- Qatar vs Switzerland utabiri wa Kombe la Dunia 2026 unaipa nafasi kubwa Switzerland kuibuka na ushindi.
- Huu ni mchezo wa pili wa Kundi B la mashindano hayo, mchezo unaotarajiwa kupigwa jijini Santa Clara siku ya Jumamosi saa 4 usiku.
- Mara ya mwisho na ya pekee kwa timu hizo kukutana ilikuwa mwaka 2018, ambapo Qatar walishinda 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
- Makala hii inakuchambulia dondoo muhimu za mechi
Qatar vs Switzerland utabiri Kombe la Dunia 2026 unaipa nafasi kubwa Switzerland kuibuka na ushindi. Huu ni mchezo wa pili wa Kundi B la mashindano hayo, mchezo unaotarajiwa kupigwa jijini Santa Clara siku ya Jumamosi. Mara ya mwisho na ya pekee kwa timu hizo kukutana ilikuwa mwaka 2018, ambapo Qatar walishinda 1-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.
Fuatilia mwenendo wote wa mashindano ya Kombe la Dunia 2026; Ratiba, matokeo, mechi, magoli na habari za papo kwa papo kupitia SportPesa Blog na ushinde mamilioni kwa kubashiri kupitia odd kubwa za SportPesa.
Shinda mamilioni na Twenzetu Duniani na SportPesa kwenye mechi Kombe la Dunia 2026
Twenzetu Duniani ya SportPesa inakuletea nafasi ya kushinda mamilioni kupitia odds kubwa za mechi za Kombe la Dunia. Ili kushinda beti mechi ya Ufunguzi kati ya Qatar vs Switzerland kwa kubonyeza picha hii chini.

Kuhusu Qatar vs Switzerland utabiri Kombe la Dunia 2026

Qatar
Timu hizi mbili zinakutana kwa mara ya kwanza katika mechi rasmi, katika mashindano haya timu hizi zimepangwa Kundi B pamoja na Canada na Bosnia na Herzegovina. Qatar wanashiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya pili pekee, katika historia yao baada ya kushiriki kama wenyeji mwaka 2022.
Qatar au kwa jina la utani ‘The Maroons’ walifuzu mashindano ya mwaka huu baada ya kuifunga UAE mabao 2-1 mwezi Oktoba mwaka jana. Hata hivyo, tangu ushindi huo wamecheza mechi sita bila kupata ushindi wowote, ikiwemo kupoteza 1-0 dhidi ya Ireland katika mechi ya kirafiki mwishoni mwa Mei. Kikosi hiko cha kocha, Julen Lopetegui kilitoka sare ya 1-1 dhidi ya El Salvador katika mchezo wao wa mwisho wa maandalizi kabla ya Kombe la Dunia uliochezwa Juni 6.
Kundi B linaonekana kuwa wazi kwa timu zote nne kutokana na uwepo wa timu zinazokaribiana viwango. Qatar, Canada, Bosnia na Herzegovina. Ushindi katika mechi ya kwanza unaweza kuiweka Qatar katika nafasi nzuri ya kufuzu hatua ya mtoano, kwa mara ya kwanza katika historia yao ya Kombe la Dunia.
SOMA HII PIA: Canada vs Bosnia Preview & Ubashiri | Kombe la Dunia 2026, 12 Juni 2026 | Utabiri, Habari za Timu na Vikosi Vinavyotarajiwa
Switzerland
Kwa upande wa Uswisi, hii itakuwa mara ya 13 kushiriki Kombe la Dunia. Katika mashindano matatu yaliyopita ya Kombe la Dunia walifika hatua ya 16 bora, hivyo kuondolewa mapema katika hatua ya makundi kutachukuliwa kama matokeo ya kushangaza. Mafanikio yao makubwa zaidi katika Kombe la Dunia yalikuja miaka ya 1934, 1938 na 1954 walipofika robo fainali. Kikosi cha kocha, Murat Yakin kinaingia katika mchezo huu baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Australia katika mechi ya mwisho ya kirafiki, huku wakiifunga Jordan mabao 4-1 mwishoni mwa Mei.
Uswisi wamepoteza mechi moja tu kati ya 14 zao za mwisho katika mashindano yote, hii ni baada ya kipigo cha mabao 4-3 dhidi ya Ujerumani katika mechi ya kirafiki mwezi Machi. Kutokana na hali hiyo, Uswisi wanaingia kwenye Kombe la Dunia wakiwa katika kiwango kizuri na wakilenga kuanza kwa kishindo kwa ushindi. Hii ni kabla ya kuvaana na Bosnia, Herzegovina na Canada.
Qatar vs Switzerland h2h
Qatar wamekutana na Switzerland mara moja tu hapo awali, ambapo Qatar walishinda bao 1-0 katika mechi ya kirafiki iliyochezwa mwaka 2018. Hivyo hii ni nafasi kwa kila timu kubadilisha rekodi hiyo ikiwa wataibuka na ushindi. Je, Qatar ataendeleza ubabe?
Fomu za Hivi Karibuni
Qatar: L, L, D, L, D, L
Uswisi: W, D, L, D, W, D
Je, bado hujashinda pesa? Cheza aviator ‘Kindege’ cha SportPesa uvune mamilioni sasa
Changamka! sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi zaidi ya Milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Jipatie nafasi ya kujishindia milioni 800 na Aviator
Habari za Timu na majeruhi

Qatar
Safu ya ushambuliaji inatarajiwa kuongozwa na Akram Afif, Yusuf Abdurisag na Edmilson Junior. Afif tayari ameifungia Qatar mabao 39 tangu alipoanza kuichezea, na anatarajiwa kuwa tegemeo kubwa la mabao katika mashindano haya. Edmilson Junior bado anasaka bao lake la kwanza akiwa na timu ya taifa, huku Mahmud Abunada akitarajia kuanza langoni. Pedro Miguel na Boualem Khoukhi wanatarajiwa kuunda safu ya kati ya ulinzi.
Switzerland
Kwa upande wa Uswisi, kocha Murat Yakin ana machaguzi mengi hasa katika safu ya ushambuliaji. Breel Embolo mwenye mabao 24, akiwa na timu ya taifa ni mmoja wa mastaa wanaotazamwa kuanza nafasi ya mshambuliaji wa kati. Mshambuliaji wa Burnley, Zeki Amdouni, anatarajiwa kuanza pia. Uswisi pia watategemea uzoefu wa Manuel Akanji, Ricardo Rodriguez na Granit Xhaka, huku Remo Freuler akiongoza safu ya kiungo.
Vikosi Vinavyotarajiwa
Qatar
Abunada; Al-Oui, Khoukhi, Pedro Miguel, Ahmed; Laye, Fathi, Gaber; Abdurisag, Afif, Edmilson.
Switzerland
Kobel; Widmer, Akanji, Elvedi, Rodriguez; Xhaka, Freuler; Vargas, Rieder, Ndoye; Amdouni.
Utabiri wetu na hitimisho

Huu ni mchezo mgumu kutabirika, lakini matokeo ya sare yanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kutokea. Hata hivyo, Uswisi wana ubora mkubwa zaidi, katika maeneo mengi ya uwanja pamoja na uzoefu mkubwa wa Kombe la Dunia. Kwa uchanganuzi wetu tunawapa nafasi kubwa Switzerland kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

