Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC Yanga SC vs Pamba Jiji FCSeleman Mwalimu Gomez
  • Yanga SC vs Pamba Jiji FC ni mchezo unaofuata kwenye NBC Premier League Agosti 28,2026
  • Saa 3:00 usiku mchezo huu utapigwa Uwanja wa KMC Complex, Mwenge
  • Pamba Jiji FC haijawahi kushinda mbele ya Yanga SC katika mechi zilizopita

Kituo kinachofuata ni Yanga SC vs Pamba Jiji FC NBC Premier League. Wababe hawa watakuwa Uwanja wa KMC Complex, Agosti 28 kwenye msako wa pointi 3 muhimu. Saa 3:00 usiku mchezo utachezwa ukiwa ni mzunguko wa 4. Pamba Jiji FC kutoka Mwanza, haijawahi kushinda dhidi ya Yanga SC.

Rekodi zinaibeba Yanga SC: Rekodi zinaibeba Yanga SC mbele ya Pamba Jiji FC Septemba 24 | Presha hakuna,mabingwa kazini

Taarifa muhimu kuhusu Yanga SC vs Pamba Jiji FC

Yanga SC vs Pamba Jiji FC
Maxi Mpia Nzengeli kiungo mshambuliaji wa Yanga SC

Mchezo: Yanga SC vs Pamba Jiji FC

Uwanja: KMC Complex

Muda: Saa 3:00 usiku

Mashindano: NBC Premier League 2026/27

Mzunguko: Mzunguko wa 4

Siku: Ijumaa

Tarehe: Agosti 28,2026

H2H Yanga SC vs Pamba Jiji FC

TareheMashindanoMechiMatokeo
03/10/2024Ligi Kuu ya NBCYanga SC vs.Pamba Jiji FC4–0
28/02/2025Ligi Kuu ya NBCPamba Jiji FC vs. Yanga SC0–3
24/09/2025Ligi Kuu ya NBCYanga SC vs.Pamba Jiji FC3–0
08/04/2026Ligi Kuu ya NBCPamba Jiji FC vs. Yanga SC0–3

Matokeo ya Yanga SC vs Pamba Jiji FC: Yanga SC 3-0 Pamba Jiji FC mabingwa waanza kwa kishindo | Kouma, Maxi na Mudathir wafunga

Yanga SC vs Pamba Jiji FC nafasi za timu

Kuelekea mchezo huu muhimu vinara ni Yanga SC wakiwa na pointi 9. Wananchi baada ya mechi 3 wameshinda zote na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 11. Inaongoza kwa kuwa na mabao mengi ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 24.

Pamba Jiji FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza haijawa na mwendo mzuri mwanzo wa msimu. Baada ya mechi 3 imepoteza mechi mbili na kupata sare moja. Kwenye msimamo ipo nafasi ya 12.

Maoni ya makocha Yanga SC vs Pamba Jiji FC

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema wamepata muda mchache wa maandalizi. Kocha huyo amebainisha kwamba licha ya muda huo wapo tayari kwa mchezo. Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita ilipata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

“Nitakuwa muongo nikisema tumepata muda wa kutosha kujiandaa kwa mechi hii. Tumekuwa na muda mchache wa maandalizi, lakini hatuna namna. Lazima tuingie uwanjani kusaka alama tatu. Najua pia Kocha Baraza, (Francis) naye hajapata muda wa kutosha wa kujiandaa,”.

Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Pamba Jiji FC, Francis Baraza amebainisha kuwa mchezo utakuwa mgumu. Matokeo yaliyopita hayakuwa mazuri kwao.

“Tumekuwa na mechi ngumu ambazo zimepita, mchezo wetu dhidi ya Yanga SC hautakuwa mwepesi. Tupo tayari na wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo. Tunakutana na timu ambayo inawachezaji wenye uzoefu nasi tupo tayari kuwakabili,”.

Hitimisho

Yanga SC vs Pamba Jiji FC ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Pamba Jiji FC haijawahi kushinda katika mechi zilizopita. Wananchi kwenye mechi 4 walishinda zote na kuvuna jumla ya pointi 12 kwenye ligi.

Share this: