- Wakati Ligi Kuu Bara (NBC Premier League) ikiwa katika mzunguko wa 18, huku baadhi ya timu zikiwa na viporo.
- Yanga SC imeendelea kutikisa kwa rekodi nyingi bora msimu huu, miongoni mwa rekodi hizo ni ile ya Yanga SC unbeaten mechi 17, yaani kuwa miongoni mwa timu 2 tu, ambazo hazijapoteza mchezo wowote.
- Katika misimu ya hivi karibuni, Yanga SC imekuwa na unbeaten tofauti ikiwemo rekodi ya mechi 49 bila kufungwa, ambapo walivunja rekodi ya Azam FC ambao wamewahi kucheza mechi 38 bila kufungwa.
Ligi Kuu Bara (NBC Premier League) ipo katika mzunguko wa 18, huku baadhi ya timu zikiwa na viporo. Mpaka sasa Yanga SC imeendelea kutikisa kwa rekodi nyingi bora, miongoni mwa rekodi hizo ni ile ya Yanga SC unbeaten, yaani hawajapoteza mchezo wowote. Ni timu mbili tu, mpaka sasa kwenye ligi ya NBC hazijapoteza mchezo Yanga SC na Azam FC. Makala hii inachambua baadhi ya rekodi na takwimu hizo.
SOMA HII PIA: Ratiba ya Yanga SC 2025/26 ni moto | Mechi 5 NBC Premier League ugenini | Msimamo, matokeo
Bado hujashinda na SportPesa? Cheza mchezo wa aviator ‘Kindege’ uvune mamilioni sasa
Sasa ni zamu yako, unaweza kushinda hadi milioni 800 kwa raundi moja tu, muda huu. Cheza mchezo wa ‘aviator’ maarufu kama Kindege. Kushiriki mchezo huu bonyeza picha hii chini.

Yanga SC unbeaten mechi 17, Pointi 41, ushindi 12, sare 5
Kwa mujibu wa takwimu za ligi, Yanga SC amba oni mabingwa watetezi wa mashindano hayo mpaka sasa wamecheza mechi 17 bila kupoteza. Yanga SC wameshinda mechi 12 na kutoka sare mechi 5 tu. Hii inawafanya kukusanya pointi 41 ambazo zinawapa jeuri ya kuongoza ligi, pengo la pointi 6 dhidi ya wapinzani wao wa karibu Simba SC.
Yanga SC imefunga mabao 35, na kuruhusu mabao 3 tu

Katika mwenendo huo wa mechi 17, safu ya ushambuliaji ya Yanga SC imeonekana kuwa na moto wa hatari kwani mpaka sasa imefunga mabao 35. Katika kuonyesha kweli wamejipanga kutetea taji lao, Yanga SC pia imekuwa ngumu kufungika wakiruhusu mabao 3 tu. Hii inaonyesha uwiano bora wa safu ya ulinzi na ushambuliaji ya timu hiyo.
Matokeo ya Yanga SC msimu huu

April 4, 2026 Yanga SC 3-0 Tanzania Prisons
March 21, 2026 Mtibwa Sugar 1-1 Yanga SC
March 18, 2026 TRA United 0-0 Yanga SC
March 15, 2026 Azam FC 0-0 Yanga SC
March 12, 2026 Tanzania Prisons 0-1 Yanga SC
March 5, 2026 Singida Black Stars 0-3 Yanga SC
March 1, 2026 Yanga SC 0-0 Simba SC
Feb 25, 2026 Yanga SC 5-0 JKT Tanzania
Feb 22, 2026 Namungo 0-1 Yanga SC
Jan 27, 2026 Yanga SC 3-1 Dodoma Jiji
Jan 19, 2026 Yanga SC 6-0 Mashujaa
Dec 7, 2026 Coastal Union 0-1 Yanga SC
Dec 4, 2026 Yanga SC 2-0 Fountain Gate
Nov 9, 2026 Yanga SC 4-1 KMC
Oktoba 28, 2026 Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar
Sep 30, 2026 Mbeya City 0-0 Yanga SC
Sep 24, 2026 Yanga SC 3-0 Pamba
Matokeo haya yanaonyesha kuwa hata katika michezo migumu, Yanga wamekuwa na uwezo wa kuepuka kupoteza mchezo. Zaidi sana wameweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kuvuna pointi nyingi, zaidi kulinganisha na wapinzani wao. Hii inawafanya kuwa kwenye nafasi nzuri, ya kuweza kushinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya 5 mfululizo.
SOMA HII ZAIDI: Yanga SC: Historia, Usajili wote, kikosi, Ratiba, Matokeo na Takwimu
Nguvu ya kikosi na safu ya ushambuliaji
Kama ilivyoelezwa hapo awali, takwimu zinathibitisha kuwa kikosi cha Yanga SC ndio timu yenye safu bora zaidi ya ushambuliaji. Mabao 35 yaliyofungwa na wachezaji wa timu hiyo, yanakuwa mengi zaidi kufungwa na timu msimu huu. Baadhi ya mastaa wenye mabao mengi ni, Prince Dube, Zouzoua Pacome na Laurindo Depu.
Ulinzi imara na nidhamu ya timu

Moja ya siri kubwa ya mafanikio ya Yanga SC msimu huu ni uimara wa safu ya ulinzi. Kuruhusu mabao matatu pekee katika mechi 17 ni rekodi bora sana, na inaonyesha nidhamu ya hali ya juu ya safu yao ya ulinzi na timu nzima katika kutimiza majukumu yao uwanjani. Muhimili mkubwa ukiwa ni kipa, Djigui Diarra ambaye kwa sasa anakosekana kwa michezo 3 baada ya kufungiwa na Kamati ya saa 72.
Unaikumbuka Unbeaten ya mechi 49

Katika misimu ya hivi karibuni, Yanga SC imekuwa na mwenendo mzuri sana. Hii ni pamoja na kuwa na mfululizo mrefu wa mechi bila kupoteza katika ligi na mashindano mengine, ikumbukwe Yanga SC ndio wanashikilia rekodi ya unbeaten ya mechi nyingi zaidi kwenye Ligi Kuu Bara. Kati ya mwaka 2020 hadi 2023 walicheza mechi 49 bila kufungwa, rekodi hii ilivunja rekodi ya Azam FC ambao wamewahi kucheza mechi 38 bila kufungwa. Unbeaten nyingine ni ya mechi 25 za Kombe la Shirikisho la CRDB Federation na ile ya mechi 47 za nyimbani.
SOMA HII PIA: Yanga SC vs Tanzania Prisons NBC Premier League: Live Score, line up, h2h, Diarra ‘Out’ Damaro ‘in’ Taarifa za timu
Hitimisho
Rekodi ya Yanga SC unbeaten ni miongoni mwa vitu ambavyo vinawafanya mashabiki wa timu hiyo kujivunia timu yao. Kwa ujumla, Young Africans SC wamekuwa na msimu wa kipekee, katika NBC Premier League 2025/2026. Msimu huu umekuwa na tamu na chungu mbalimbali, lakini uongozi wat imu hiyo umeonyesha ukomavu mkubwa, wa uvumilivu na kubaki na mshikamano wa Pamoja. Ni wazi iwapo wataendelea na kiwango hiki, Yanga wako kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao na kuandika historia nyingine kubwa katika soka la Tanzania.

