- FT: Simba SC 0-1 Police Kenye kilele cha Simba Day, Uwanja wa Uhuru, Agosti 8,2026
- Elvis Rupia afunga bao la ushindi dakika ya 90+1 zikisalia dakika 3 mpira kufika tamati
- Ibrahim Doumbia mshambuliaji wa mabao akwama kufunga, Neo Maema amerejea kazini
Ubao wa Uwanja wa Uhuru umesoma Simba SC 0-1 Police Kenya kilele cha tamasha la Simba Day. Matokeo haya ni mchezo wa kwanza kwa mnyama kupoteza 2026. Kabla ya mechi ya leo ya kirafiki, mnyama alicheza mechi tatu Kagame Cup, Rwanda alishinda moja na sare mbili. Bao la ushindi limefungwa na Elvis Rupia dakika ya 90+1.
Simba SC 0-1 Police Kenya kilele cha Simba Day
Ni Simba SC 0-1 Police Kenya haya ni matokeo rasmi kwenye mchezo wa kuhitimisha sherehe za miaka 90 ya timu hiyo iliyoanzishwa 1936. Mbele ya mashabiki waliojaza Uwanja wa Uhuru, wachezaji wameruhusu ushindi kuwa mali ya mgeni Police Tanzania. Ni dakika za lala salama safu ya ulinzi iliruhusu kufungwa.
Hili ni tamasha la 17 kufanyika mara baada ya kuanzishwa kwake na muasisi alikuwa ni Hassan Dalali aliyekuwa mwenyekiti wa Simba SC wakati huo. Timu nyingine ambayo iliwahi kuifunga Simba SC kwenye tamasha ni TP Mazembe kupitia kwa Jean Baleke. Ikumbukwe kwamba Rupia aliwahi kucheza katika NBC Premier League akiwa na Klabu ya Singida Black Stars.
Bao la ushindi limefungwa wakati Simba SC walipokuwa wakifanya shambulizi kupitia kwa Ibrahim Doumbia. Mara baada ya mshambuliaji huyo kushindwa kufunga, Police Kenya wakawa kwenye umiliki wa mpira. Walipigiana pasi mpaka lango la mnyama na kupelekea kuruhusu bao hilo zikiwa zimesalia dakika 3 mpira kufika mwisho.
Neo maema amerejea kazini, Doumbia akwama
Kiungo wa Simba SC, Neo Maema amerejea kazini mara baada ya mkataba wake wa mkopo kuishia.Alirejea Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini na Agosti 6 alikuwa sehemu ya kikosi kilichofanya mazoezi Uwanja wa Uhuru. Kwenye mchezo wa leo alianzia benchi na aliingia dakika ya 30 akichukua nafasi ya Yusuph Kagoma ambaye alipata maumivu kipindi cha kwanza.
Mshambuliaji wa mabao Ibrahim Doumbia amekwama kufungua akaunti ya mabao mbele ya mashabiki wa Tanzania. Katika orodha ya wachezaji wapya hakuna aliyepata nafasi yakufunga leo kwenye kilele cha Simba Day. Mchezo unaofuata baada ya huu ni Agosti 12, 2026, Yanga SC vs Simba SC, Kariakoo Dabi, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.


