Milan morali kuelekea mchezo wake wa Serie A dhidi ya Atalanta mwishoni mwa wiki, kabla ya kukutana na Bournemouth katika mchezo wake unaofuata wa Europa League. Kwa upande wa Salzburg, kipigo hicho kinaendeleza mwenendo wake mbaya dhidi ya Milan. Katika michezo mitano ya mwisho ya mashindano makubwa ya Ulaya dhidi ya vigogo hao wa Italia, Salzburg haijapata ushindi, ikiwa na sare moja na vipigo vinne, endelewa kufuatilia SPortPesa Blog.

 

Share this:

ByJoel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.