
NBC Premier League: Geita Gold vs Dodoma Jiji FC | H2H | Prediction | Livescore
- Geita Gold vs Dodoma Jiji FC pambano lakukata na shoka NBC Premier League 2026/27
- Obrey Chirwa anatarajiwa kuiongoza safu ya ushambuliaji ya Geita Gold dhidi ya Dodoma Jiji FC yenye beki kisiki Abdi Banda.
- H2H katika mechi 4 zilizopita, wenyeji walipata ushindi mechi 2 na Dodoma Jiji FC ilishinda mchezo mmoja, sare 1
- SportPesa Blog tumekuletea uchambuzi wa mchezo huu utakaopigwa saa 1:00 usiku.
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unatarajiwa kuwa mkali kati ya Geita Gold vs Dodoma Jiji FC Oktoba 16,2026. Timu hizi zitakutana katika pambano muhimu la kusaka pointi tatu, huku kila upande ukiwa na malengo yake ya msimu.Saa 1:00 usiku pambano hili kali linatarajiwa kupigwa Uwanja wa Bukombe,Geita.
Hapa tumekuletea uchambuzi wa kina wa kabla ya mechi, tukichunguza fomu za timu, takwimu za hapo awali, na wachezaji muhimu wanaotarajiwa kuleta mabadiliko uwanjani. Geita Gold kwenye msimamo ni nafasi ya 12 ikiwa na pointi 7 inawakaribisha Dodoma Jiji FC wenye pointi 11 nafasi ya 6.
SOMA HII PIA:Geita Gold FC: Matokeo ya Ligi Kuu Bara 2026/27, Ratiba na Msimamo
Bashiri na SportPesa ushinde mamilioni
Suka mkeka wako kwa umakini uvune mamilioni kupitia SportPesa.Geita Gold vs Dodoma Jiji FC unapigwa leo kuna chaguzi nyingi na unaweza kuvuna mkwanja wakati mchezo unaendelea.Bashiri kwa uwajibikaji,bofya link hapa chini:-

Geita Gold vs Dodoma Jiji FC taarifa muhimu
| Kipengele | Maelezo |
| Mashindano | NBC Premier League |
| Mchezo | Geita Gold vs Dodoma Jiji FC |
| Uwanja | Bukombe |
| Tarehe | 16/10/2026 |
| Timu mwenyeji | Geita Gold |
Habari za timu na majeraha
Kwa upande wa Geita Gold, hakuna ripoti za majeraha makubwa zilizothibitishwa hadi sasa. Kocha Mkuu, Zuber Katwila amebainisha kuwa wapo kamili kwa mchezo.Hii inamaanisha kocha yupo na kikosi kamili cha kuchagua, jambo ambalo linaweza kuwapa faida ya kimbinu.
Dodoma Jiji FC kupitia kocha Vincent Masham amebainisha maandalizi yapo kamili.Kuhusu majeraha ameweka wazi kuwa wachezaji wote wapo fiti.Ameongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao.
H2H Geita Gold vs Dodoma Jiji FC
Katika mechi 4 walizokutana wababe hawa, Geita Gold ilipata ushindi mechi 2, Dodoma Jiji FC mara 1.Wababe hawa walitoshana nguvu mara moja.Mchezo wa leo unaongeza ushindani kwa wababe wawili katika dakika 90.
09/03/2024 Dodoma Jiji FC 0-1 Geita Gold
21/10/2024 Geita Gold 2-2 Dodoma Jiji FC
14/01/2023 Geita Gold 2-0 Dodoma Jiji FC
29/09/2022 Dodoma Jiji FC 1-0 Geita Gold
Wachezaji muhimu na mbinu
Kwa Geita Gold, macho yataelekezwa kwa washambuliaji wao akiwemo Obrey Chirwa wamekuwa wakifanya vizuri katika mechi zilizopita.Uwepo wa Martin Kigi unaongeza nguvu kwenye kikosi.Uwezo wao wa kufunga mabao utakuwa muhimu katika kuvunja ngome ya Dodoma Jiji. Viungo wao pia wanatarajiwa kudhibiti eneo la kati na kutoa pasi za hatari.
Dodoma Jiji watategemea zaidi ulinzi wao imara na mashambulizi ya kushtukiza.Mlinda mlango Ally Salim anawaongezea nguvu kutokana na uzoefu alionao. Wana wachezaji wenye kasi akiwemo Abdi Banda wanaweza kuleta madhara makubwa kwa mabeki wa Geita Gold. Kiungo wao mchezeshaji atakuwa na jukumu muhimu la kuunganisha safu ya ulinzi na ushambuliaji.
Utabiri na mtazamo wa wahariri
Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na umuhimu wake kwa timu zote mbili. Geita Gold watakuwa na faida ya kucheza nyumbani, huku Dodoma Jiji wakiwa na morali nzuri kutokana na fomu yao ya sasa.
Kutokana na uchambuzi wa fomu na uwezo wa timu, tunaona mchezo huu unaweza kuwa na matokeo ya sare au ushindi mwembamba kwa upande mmoja. Utabiri wetu ni kwamba mchezo utakuwa na mabao machache na ushindani mkali katikati ya uwanja.
SOMA HII PIA:Matokeo ya NBC Premier League mzunguko wa 6 | Yanga SC 1-0 Geita Gold | Azam FC 0-2 Simba SC | SportPesa Blog
Hitimisho
Mchezo wa Geita Gold vs Dodoma Jiji FC ni pambano la kukata na shoka.Kupoteza kwa kufungwa mabao 4-0 dhidi ya Pamba Jiji FC kunawaongezea hasira wenyeji.Dodoma Jiji FC imetoka kupata sare yakufungana bao 1-1 Singida Black Stars hivyo itaingia kwa hesabu za kusaka pointi ugenini.

