- Azam FC vs Pamba Jiji FC ni leo Jumapili Agosti 23, 2026 Uwanja wa Azam Complex
- Muda ni kuanzia saa 1:00 usiku wababe hawa watakuwa uwanjani kusaka pointi 3 muhimu
- Aishi Manula mlinda wa matajiri atakosekana kwenye mchezo wa leo kutokana na adhabu ya kadi nyekundu
Burudani inaendelea leo Azam FC vs Pamba Jiji FC ni ratiba inayofuata kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Mzunguko wa 3 utapigwa Uwanja wa Azam Complex. Matajiri wa Dar wataingia uwanjani wakiwa hawajapoteza mchezo katika mechi mbili zilizopita.Walianza kwa sare ya kufungana 1-1 Polisi Tanzania na mchezo uliopita Azam FC 2-1 TRA United.
Hii hapa ratiba ya Ligi Kuu ya NBC: Ratiba ya Ligi Kuu ya NBC 2026/27: Mechi zote 240 | Tarehe | Muda wa mechi | Uwanja utakaotumika
Shinda mamilioni na SportPesa sasa hivi
Una nafasi yakushinda mamilioni kupitia SportPesa ukisuka mkeka wako. Azam FC vs Pamba Jiji FC leo saa 1:00 usiku. Bashiri kwa uwajibikaji, bofya link hapa.

Taarifa muhimu Azam FC vs Pamba Jiji FC

Makundi ya ligi ya NBC haya hapa: Ligi Kuu NBC 2026/27 | Yanga SC na Simba SC kileleni | Pointi 6 Mechi 2 | msimamo | Takwimu
| Kipengele | Azam FC | Pamba Jiji FC |
|---|---|---|
| Kocha Mkuu | Florent Ibenge | Francis Baraza |
| Mechi Zilizochezwa | 2 | 2 |
| Pointi | 4 | 1 |
| Mzunguko | Mzunguko wa 3 | Mzunguko wa 3 |
| Uwanja | Azam Complex (Nyumbani) | Azam Complex (Ugenini) |
| Tarehe na Siku | Agosti 23, 2026 (Jumapili) | Agosti 23, 2026 (Jumapili) |
| Muda wa Mechi | Saa 1:00 Usiku (EAT) | Saa 1:00 Usiku (EAT) |
| Mashindano | NBC Premier League | NBC Premier League |
Azam FC vs Pamba Jiji FC inachezwa muda gani?
Mechi kali ya Azam FC vs Pamba Jiji FC inatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku. Matajiri wa Dar watakuwa nyumbani kwenye mchezo wa pili. Katika mchezo uliopita walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TRA United.
Matokeo ya Azam FC 2026/27
15 Agosti 2026, Polisi Tanzania 1-1 Azam FC
20 Agosti 2026, Azam FC 2-1 TRA United
Kwenye mechi ya kwanza Azam FC walianza kwa kugawana pointi mojamoja ugenini. Mchezo wa pili walipata ushindi huku mlinda mlango Aishi Manula akionyeshwa kadi nyekundu. Kipa huyo atakosekana kwenye mchezo wa leo Uwanja wa Azam Complex.
Matokeo ya Pamba Jiji FC 2026/27
14 Agosti 2026, Pamba Jiji FC 1-1 Pamba Jiji FC
19, Agosti 2026, Pamba Jiji FC 1-2 Simba SC
Pamba Jiji FC yenye ngome yake Mwanza ilianza kwa sare ugenini. Mchezo wa kwanza kuwa nyumbani ilipoteza kwa kufungwa dhidi ya Simba SC. Licha yakutopata ushindi inaonyesha kwamba safu ya ushambuliaji inatumia nafasi ambazo inapata.
H2H Azam FC vs Pamba Jiji FC
| Tarehe | Mashindano | Mechi | Matokeo |
|---|---|---|---|
| 14/05/2026 | Ligi Kuu Bara | Azam FC vs Pamba Jiji FC | 2 – 0 |
| 02/03/2026 | Ligi Kuu Bara | Pamba Jiji FC vs Azam FC | 2 – 2 |
| 09/02/2025 | Ligi Kuu Bara | Pamba Jiji FC vs Azam FC | 1 – 0 |
| 14/09/2024 | Ligi Kuu Bara | Azam FC vs Pamba Jiji FC | 0 – 0 |
Azam FC vs Pamba Jiji FC timu hizi zimekutana kwenye mechi 4 ndani ya NBC Premier League. Ushindi ni mechi moja kwa Azam FC sawa na Pamba Jiji FC. Sare ni mechi 2.
Azam FC vs Pamba Jiji FC utabiri
Azam FC ina rekodi bora mwanzo wa msimu. Ina faida ya kuwa nyumbani dhid ya Pamba Jiji FC iliyotoka kupoteza dhidi ya Simba SC. Matokeo ni ushindi kwa Azam FC.
Utabiri wa matokeo: Azam FC 2-0 Pamba Jiji FC. Haya ni maoni ya mhariri sio matokeo rasmi. Mshindi atajulikana mara baada ya dakika90 kukamilika.
Hitimisho
Azam FC vs Pamba Jiji FC mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Matajiri wa Dar kwenye msimamo ni nafasi ya 6 wamekusanya pointi 4. Pamba Jiji FC nafasi ya 12 wamekusanya pointi 1 baada ya mechi 2.

