
- Kivumbi Simba SC vs Yanga SC ni leo 10/10/2026 saa 1:00 mtanange wakukata na shoka utapigwa
- Pilato Ahmed Arajiga ametangazwa kuwa mwamuzi wa mchezo huu mkali utakaopigwa saa 1:00 usiku.
- Simba SC waliweka kambi Afrika Kusini na Yanga SC kambi ilikuwa Avic Town, Kigamboni, Dar
Uwanja wa Uhuru Simba SC vs Yanga SC ni leo 10/10/2026, inakaribia kutikisa anga la soka la Tanzania. Mashabiki wa pande zote mbili wanajiandaa kushuhudia burudani ya hali ya juu katika mchezo huu muhimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Ilikuwa ni siku 10 zinahesabiwa hatimaye ni saa zimesalia.
Ni Ahmed Arajiga atakuwa pilato wa mchezo huu mkubwa wa mzunguko wa kwanza. Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo na Yanga SC nafasi ya kwanza wote wana pointi 18 baada ya mechi 6. Tofauti ni kwenye mabao yakufunga na kufungwa.
SOMA HII PIA:Simba SC vs Yanga SC: Wakali wa mipira ya kutenga kuelekea Kariakoo Dabi Oktoba 10, 2026 | Uwanja wa Uhuru
Shinda mamilioni na SportPesa
Una nafasi kubwa kushinda mamilioni ukibashiri mchezo wa Simba SC vs Yanga SC kupitia SportPesa. Rahisi mno, suka mkeka wako na ubashiri kwa uwajibikaji. Bofya link hapa uchague option uipendayo ukombe mihela.

Simba SC vs Yanga SC ni leo kinabondwa
Mwisho wa ubishi unakaribia, Simba SC vs Yanga SC ni leo kinabondwa kwa wababe wawili kusaka pointi 3 muhimu.Timu zote mbili zimekuwa zikifanya maandalizi makali kuelekea dabi hii. Makocha wamekuwa wakifanya kazi usiku na mchana kuhakikisha wachezaji wao wako fiti kimwili na kiakili. Simba SC waliweka kambi Afrika Kusini na Yanga SC kambi ilikuwa Avic Town Kigamboni, Dar.
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema walipata muda wakutosha kufanya maandalizi. Kuhusu kambi ya Afrika Kusini alibainisha kuwa ilikuwa yenye mafanikio makubwa. Kuhusu eneo alilofanyia maboresho ni ushambuliaji na ulinzi kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Yanga SC.
“Tumefanyia kazi eneo la ushambuliaji na ulinzi kuelekea mchezo wetu dhidi ya Yanga SC, tunatambua mchezo utakuwa mgumu tupo tayari. Huu ni mchezo mkubwa na mgumu tumejiandaa kuwakabili wapinzani wetu,”.
Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema wanatambua mchezo wa leo ni mgumu. Kocha huyo amebainisha kuwa wataingia kwa umakini na hesabu ni kumiliki mchezo ili washinde. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.
“Dabi ya Kariakoo ni kubwa na tunalitambua hivyo, tutaingia uwanjani kwa umakini na malengo ni kumiliki mchezo ili kupata ushindi, mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuwaongezea nguvu wachezaji wetu,” .
Simba SC vs Yanga SC nani kuvunja unbeaten?
Rekodi zinaonyesha kuwa 2026/27 wababe hawa wawili bado hawajapoteza mchezo. Mara baada ya mechi 6 hakuna timu iliyopoteza. Swali ni nani atavunja unbeaten ya mpinzani ndani ya dakika 90?
Mshindi wa leo atakuwa mbabe mbele ya mpinzani wake. Simba SC vs Yanga SC haijawahi kuwa mechi rahisi. Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo mkali wenye kusisimua.
SOMA HII PIA: [Kiungo cha ndani kuhusu historia ya Kariakoo Dabi au takwimu za zamani za timu hizi]
Utabiri na matarajio
Kutabiri matokeo ya Kariakoo Dabi ni jambo gumu kutokana na upinzani mkali na ari ya timu zote mbili. Hata hivyo, wachambuzi wa soka wanatarajia mchezo wa wazi na wenye ushindani mkubwa. Timu itakayotumia vizuri nafasi zake na kuwa na nidhamu ya hali ya juu ndiyo itakayopata matokeo chanya.
Kwa rekodi za mechi zilizopita ndani ya NBC Premier League inaonyesha Yanga SC ni imara kwenye kufunga. Mabao 16 kwenye mechi 6. Simba SC imefunga mabao 11 katika mechi 6. Katika eneo ambalo wote wamekuwa sawa ni eneo la ulinzi kila timu imefungwa mabao 2 na pointi zao ni 18 wakitofuatiana katika idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Utabiri wa mhariri ni matokeo ya sare kwa wababe hawa wawili. Simba SC 1-1 Yanga SC. Haya ni maoni ya mhariri na sio matokeo kamili. Cheza na ushinde na SportPesa!
SOMA HII PIA:Maswali ya Kiufundi Kuelekea Kariakoo Dabi: Simba SC vs Yanga SC
Hitimisho
Jambo la Simba SC vs Yanga SC ni leo 10/10/2026 Uwanja wa Uhuru, Dar. Saa 1:00 wababe hawa watakuwa kazini kusaka pointi 3 muhimu. Endelea kufuatilia SportPesa Blog kwa sasisho zaidi na uchambuzi wa kina wa Kariakoo Dabi. Usikose burudani hii ya soka la Tanzania!

