- Usajili Yanga SC 2026/27 umekamilika kwa zaidi ya asilimia 90, na kuendelea kuzua mjadala mkubwa wa kwenye soka ndani na nje ya Tanzania.
- Kwa rekodi rasmi mpaka sasa Yanga SC imekamilisha usajili wa mastaa wapya 11 ambao ni; Juma Abushiri, Hussein Mihambo, Abdulnasir Muhamed, Mohamed Mussa, Erick Mwijage, Suleiman Mbarouk, Ibrahima Toure, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Peter Shalulile na Fred Ngoma.
- Kwa mujibu wa Msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe amesalia mchezaji mmoja kutambulishwa huku mastaa mbalimbali wakihusishwa.
- Kati ya mastaa hao wachezaji 6 wapya ni wachezaji wazawa, huku wachezaji 5 wakiwa ni wa kigeni. Makala hii inachambua kwa ufupi usajili mpya wa wazawa Yanga SC 2026/27.
Uongozi wa Yanga SC hautanii, ambapo mpaka sasa umekamilisha usajili wa wachezaji 11 katika dirisha hili kubwa la usajili, kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa 2026/27. Kati ya Nyota hao wachezaji 6 ni Nyota wazawa, huku wachezaji watano waliosalia wakiwa ni Nyota wa kigeni. Haya yote yanafanyika wakati ambao, zimebaki siku 15 tu, kuelekea kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27 huku Yanga SC wakianza kampeni kama bingwa mtetezi. Makala hii inachambua kwa ufupi mastaa wapya wazawa watakaovaa uzi wa Yanga SC msimu wa 2026/27.
Je, bado hujashinda mamilioni ya aviator ‘Kindege’ cha SportPesa? Cheza ushinde mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.
Muhtasari Kuhusu usajili mpya Yanga SC 2026/27, Bilioni 15!

Kwa mujibu wa Msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe amesema kuwa Bajeti ya usajili msimu huu Rais wa Yanga SC Eng. Hersi alimuzungumza na mfadhili wao GSM na kumuuliza msimu huu tunafanyaje. GSM akamjibu kuwa tafuta wachezaji pesa nitatoa. Kuendana na taarifa hiyo ya Kamwe GSM ameweka bajeti ya Bilioni 15 kusajili tu.
Hawa hapa wachezaji wapya wazawa wa Yanga SC 2026/27
Mohamed Mussa
Nyota huyu ni mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC, ambaye msimu uliopita alikuwa akihudumu na kikosi cha Mashujaa FC ya Kigoma. Alitambulishwa Jangwani rasmi Julai 21, 2026. Mussa amesajiliwa kuongezea nguvu safu ya ulinzi ya Yanga SC.
Juma Issa Abushir
Mchezaji wa kwanza kutambulishwa mitaa ya Jangwani ni beki chipukizi ambaye ni mzawa. Julai 18,2026 alitambulishwa Juma Issa Abushir huyu ni beki kutoka Fountain Gate maarufu kwa jina la Chuga Boy. Alianza maisha ya soka kwenye kituo cha Future Stars kilichopo Arusha akiwa na miaka 6 tu.
Hussein Mihambo
Mali nyingine mpya ndani ya kikosi cha Yanga SC ni mshambuliaji wa kazi. Anaitwa Hussen Mihambo aliyekuwa akicheza Mashujaa FC. Ni Julai 20,2026 alitambulishwa Jangwani kuwa ingizo jipya.
Abdulnasir Muhamed
Beki wa kulia Abdulnasir Muhamed aliyekuwa Mashujaa FC naye ni kijani na njano. Alitambulishwa Julai 20,2026 kuwa mtaa wa Kariakoo.Ni kandarasi ya miaka miwili inaelezwa kuwa amesaini.
Erick Mwijage
Mwijage amejiunga na Yanga SC, akisajiliwa kutoka kikosi cha KMC ambayo tayari imeshuka daraja. Mwijage ndani ya Ligi Kuu ya NBC amefanikiwa kupita ndani ya timu mbalimbali ikiwemo; Kagera Sugar na Geita Gold. Mwijage anakuwa mchezaji wa 5 kusajiliwa na Yanga SC na kutambulishwa ndani ya dirisha hili la usajili.
Suleiman Mbarouk
Klabu ya Young Africans SC imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Suleiman Mbarouk, mwenye umri wa miaka 18, akitokea JKU FC ya Zanzibar. Suleiman ameweka saini ya mkataba wa miaka mitatu na Yanga SC, huku klabu hiyo ikikamilisha taratibu za kuvunja mkataba wake uliokuwa umebaki kwa mwaka mmoja na JKU.
Hitimisho
Usajili Yanga SC 2026/27 unakaribia kukamilika huku ukitoa taswira ya mchanganyiko wa uzioefu na ubora. Ali Kamwe, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano kutoka Jangwani amebainisha watafanya maboresho makubwa. Timu hiyo ina kibarua cha kutetea ubingwa 2026/27. Endelea kufuatilia SportPesa blog.

