Wananchi hawana jambo dogo kuna orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2026/27 wazawa na wageni tayari kwa kazi. Miongoni mwa jina ambalo limekuwa gumzo ni Peter Shalulile raia wa Afrika Kusini. Chuga Boy kutoka Fountain Gate alikuwa mchezaji wa kwanza kutambulishwa. Mabingwa hao watetezi wana benchi jipya ambalo litakuwa na kazi kuwanoa wachezaji katika mechi za ushindani.
Ijue timu itakayokabilana na Yanga SC: Wiki ya Mwananchi SportPesa Yanga Day 2026 imepamba moto | Wachezaji wapya na mchezo wa kirafiki
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2026/27 na benchi la ufundi

Leo tumekuletea orodha ya wachezaji waliosajiliwa Yanga SC 2026/27 mara baada ya dirisha la usajili kufunguliwa. Kwa mujibu wa Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga SC alibainisha kuwa wamesajili wachezaji bora. Aliongeza kuwa kila mchezaji atafanya kazi kubwa uwanjani.
“Tumefanya usajili makini kwa kuleta wachezaji wenye uwezo mkubwa. Tunatambua kwamba kila mmoja anatambua umuhimu wa kuwa kwenye hii timu. Kazi kubwa ni kuhakikisha mashabiki wanafurahi,”.
Hawa hapa wachezaji wapya na benchi la ufundi ambalo ni jipya tumekusogezea. Hawa wote watakuwa na kazi kutetea taji ambalo walitwaa msimu wa 2025/26:-
Farouk Komara
Alitambulishwa Agosti 4,2026. Huyu ni mali ya Yanga SC. Ni raia wa Ivory Coast beki mwenye uwezo wa kucheza kiungo mkabaji. Ana miaka 26 alikuwa Klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini kabla ya kutambulishwa Jangwani.
Peter Shalulile
Mshambuliaji wa zamani wa Mamelod Sundowns alitambulishwa Yanga SC, Julai 27,2026 kwa kandarasi ya miaka miwili. Yupo ndani ya Bongo kwa ajili ya kazi. Miongoni mwa washambuliaji wenye uwezo mkubwa na alikuwa anahitajika na timu kubwa Afrika akachagua Jangwani.
Albert Kangwanda
Yanga wanaye MVP wa Zambia, Albert Kangwanda. Msimu uliopita alifunga mabao 17 na asisti 9 amesaini dili la miaka miwili. Amecheza Al Hilal Omdurman ya Sudan, CSF Spartanii (Moldava), HNK Gorica, (Croatia) na Red Arrows ya Zambia. Julai 24 2026 alitambulishwa
Cheikh Touré
Huyu ni mshambuliaji raia wa Ufaransa anaitwa Cheikh Touré ana miaka 29. Nyota hoyo amewahi kupita kwenye vilabu vya AS Nancy ya Ufaransa na Al-Jabalain ya Saudi Arabia. Julai 24 2026 alitambulishwa kuwa njano na kijani.
Zakouani
Yanga SC imekamilisha usajili wa Housseine Zakouani (28) raia wa Comoros. Nyota huyo amelelewa kwenye academy ya Olympique Marseille Ufaransa,pia amecheza kwenye vilabu vya Châteauroux, Hyères 83 FC na US Thionville Lusitanos zote za Ufaransa. Amejiunga na Yanga SC kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Al-Zulfi ya Saudi Arabia. Alitambulishwa Julai 24,2026.
Mwijage
Erick Mwijage winga mpya ndani ya Yanga SC. Julai 22,2026 alitambulishwa katika kikosi cha Wananchi. Huyu 2025/26 alikuwa mali ya KMC FC ambayo imeshuka daraja. Atakuwa na mabingwa watetezi wa NBC Premier League 2026/27.
Mohamed Mussa
Alitambulishwa Yanga SC Julai 21 Mohamed Mussa ni beki. Mzawa huyu alikuwa ndani ya Mashujaa FC 2025/26. Anaanza changamoto mpya akiwa ni kijani na njano.
Juma Issa Abushir

Usajili mpya Yanga SC : Usajili Yanga SC 2026/27: Hawa hapa wachezaji wapya 5 wazawa
Julai 18,2026 alitambulishwa Juma Issa Abushir huyu ni beki kutoka Fountain Gate maarufu kwa jina la Chuga Boy. Mchezaji kijana ambaye alikuwa ana uhakika wa namba alipokuwa msimu uliopita.
Mihambo
Hussen Mihambo nyota wa zamani wa Mashujaa FC Julai 20,2026. Atakuwa kwenye changamoto mpya msimu wa 2026/27.
Abdulnasir Muhamed
Beki wa kulia Abdulnasir Muhamed aliyekuwa Mashujaa FC. Ni kijani na njano alitambulishwa Julai 20,2026. Kutoka mwisho wa reli Kigoma mpaka Jangwani kwenye maisha mapya.
Benchi la ufundi
Simo Dladla
Ni kocha msaidizi ametambulishwa Julai 21, 2026 Simo Dladla raia wa Afrika Kusini. Kocha huyu ana uzoefu kwenye masuala ya ufundi ambapo 2020/21 alikuwa Kocha Mkuu Richard Bay, 2021/22 alikuwa kocha msaidizi Maroka Swallows, 2022/23 alikuwa Kocha Mkuu Uthonghath FC, 2023/25 alikuwa Kocha Mkuu, Maritzburg Utd na 2025/26 alikuwa kocha msaidizi Golden Arrows.
Kagisho Dikgacoi
Coach wa set piece anaitwa Kagisho Dikgacoi Julai 21,2026. Huyu ni mchezaji wa zamani wa Fulham FC 2008/11, Crystal Palace 2012/14 na Cardiff City 20214/16. Raia huyu wa Afrika Kusini alicheza Kombe la Dunia 2010. AFCON 2008/13 na Europa League Final 2010 akiwa na Fulham.
Yardaan Valodia
Mchambuzi wa mbinu Yardaan Valodia ametambulishwa Julai 21,2026 Yanga SC alifanya kazi na Memolodi Sundown, Moroka Swallow, Golden Arrows. Mtaalamu huyu amepata mafunzo FC Barcelona na leseni ya CAF.
Greg Etafia
Kocha wa makipa Greg Etafia huyu ni kocha wa makipa ametambulishwa Julai 21,2026. Amefanikiwa kuifundisha timu ya taifa ya Nigeria, Nigeria (Sydney Olympics 2000), AFCON 2004 nafasi ya 3 akiwa na timu ya taifa ya Nigeria.
Manqoba Mngqithi
Kocha Mkuu Manqoba Mngqithi raia wa Afrika Kusini alitambulishwa Julai 10,2026. Tayari ameanza kazi kwa kuwapa mbinu wachezaji wapya na aliowakuta. Kazi kubwa ni kuhakikisha anapambana kutetea taji na mpira safi uwanjani.

