- Ni Simba SC vs Coastal Union Uwanja wa Mej.Jen. Isahmuyo Agosti 27,2026
- Anthony Mligo, Ibraheem Jabaar, Nickson Kibabage kuikosa Coastal Union ya Tanga
- Shiza Kichuya, Farid Mussa kamili kumkabili mnyama saa 1:00 usiku
- Kwenye msimamo Simba SC ipo nafasi ya 2 ikiwa na pointi 9 inakabiliana na Coastal Union iliyo nafasi ya 14 na pointi 1.
Simba SC vs Coastal Union ni leo Uwanja wa Meja Jen.Isahmuyo mchezo wa mzunguko wa 4. Mnyama anacheza mchezo wake wa kwanza nyumbani baada ya kucheza mechi 3 ugenini. Simba SC kwenye msimamo ipo nafasi ya pili inakutana na Coastal Union iliyo nafasi ya 14.
Kijue kikosi cha Coastal Union: Coastal Union FC: History, Squad, Fixtures, and Latest Updates
Bado hujashinda? Cheza na ushinde mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa
Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini

Simba SC vs Coastal Union taarifa muhimu za mchezo

Mchezo: Simba SC vs Coastal Union
Mashindano: NBC Premier League
Uwanja: Meja. Jen. Isahmuyo
Muda: Saa 1:00 usiku
Tarehe: Agosti 27,2026
Mzunguko: Mzunguko wa 4
Duchu arejea, Kasali kamili gado

David Kameta maarufu kwa jina la Duchu amemaliza adhabu. Huyu ni mchezaji wa kwanza ndani ya kikosi cha Simba SC kuonyeshwa kadi nyekundu. Alionyeshwa katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, uliochezwa Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
Beki huyo alionyeshwa kadi dakika ya 53 alimchezea faulo beki David Luhende. Mwisho matokeo ilikuwa ni Kagera Sugar 0-2 Simba SC wakikomba pointi 3 za mchezo wa kwanza uliochezwa Agosti 16. Alikosekana kwenye mechi 3, ya kwanza ni ile aliyotolewa, Pamba Jiji FC na Singida Black Stars.
Kwa upande wa mlinda mlango namba moja, Mamadou Kasali naye amerejea katika ubora. Kipa huyu alipata maumivu mchezo wa kwanza dhidi ya Kagera Sugar. Tayari ameanza mazoezi na alikosekana kwenye mechi mbili ilikuwa dhidi ya Pamba Jiji FC na Singida Black Stars.
Simba SC vs Coastal Union taarifa ya wachezaji watakaokosekana
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema wapo wachezaji watakaokosekana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union. Licha ya kukosekana kwa wachezaji hao wanaamini waliopo watapambana kupata matokeo. Aliongeza kwa kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani.
“Anthony Mligo na Ibraheem Jabaar hawa tutawakosa kwenye mchezo kwa kuwa bado wana adhabu ya kadi nyekundu ambazo walipata. Nickson Kibabage bado hajawa fiti naye hatakuwa sehemu ya kikosi,” amesema.
Ikumbukwe kwamba Ibraheem Jabaar raia wa Nigeria alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 43. Ilikuwa Uwanja wa Kirumba, Pamba Jiji FC 1-2 Simba SC, Agosti 19, 2026. Kiungo huyo alimpiga kiwiko, Abdulkarim Yunus. Beki Anthony Mligo alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 84 Agosti 22, 2026.Ilikuwa Uwanja wa Airtel ulisoma Singida Black Stars 1-2 Simba SC. Beki huyo alimchezea faulo Yusuph Khamis.
Ijue ratiba ya Simba SC: Ratiba ya Simba SC NBC Premier League 2026/27 mechi 5 zijazo | Matokeo | SportPesa Blog
Coastal Union kamili na Farid Mussa
Kwa upande wa Coastal Union hawa wapo kamili kuikabili Simba SC. Wakali hawa kutoka Tanga wamebainisha kuwa maandalizi yapo vizuri. Kupitia kwa Ofisa Habari, Diego amesema kwamba wachezaji wote wapo vizuri akiwemo Farid Mussa nyota wa zamani wa kikosi cha Yanga SC.
“Kila kitu kipo sawa na maandalizi yanakwenda vizuri. Tunatambua hatujawa na matokeo mazuri kwenye mechi zetu zilizopita tutaingia uwanjani kwa tahadhari. Wachezaji waliopo wote wapo kamili akiwemo Farid Mussa, Shiza Kichuya,” amesema Diego.
Hitimisho
Simba SC vs Coastal Union saa 1:00 usiku wababe hawa watakuwa uwanjani kusaka pointi 3 muhimu. Seleman Matola, kocha msaidizi wa mnyama amebainisha kuwa mechi yao haitakuwa nyepesi. Mchezo wa mwisho walipokutana ubao wa Uwanja wa Mkwakwani ulisoma Coastal Union 1-2 Simba SC.

