Madagascar vs Taifa StarsSimo Msuva StarsSimo Msuva Stars

Madagascar vs Taifa Stars
Miguel Gamond, Kocha Mkuu wa Stars

Madagascar vs Taifa Stars ni ratiba inayofuata mchezo muhimu wa kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027. Hii ni kampeni ya PAMOJA 2027. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali, huku timu zote zikihitaji pointi tatu muhimu. Timu zote mbili hazijakusanya pointi kwenye Kundi L. Matokeo yaliyopita ilikuwa Taifa Stars 0-2 Guinea Bissau na Nigeria 2-1 Madagascar.

SOMA HII PIA: Taifa Stars 0-2 Guinea-Bissau AFCON 2027 | H2H | Highlights | SportPesa Blog

Bado hujashinda pesa? Cheza ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa

Ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

image

Hali ya vikosi na majeraha

Kwa upande wa Taifa Stars, Kocha Mkuu, Miguel Gamondi amebainisha kwamba wachezaji wote wapo fiti. Mbwana Samatta atakosekana kwenye kikosi kwa kuwa aliomba kustaafu hayupo kwenye orodha ya wachezaji waliopo kambini.Simo Msuva nahodha wa Stars amebainisha kuwa wachezaji wapo kamili kwa mchezo mgumu wakiwa ugenini.

H2H Madagascar vs Taifa Stars

Rekodi zinaonyesha kuwa katika mashindano rasmi timu hizi zimekutana mara 10. Ushindi ni mara 4 kwa Stars na Madagascar ni mara 3 na sare ni 3. Safu ya ushambuliaji ya Madagascar inaonekana kuwa kali ikifunga mabao 17 na ile ya Tanzania ikifunga mabao 15 kwenye mechi ambazo walikutana.

1965, Taifa Stars ilikubali kipigo cha mabao 5-1 mchezo wa pili walipokutana ilishinda mabao 2-1. Kwenye mashindano kufuzu Olmpiki Tanzania iliangukia pua kwa kufungwa nje ndani. 1967, Tanzania ilichapwa 4-2 mchezo wa kwanza na ule wa pili ilichapwa 2-0 hivyo mchezo unatarajiwa kuwa ni mkali.

Wachezaji muhimu na mbinu za kiuchezaji

Kwa Taifa Stars, Simon Msuva licha yakushindwa kufunga kwenye mchezo uliopita dhidi ya Guinea-Bissau ni nyota mwenye uwezo mkubwa. Ibrahim Bacca kwenye upande wa ulinzi na Bakari Nondo. Fei Toto eneo la kiungo amekua imara hasa kutokana na sifa yake yakupiga mashuti ya mbali.

Madagascar ina wachezaji wenye uwezo mkubwa kutengeneza hatari na kushambulia. Nyota Ehsan Kari ni mfugaji wa bao pekee mchezo uliopita dhidi ya Nigeria.

SOMA HII PIA:Taifa Stars vs Guinea-Bissau AFCON 2027 |H2H | Prediction | SportPesa Blog

Utabiri na mtazamo wa wahariri

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu na wenye ushindani mkali. Ingawa Taifa Stars ina uzoefu, kucheza ugenini dhidi ya Madagascar yenye hamasa kunaweza kuwa changamoto. Tunatarajia mchezo wa kufungana na matokeo ya sare yanawezekana, au ushindi mwembamba kwa upande mmoja.

Ushindi kwa Taifa Stars utakuwa muhimu sana katika kuimarisha nafasi zao za kufuzu AFCON 2027. Hata hivyo, sare pia inaweza kuwa matokeo mazuri ugenini.

Hitimisho

Madagascar vs Taifa Stars ni mchezo muhimu kuwanifa kufuzu AFCON 2027. Tanzania imefuzu tayari kwa kuwa ni mwenyeji. Itashirikiana na Kenya na Uganda kuaandaa mashindano haya makubwa.

Share this: