Mabingwa wa kihistoriaMabingwa wa kihistoria
  • Namba hazidanganyi, ubingwa unanukia Yanga SC ndivyo unavyoweza kusema, baada ya matokeo mabovu ya wapinzani wake katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara yaani (NBC Premier League),
  • Mpaka sasa Yanga SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa pengo la tofauti ya pointi 8, dhidi ya Simba SC walio kwenye nafasi ya 2 japo wana mechi moja ya kiporo.
  • Makala hii inakupitisha katika dondoo muhimu na Takwimu za msimamo wa ligi Kuu Tanzania bara, na kueleza kwanini ubingwa unanukia Yanga SC.

Ubingwa unanukia Yanga SC ndivyo unavyoweza kusema na namba hazidanganyi, hii ni baada ya matokeo mabovu ya wapinzani wake katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara yaani (NBC Premier League), klabu za Simba SC na Azam FC. Mpaka sasa Yanga SC inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC kwa pengo a tofauti ya pointi 8. Makala hii inakupitisha katika dondoo muhimu na Takwimu za msimamo wa ligi Kuu Tanzania bara, na kueleza kwanini ubingwa unanukia Yanga SC.

SOMA HII PIA: Yanga SC na maajabu 2025/26 | Matokeo ya hivi punde, wafungaji na msimamo NBC Premier League

Bado haujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mpaka milioni 800 sasa

Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Sportpesa Aviator- 800Mil

Ubingwa unanukia Yanga SC, pointi 8 kileleni msimamo Ligi Kuu ya NBC

Msimamo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)
Msimamo wa Ligi Kuu Bara (NBC Premier League)

Mpaka kufikia sasa Yanga SC ndio vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara, hii ni baada ya kufikisha pointi 44, baada ya kucheza mechi 18. Simba SC wanakamatia nafasi ya 2 na pointi zao 36 walizokusanya katika michezo 17, huku pia wakiwa na mchezo mmoja wa kiporo. Azam FC wao wanasalia kwenye nafasi ya 3, na pointi zao 34 walizokusanya katika michezo 18.

Takwimu hizo zinamaanisha kuwa Yanga SC sasa wanaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi 8 dhidi ya wapinzani wake wa karibu timu za Simba SC na Azam FC. Hii inawafanya Yanga SC waanze kusikia harufu ya ubingwa wa msimu huu wa 2025/26. Ikumbukwe mpaka sasa Yanga SC ndio mabingwa watetezi, wakifanya hivyo kwa misimu 4 mfululizo.

SOMA HII ZAIDI: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu

Simba SC, Azam FC hali tete!

Matokeo ya Simba SC na Azam FC leo
Matokeo ya Simba SC na Azam FC leo

Wapinzani wakuvwa wa Yanga SC katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara, yaani Simba SC na Azam FC leo alhamisi walikuwa na kazi pevu ambapo kila timu imeshuka uwanjani na kuambulia sare. Simba SC wakiwa ugenini Arusha kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, wamelazimishwa Suluhu na TRA. Huku vilio vikisikika Msimbazi, Azam FC wanaokamatia nafasi ya tatu kwenye msimamo, nao wameambulia Suluhu mbele ya wenyeji wake Mbeya City.

Hali hii inazifanya timu hizi kupoteza pointi 4 kwa ujumla yaani pointi mbili kila timu, huku zikiongeza pengo la pointi 2 kila mmoja kulinganisha na vinara Yanga SC. Hii inafanya mbio za ubingwa zizidi kufifia kwao, na kuipa Yanga nafasi kubwa ya kutawala kileleni kwa msimamo bila presha. Hali inazidi kuwa ya hofu kwa wapinzani hawa wa Yanga SC ikizingatiwa imesalia mizunguko michache ligi kuisha.

SOMA HII PIA: Yanga SC wiki ya wananchi ni Ijumaa Septemba 12

Zimebaki mechi 12 tu, ligi kuisha

NBC Premier League ratiba 2025/26 Aprili
Azam FC

Huku Ligi Kuu ya NBC ikiwa imeingia mzunguko wa 18, hii inamaanisha kuwa mpaka sasa zimesalia mechi 12 tu, ligi kumalizika na bingwa kupatikana. Ikumbukwe kwenye Ligi Kuu ya NBC kuna timu 16, ambapo kila timu hucheza mechi 2 dhidi ya timu nyingine zote kwenye ligi (Mechi ya nyumbani na mechi ya ugenini). Kati ya mechi hizo moja inakuwa ya mzunguko wa kwanza, na nyingine ya mzunguko wa pili. Hivyo kihesabu timu hucheza mechi 30 kabla ya kumaliza msimu.

Hitimisho: Yanga SC bado ni ‘Unbeaten’ 2025/26

Ubingwa unanukia Yanga SC
Yanga

Pamoja na rekodi nyingi bora za Yanga SC walizoandika msimu huu, mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC wanashikilia rekodi ya kutopoteza mechi ‘unbeaten’. Mpaka sasa ni timu 2 tu, kwenye ligi ambazo hazijanusa ladha ya kufungwa, ambazo ni Yanga SC na Azam FC. Mabingwa hao mara 31 wa NBC Premier League wanaifukuzia rekodi yao kali ya ‘unbeaten’ kwenye mechi 49, waliyoiandika katika kipindi cha kuanzia msimu wa 2020-21 mpaka 2022/23,

Share this:

By Joel Thomas

Joel Thomas is a Tanzanian sports writer with a BSc (Education) from Mwenge Catholic University. He spent 4 years at Global Publishers and is in his second year with SportPesa, covering football and betting education for local fans. Anapenda soka na anaandika kwa uwajibikaji.