Brighton vs Arsenal Premier League 2026/27 | H2H | Prediction | Lineups

ByLunyamadizo Mlyuka

September 19, 2026
Brighton vs ArsenalArsenal vs BrightonArsenal vs Brighton

Brighton vs Arsenal
Fabian Kocha Mkuu wa Brighton

Brighton vs Arsenal ni leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza 2026/27. Mchezo huu unatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na ubora wa timu zote mbili na malengo yao msimu huu. Arsenal wanatafuta kuendeleza rekodi yao nzuri, huku Brighton wakitaka kutumia uwanja wao wa nyumbani kupata pointi muhimu.

Mchezo huu utapigwa Uwanja wa American Express (Falmer Stadium) huko Brighton. Saa 11:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki. Mabingwa watetezi watakuwa kazini kusaka pointi 3 muhimu. Washika bunduki chini ya Kocha Mkuu, Mikel Arteta wanaongoza ligi wakiwa na pointi 12. Brighton ipo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 7. Fuatilia matukio muhimu, stats, lineups, Livescores kupitia SportPesa Score.

Ijue ratiba ya Arsenal: Arsenal FC: Ratiba, Matokeo, Msimamo, Kikosi na Habari Mpya

Shinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa

Una nafasi yakushinda mamilioni sasa hivi ukipaisha Kindege cha SportPesa. Rubani makini anapaa angani akiwa na uhakika. Mwanzo wa wiki muda sahihi kuvuna mamilioni. Bofya hapa chini ushinde sasa hivi.

Brighton vs Arsenal taarifa muhimu

Kipengele Maelezo
Mashindano Premier League
Mchezo Brighton & Hove Albion vs Arsenal
Siku Jumamosi, Septemba 19, 2026
Uwanja American Express
Muda Saa 11:00 jioni saa za Afrika Mashariki

Brighton vs Arsenal Prediction

Kutokana na fomu ya Arsenal iliyoanza nayo matokeo yatakuwa upande wake licha ya kwamba atakuwa ugenini. Mechi zote 4 washika bunduki wamecheza hivyo watakuwa kazini kusaka pointi 3 ugenini. Matokeo yanaweza kuwa Brighton & Hove Albion 1-2 Arsenal. Haya ni maoni ya mhariri sio matokeo rasmi.

Brighton vs Arsenal taarifa za wachezaji

Fabian Hurzeler Kocha Mkuu wa Brighton amesema atakosa huduma ya Femi Azeez mpaka pale mapumziko ya mechi za kimataifa yatakapokwisha. Pia amethibitisha kwamba Luka Vuskovic atajumuishwa kwenye mchezo na  Jaouen Hadjam kuna uwezekano akawepo pia.

Arsenal kwa upande wa kikosi Arteta amesema kila kitu kinakwenda sawa. Kuhusu Ben White amebainisha kwamba yupo fiti. Kuhusu kurejea kwa Jurrien Timber, Piero Hincapie, na Cristhian Mosquera, Arteta amesema: “Kila mmoja anazidi kuwa imara, tumekuwa na mazoezi nao kuona wanarejea kwenye ubora,”.

H2H

Arsenal wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya Brighton katika michezo 18 iliyopita, wakishinda mara kumi. Hii inawapa faida ya kisaikolojia wanapoelekea kwenye mchezo huu. Hata hivyo, Brighton wamekuwa timu ngumu kucheza nayo nyumbani na wanaweza kutoa upinzani mkali.

Katika msimu huu wa 2026/27, Arsenal wameanza vizuri, wakishika nafasi ya kwanza kwa pointi 12 kutoka mechi nne. Brighton wako nafasi ya nne na pointi 7 kutoka mechi nne. Takwimu hizi zinaonyesha kuwa timu zote ziko katika hali nzuri ya kiushindani.

Prediction Lineups Brighton & Hove Albion vs Arsenal

Brighton: Verbruggen, Kadıoglu, Vuškovic, Dunk, Boscagli, Gross, Ayari, Gómez, Yalcouye, De Cuyper, Kostoulas.

Arsenal: Raya, Timber, Konsa, Gabriel, Calafiori, Rice, Guimaraes, Saka, Odegaard, Tzolis, Havertz.

Hitimisho

Brighton vs Arsenal ni mchezo mkali ndani ya Premier League. Arteta amekuwa anapata matokeo kwenye mechi za ushindani. Anakutana na vijana wa Brighton wenye shauku yakusaka pointi 3 muhimu.

 

 

Share this: