Matokeo ya NBC Premier League mzunguko wa 6 | Yanga SC 1-0 Geita Gold | Azam FC 0-2 Simba SC | SportPesa Blog

ByLunyamadizo Mlyuka

September 22, 2026
Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa 6Juma KasejaJuma Kaseja
  • Yajue Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa 6 ushindani umezidi kuwa mkali ndani ya uwanja
  • Maxi Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ni Man of The Match dhidi ya Geita Gold
  • Ushindani mkubwa umeleta matokeo tofauti ikiwemo Mashujaa FC 2-1 Singida Black Stars, Dodoma Jiji FC 1-0 Namungo FC.
  • SportPesa Blog tumekuletea matokeo na wafungaji wa mabao katika mechi

Ligi Kuu Tanzania Bara inazidi kuchanja mbunga huku kila timu ikipambana kusaka pointi 3 muhimu uwanjani. Azam FC 0-2 Simba SC ni matokeo ya mchezo wa Mzizima Dabi uliofuatiliwa kwa ukaribu. Kagera Sugar 1-1 Fountain Gate ni mchezo wa mwisho kwa Juma Kaseja kukaa kwenye benchi la ufundi akiwa na matajiri wa Bukoba.

SOMA HII PIA: Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara 2026/27

Vuna mamilioni sasa hivi ukipaisha kindenge

Kuna jambo umekwama kwa sasa kuhusu mkwanja? Usiogope, rubani ni jasiri na kazi yake ni kupaisha kindege cha SportPesa. Cheza sasa hivi Aviator uvune mamilioni bofya hapa chini, muda ni wako na nafasi ya ushindi inakusubiri.

image
Paisha kindege uvune mamilioni sasa hivi

Haya hapa matokeo ya NBC Premier League mzunguko wa 6

Matokeo ya Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa 6
Paul Peter nyota wa JKT Tanzania vs Mudathir wa Yanga SC.
TareheMatokeoWafungajiUwanja
Septemba 9, 2026Mashujaa FC 2-1 Singida Black StarsSamson Madeleke dakika ya 54 na Haroun Lyawatwa dakika ya 90+2 Singida Black Stars mtupiaji Ahmed Pipino, dakika ha 50Lake Tanganyika, Kigoma
Septemba 11, 2026Dodoma Jij FC 1-0 Namungo FCYassi Mgaza dakika ya 34Jamhuri, Dodoma
Septemba 12, 2026Polisi Tanzania 2-0 Mbeya CityAnuary Jabir dakika ya 38 na 45+1 kwa mkwaju wa penaltiUwanja wa Sheikh Amri Abeid
Septemba 12, 2026Coastal Union 2-1 JKT TanzaniaMaabad Maabad dakika ya 10 mkwaju wa penalti na Shiza Ramadhani dakika ya 78 bao la JKT Tanzania mfungaji Hassan Otalo dakika ya 45+3Uwanja wa Mkwakwani
Septemba 13, 2026Pamba Jiji FC 1-3 TRA UnitedBao la Pamba Jiji FC limefungwa na Abdulkarim Iddy dakika ya 76 na TRA United yamefungwa na Anni Elihah dakika ya 5, Nonyemi Okorocha OG dakika ya 8 na Emmanuel Mwanengo dakika ya 38Uwanja wa CCM Kirumba
Septemba 13, 2026Kagera Sugar 1-1 Fountain GateMasanja Jesto dakika ya 26 na Andrew Vicent alijifunga dakika ya 33Uwanja wa Kaitaba
Septemba 15, 2026Yanga SC 1-0 Geita GoldOumar Kamara dk 55Uwanja wa KMC Complex
Septemba 15, 2026Azam FC 0-2 Simba SCFasika Idumba OG dk 58, Clatous Chama dakika ya 68.Azam Complex

SOMA HII PIA: Simba SC: Matokeo, Ratiba na Msimamo Ligi Kuu Bara 2026/27

Juma Kaseja afungashiwa virago

Matokeo ya Kagera Sugar 1-1 Fountain Gate ni mchezo wa mwisho wa Juma Kaseja aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo. Septemba 21, 2026 uongozi wa timu hiyo ulitoa taarifa yakuvunja benchi zima la ufundi. Cedric Kaze, raia wa Burundi alitambulishwa rasmi kupewa mikoba kuinoa timu hiyo.

Hitimisho

Mzunguko wa 6 Ligi Kuu Tanzania Bara mchezo uliokusanya mabao mengi ni ule Pamba Jiji FC 1-3 TRA United.Timu mbili zimefuta kazi makocha wao ilianza TRA United mzunguko wa 5 na mzunguko wa 6 Kagera Sugar. Yanga SC na Simba SC bado hazijapoteza mchezo 2026/27.

Share this: