
Azam FC ni moja ya timu iliyo ndani ya 3 bora katika msimamo wa NBC Premier League. Chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge baada ya mechi 7 imekusanya pointi 14. Timu hiyo imejumuisha wachezaji hodari akiwemo Feisal Salum maarufu kwa jina la Fei Toto, Pascal Msindo, Sopu na Idd Nado. Matokeo ya hivi punde ilikuwa Mzizima Dabi, Septemba 16, 2026 Azam FC 0-2 Simba SC, mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.
SOMA HII PIA:Usajili wa Azam FC 2026/27: Ilese, Taiwo Adolf Mtasigwa akutana na Thank You | SportPesa Blog
Shinda na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa hivi
Ni zamu yako kushinda na SportPesa, unaweza kushinda mamilioni sasa hivi. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kupitia Kampuni bora ya michezo ya kubashiri ya SportPesa bonyeza picha hii chini.
Msimamo wa Azam FC NBC Premier League 2026/27
| Nafasi | Timu | Mechi | Ushindi | Pointi |
| 1 | Yanga SC | 6 | 6 | 18 |
| 2 | Simba SC | 6 | 6 | 18 |
| 3 | Azam FC | 7 | 4 | 14 |
Azam FC ipo nyuma ya Yanga SC na Simba SC kwenye msimamo. Imepoteza mchezo mmoja pekee ilikuwa dhidi ya Simba SC. Ipo ndani ya tatu bora na safu ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 11.
Matokeo ya Azam FC
| Tarehe | Matokeo |
| 15 Agosti 2026 | Polisi Tanzania 1-1 Azam FC |
| 20 Agosti 2026 | Azam FC 2-1 TRA United |
| 23 Agosti 2026 | Azam FC 2-1 Pamba Jiji FC |
| 28 Agosti 2026 | Geita Gold 2-2 Azam FC |
| 31 Agosti 2026 | Kagera Sugar 0-2 Azam FC |
| 7 Septemba 2026 | Azam FC 2-0 Namungo FC |
| 16 Septemba 2026 | Azam FC 0-2 Simba SC |
Mipango ya Azam FC
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC ameweka wazi kuwa mpango mkubwa ni kupata matokeo mechi zijazo. Ibwe alibainisha kuwa mchezo dhidi ya Simba SC walipambana kutafuta matokeo licha yakupoteza. Amewaomba mashabiki kuendelea kuinga mkono timu hiyo.
“Msimu unaanza na tuna mechi nyingine zinafuata hizo tutapambana kupata matokeo mazuri. Wachezaji wanapambana kuona kila mchezo unakuwa na matokeo mazuri. Mashabiki wazidi kuwa nasi kupoteza mchezo mmoja haina maana kwamba tumetoka kwenye reli bado tupo imara,”.
Kwa nini msimamo bado unawapa nafasi?
Ligi bado ni mbichi ikiwa ni raundi ya 6. Matajiri wa Dar chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge bado wana nafasi kupata matokeo kwa mechi zinazofuata. Ikumbukwe kwamba ni mchezo mmoja pekee wamepoteza ndani ya msimu mpya wa 2026/27.

Mechi zijazo za Azam FC
| Tarehe | Mechi |
| Oktoba 8, 2026 | Coastal Union vs Azam FC |
| Oktoba 28, 2026 | Azam FC vs Mbeya City |
| Oktoba 31, 2026 | JKT Tanzania vs Azam FC |
| Novemba 20, 2026 | Azam FC vs Singida Black Stars |
| Novemba 27, 2026 | Fountain Gate vs Azam FC |
| Desemba 4, 2026 | Yanga SC vs Azam FC |
| Desemba 12, 2026 | Azam FC vs Dodoma Jiji FC |
Hitimisho
Azam FC wameanza kwa kasi ndani ya msimu wa 2025/26 na mchezo wao wa kwanza ugenini waligawana pointi na Polisi Tanzania. Kuna mechi nyingine kali zinafuata mbele yao. Miongoni mwa mchezo mkali ni ule wa Dar Dabi, Yanga SC vs Azam FC unatarajiwa kuchezwa Desemba 4, 2026.


