- Usajili mpya Simba SC 2026/27 umekamiliam, ambapo majina 8 ya nguvu yametambulishwa kuelekea msimu mpya.
- Ikumbukwe dirisha kubwa la usajili kwa Tanzania lilifungwa rasmi Jumamosi ya Agosti 15, 2026 baada ya kuwa wazi kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja.
- Mastaa wapya 8 wa Simba SC ni; Ibrahim Nindi, Ibraheem Jabaar, Keletso Makgalwa, Ibrahim Doumbia, Kelvin Nashon, Nathaniel Chilambo, Ismail Mgunda, Bakari Msimu.
- Makala hii inachambua kwa ufupi usajili mpya uliokamilika wa Simba SC 2026/27.
Tayari dirisha kubwa la usajili kwa Ligi zilizo chini ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF), limefungwa rasmi Jumamosi Agosti 15, 2026. Dirisha la usajili lilifungwa baada ya kuwa wazi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja, tangu Julai 6, 2026. Licha ya kuonekana kupitia kipindi kigumu kwenye dirisha hili la usajili, hasa baada ya kumpoteza kwa kushtukiza mshambuliaji Selemani Mwalimu Uongozi wa Simba SC umepambana. Timu hiyo imefanya maboresho kadhaa ya kikosi chao, kwa kusajili Nyota wapya 9 ambao watatumika msimu huu na makala hii inawachambua kwa ufupi mastaa hao.
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

SportPesa Aviator Maximum Payout – TZS Million
Muhtasari kuhusu usajili mpya Yanga SC 2026/27, Bilioni 15!
Simba SC imekamilisha usajili na kuwatangaza Nyota wao wapya 9, kuelekea msimu mpya wa 2026/27. Kwa tathimini ya harakaharaka, usajili wa Simba una sura mbili, upande ukiwa ni wa mafanikio na upande mwingine wa kufeli. Huu hapa usajili uliokamilika wa wachezaji wapya wa Simba SC 2026/27,

Ibrahim Abbas Nindi
Ndiye mchezaji wa mwisho kukamilisha usajili na kutambulishwa rasmi na Simba SC. Katika umri anaoelezwa kuwa nao, anakuja kuleta ushindani mkubwa wan amba hasa katika safu ya ulinzi. Ana uzoefu mkubwa akiwahi kupita katika timu mbalimbali za Ligi Kuu Bara.
KUJUA USAJILI NA MALENGO YA SIMBA 2026/27 SOMA HII: Simba SC: Usajili na malengo ya msimu wa 2026/27
Keletso Makgalwa
Huyu ni kiungo mshambuliaji hatari kutoka nchini Afrika Kusini, Makgalwa amejiunga na Simba akitokea Sekhukhune United. Makgalwa mwenye miaka 29, msimu uliopita alifanikiwa kutoa asisti 6 kwenye mechi 27 alizocheza ligi ya Afrika Kusini. Nyota huyo alitambulishwa na Simba SC Julai 25,2026.
Kelvin Nashon
Kelvin Nashon kiungo mkabaji alijiunga na kutambulishwa Simba SC rasmi Julai 19,2026. Nyota huyu mzawa msimu wa 2025/26 alikuwa akihudumu ndani ya kikosi cha Pamba Jiji FC. Tayari ameanza majukumu mapya akiwa na uzi wa unyamani.
Ibrahim Doumbia

Ibrahim Doumbia raia wa Mali ni mshambuliaji mpya alitambulishwa rasmi Julai 24 kutoka Klabu ya Association Sportive de Korofina ya Mali. Rekodi zinaonyesha kuwa alimaliza msimu akiwa na mabao 17 akiwa ni mfungaji bora. Ndani ya Ligi Kuu ya Tanzania bado mashabiki wa Simba wanasubiri moto wake.
KUHUSU USAJILI MPYA SIMBA SC 2026/27, SOMA HII: Mkakati wa usajili mpya Simba SC 2026/27 | Kelvin Nashon, Chilambo na Bakari Msimu kazi imeanza | SportPesa Blog
Ismail Mgunda
Amejiunga na Simba SC kwa ghafla kama mbadala wa Selemani Mwalimu ‘Gomez’ aliyetimkia Yanga SC. Msimu uliopita alihudumu ndani ya kikosi cha Mashujaa United ya Kigoma. Tayari straika huyo ameanza mazoezi tayari kwa ajili ya kuanza kuwasha moto uwanjani.
Nathaniel Chilambo
Nathaniel Chilambo beki wa kulia ambaye naye ni ingizo jipya msimbazi. Alikamilisha usajili wake na kutangazwa rasmi ndani ya Simba SC Julai 20, 2026. Mbavu hii ya kulia 2025/26 ilikuwa ikihudumu ndani ya kikosi cha Azam FC. Atakuwa akishirikiana na beki Shomari Kapombe ambaye ni nahodha wa timu hiyo.
Bakari Msimu
Msimu amejiunga na Simba SC akitokea Coastal Union ya Tanga. Akiwa na kikosi cha Coastal Union msimu uliopita alionyesha kiwango bora, na kuchangia mafanikio makubwa ya timu hiyo. Wanasimba wanasubiri kwa hamu kuanza kuona balaa lake uwanjani.
Ibraheem Jabaar

Miongoni mwa maingizo mapya ya nguvu waliyoyafanya Simba SC. Jabaar amejiunga na Simba SC akitokea kikosi cha Stellenbosch ya Afrika Kusini. Ameonyesha utashi mkubwa wa kujua kandanda, japo hofu imebaki juu ya nidhamu yake hasa baada ya tukio la kadi nyekundu ya uzembe baada ya kumpiga kiwiko mpinzani uwanjani.
KUJUA WALIOSAJILIWA, WALIOPEWA THANKYOU SIMBA, SOMA HII: Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Simba SC 2026/27 | Thank You | SportPesa Blog
Hitimisho
Usajili mpya Simba SC 2026/27 umekamilika na unaakisi taswira ya mchanganyiko wa mafaniko na kufeli. Simba ilipata pigo kubwa la kuondokewa na straika wao, Selemani Mwalimu ‘Gomez’ ambaye amejiunga na Yanga SC. Lakini juu ya yote, uongozi wa Simba ulijipanga na kushusha baadhi ya mastaa muhimu ambao wanatarajiwa makubwa. SportPesa Blog inaendelea kukuletea taarifa zote za papohapo.

