Simba SC yaweka kambi Afrika Kusini kujiandaa kuikabili Yanga SC | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

September 24, 2026
Simba SCKibabageKibabage
  • Simba SC vs Yanga SC ni mchezo unaofuata kwenye ratiba kwa wababe hawa wawili kukutana Oktoba 10, 2026
  • Msafara wa Simba SC umeelekea Afrika Kusini kujiandaa kuikabili Yanga SC
  • Rais wa Simba SC na mwekezaji, Mohammed Dewji amesimamia kila kitu kuhakikisha kambi inafanikiwa asilimia 100 ya gharama

Kikosi cha Simba SC Septemba 24, 2026 kimekwea pipa kuelekea Afrika Kusini kwa kambi maalumu. Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Steve Barker inatarajiwa kuvaana na Yanga SC, Oktoba 10, 2026. Miongoni mwa wachezaji waliojumuishwa kwenye kikosi ni Nickson Kibabage, Hussen Abel, Hamza Jr, Duchu na kocha msaidizi Seleman Matola.

Soma hii pia: Simba SC Fixtures: Full Schedule, Dates and Kickoff Times

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindenge

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

image

Taarifa muhimu kuhusu kambi ya Simba SC Afrika Kusini

Simba SC
Seleman Matola kocha msaidizi wa Simba SC.
KipengeleMaelezo
Timu Simba SC
KambiAfrika Kusini
Muda wa kambiSiku 10
Tarehe ya kuondoka TanzaniaSeptemba 24, 2026
Kocha MkuuSteve Barker
Mchezo unaofuataSimba SC vs Yanga SC
TareheOktoba 10, 2026

Sababu ya kambi Afrika Kusini

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema sababu kubwa ya kambi hiyo ni maandalizi kwa mechi za kitaifa na kimataifa.Ahmed amebainisha uamuzi huo umeungwa mkono na Rais wa Simba SC na mwekezaji, Mohammed Dewji ambaye amejitoa kugharamia kambi ya siku 10.

“Baada ya kumaliza mechi zetu raundi ya 6 timu ilipata mapumziko ya siku 7. Mara baada ya mapumziko hayo Septemba 23 wachezaji walirudi kambini na Septemba 24 safari kuelekea Afrika Kusini. Hapo tunakwenda kwa ajili ya kambi maalumu ya siku 10.

“Tunamshukuru Rais wa Simba SC na mwekezaji, Mohammed Dewji ambaye amejitoa kugharamia kila kitu kwa siku 10. Tunakwenda kwenye utulivu mkubwa kwa maandalizi ya mechi zinazofuata.Tuna kila sababu kuwatangazia Wanasimba kuwa kilichofanyika ni jambo jema ni jukumu lake kuihudumia timu.

“Kuongeza thamani ya kambi na kuongeza deni kwa wachezaji waone kuwa wana deni kubwa Oktoba akaingia mfukoni na kutoa pesa. Kambi hii asilimia 100 imegharamiwa na Mo. Tunakwenda kwenye sehemu ya gharama kuweka kambi kwa sasa.

Wachezaji waliopo kwenye msafara

Kwenye msafara wa kikosi kilichoelekea Afrika Kusini, mlinda mlango Hussen Abel amejumuishwa.Hamza Jr beki, Kibabage, Mgunda ambaye ni mshambuliaji, Duchu ambao hawajaitwa kwenye timu za taifa.

Rushine ambaye ni beki, Neo Maema raia wa Afrika Kusini hawa walitangulia mapema hivyo wataungana na timu kambini. Kocha Mkuu, Steve Barker naye yupo Afrika Kusini ambapo ni nyumbani.

Soma hii pia: Simba SC: Matokeo, Ratiba na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27

Hitimisho

Kikosi cha Simba SC kimeweka kambi Afrika Kusini kwa maandalizi ya mwisho kwa mechi za Oktoba. Mchezo mkubwa unaosubiriwa kwa shauku ni Kariakoo Dabi, Simba SC vs Yanga SC unatarajiwa kupigwa Oktoba 10, 2026. Baada ya siku 10 kikosi kitarejea Dar kuendelea na mechi za Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.

Share this: