Aziz Ki na Allan Okello AIAziz Ki na Allan Okello AI
  • Taarifa za Aziz Ki kurudi Yanga SC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu NBC zimezidi kushika kasi.
  • Taarifa hizi zinakuja zikiwa zimesalia siku chache kabla ya dirisha kubwa la usajili kufunguliwa, mara baada ya ligi kumalizika.
  • Nyota huyo kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Al Ittihad ya Libya, aliyojiunga nayo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.
  • Tetesi za usajili ndani ya Yanga SC zimethibitisha, mpango huo upo na una asilimia kubwa.

Taarifa za Aziz Ki kurudi Yanga SC kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu NBC zimezidi kushika kasi, zikiwa zimesalia siku chache kabla ya dirisha kubwa la usajili kufunguliwa. Nyota huyo kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Al Ittihad ya Libya aliyojiunga nayo akitokea Wydad Casablanca ya Morocco. Tetesi za usajili ndani ya Yanga SC zimethibitisha, mpango huo upo na una asilimia kubwa.

Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Ligi Kuu ya NBC 2025/26; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog.

Cheza na ushinde sasa na ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni muda huu

Je, hujashinda na kindege cha SportPesa? Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi mamilioni muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kubashiri SportPesa bonyeza picha hii chini.

Aviator game promotional banner featuring a red propeller plane and a jackpot of 800,000,000.

Aviator: High-flying wins up to 800,000,000.

Kuhusu Aziz Ki kurudi Yanga SC

Aziz Ki vs Mamelodi Sundowns
Aziz Ki vs Mamelodi Sundowns

Taarifa za ndani ya Yanga SC zimethibitisha kuwa, upo uwezekano mkubwa wa nyota huyo kurejea Jangwani katika dirisha lijalo la usajili. Kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kuchapishwa na vyombo mbalimbali vya Habari, inaelezwa Aziz Ki anataka kurejea Yanga. Hii ni kutokana na changamoto ya maisha yake ya soka tangu alipoondoka, ambapo amekosa nafasi ya kucheza mara kwa mara huko alipo.

Ripoti hizo zimethibitisha kuwa Yanga SC nao wamekuwa wakifuatilia kwa karibu hatma ya mchezaji huyo, huku mashabiki wakitamani kumuona akirudi tena. Katika siku za karibuni, tetesi hizo zimeongezeka baada ya Aziz Ki mwenyewe kunukuliwa akieleza kuwa mlango wa kurejea Tanzania bado uko wazi.  Aziz Ki alijijengea heshima kubwa akiwa Yanga kutokana na uwezo wake wa kutengeneza nafasi, kufunga mabao muhimu na kuamua matokeo ya mechi kubwa.

Baadhi ya wachambuzi wa soka wanaamini kama dili hilo litafanikiwa, basi kurejea kwake kunaweza kuongeza ushindani mkubwa katika kikosi cha Yanga SC. Uzoefu wake wa kucheza mashindano ya kimataifa, na uwezo wa kubeba majukumu makubwa uwanjani vinathibitisha hilo. Hata hivyo, hadi sasa hakuna tamko rasmi lililotolewa na Yanga SC, wala upande wa mchezaji kuhusu kukamilika kwa mazungumzo yoyote ya usajili.

SOMA HII PIA: Aziz Ki atarejea Yanga SC | Wydad Casablanca kumtema | Tetesi za usajili

Maisha ya Aziz Ki ndani ya Yanga SC

Aziz Ki vs Simba
Aziz Ki vs Simba

Aziz Ki ambaye ni Nyota wa kimataifa wa Burkina Faso, aliitumikia Yanga SC kwa mafanikio makubwa tangu alipojiunga nao akitokea ASEC Mimosas msimu wa 2022/23. Katika kipindi cha misimu 3 aliyochezea Yanga SC, Aziz Ki alifanikiwa kucheza mechi 114, akifunga mabao 52 na kutoa pasi za mwisho (assists) 32. Hii ilimfanya kuwa miongoni mwa Nyota hatari kwenye Ligi Kuu ya NBC, kabla ya kujiunga na Wydad Casablanca.

Mafanikio ya Aziz Ki akiwa na Yanga SC

Makombe

Akiwa na Yanga SC katika kipindi hiko cha misimu mitatu, Aziz Ki alifanikiwa kukusanya makombe 9, ambayo ni; Makombe 2 ya Ligi Kuu ya NBC, makombe 2 ya CRDB Federation Cup na makombe 2 ya Ngao ya Jamii. Makombe matatu yaliyosalia ni ya mashindano yasiyo rasmi.

Mfungaji bora na MVP 2023/24

Aziz Ki
Aziz Ki

Msimu wa 2023/24 unabaki kuwa msimu wake bora zaidi akiwa na Yanga SC, ambapo alifanikiwa kufunga mabao 21 na kuwa mfungaji bora (Top Scorer) wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Pamoja na tuzo hiyo Aziz Ki pia alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka MVP wa ligi Kuu Bara. Ikumbukwe kuwa pia msimu huo alitoa asisti 16 za mashindano yote.

SOMA HII ZAIDI: Aziz Ki ameanza kazi Wydad Casablanca, Yanga SC ameacha rekodi

Mafanikio mashindano ya CAF

Aziz Ki ni miongoni mwa mastaa wa kizazi cha dhahabu cha Yanga SC ambacho kilicheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, msimu wa 2022/23. Lakini pia aliiongoza Yanga SC kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2023/24. Msimu huu walikaribia kuwaondosha mabingwa wa sasa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Atimkia Wydad Casablanca

Aziz Ki Wydad
Aziz Ki Wydad

Kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2024/25, Aziz Ki aliwaaga mashabiki wa Yanga SC kuwa anajiunga na Wydad Casablanca ya Morocco. Usajili huo ulilazimika kukamilika kabla ya msimu kumalizika, kwa kuwa Wydad walikuwa wanamuhitaji mapema kwa ajili ya mashindano mapya ya Club World Cup. Hata hivyo, mambo hayajaonekana kwenda kama ilivyotarajiwa katika klabu alizochezea baada ya kuondoka Tanzania.

SOMA HII PIA: Stephane Aziz Ki huyoo Marekani kuwavaa Manchester City ya Guardiola

Hitimisho

Taarifa kuhusu Aziz Ki kurudi Yanga SC zimeendelea kubaki katika kiwango cha tetesi, kwa kuwa hakuna upande uliothibitisha. Mashabiki wa Yanga SC wanasubiri kuona kitakachotokea mara dirisha la usajili litakapofunguliwa. Iwapo Aziz Ki atarejea Yanga, itakuwa ni habari kubwa kwa soka la Tanzania kutokana na mchango mkubwa aliowahi kuutoa katika mafanikio ya timu hiyo.

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.